Watz wangapi wanaifikia jf?Upo kazini hapa kujaribu kuzuia ukweli. Sidhani kama utaweza. Mkuu Wa ulinzi na usalama WA mkoa kanaswa
Sehemu pekee ya kumuhukumu kwa waki na yeye kujitetea ni kwenye social media huko kwingine wako busy kujaribu kufunika kombe ili....
Kwahiyo akiendelea kukwepa itakuwaje?imeshaonekana anakwepa kwanini gwajima sasa asiutoe huo ushahidi sheria ifuate mkondo wake?Huyu ni Mkuu Wa mkoa ndugu NN
Angeambiwa anaendesha gari pasipo leseni naamini angeweka copy ya leseni yake kuonyesha honesty
Kuhusu hili angeweza pia kuweka cheti chake hata kama kina D Tatu kikionyesha majina na Shule aliyosoma then kama alibadiri jina Fulani ataeleza lakinj hapa pasipo ushahidi Gwajima na wengine wamaeleza jambo husika kwa mlolongo ambao ingekuwa anapakaxiwa angeukanusha kwa urahisi zaidi.
Afanyeje wakati Gwajima ansobekana yuko well informed kuhusu mbinu akizotumia kufanikisha uhalifu wake na kuna mengine aweza kuwa ameyahifadhi akimsuburi kanushe.
Waandishi wanamhoji yeye anawatuma kwa baba yake !
Hivi unategemea mtu atoe ushahidi wa kumfunga mwenyewe? Si kuna mtu anadai ana ushahidi dhidi ya makonda ofisini kwake kwanini asiutoe kwenye mamlaka husika sheria ichukue mkondo wake?Hoja sio nilitaka wafanye nini bali hoja ni kwamba wahalifu wote hutumia hoja ya kudai ushahidi ili kufifisha tuhuma dhidi yao na si kwamba huwa wanadai ushahidi kwavile wanafahamu wapo clean... la hasha!!!
Hivi unategemea mtu atoe ushahidi wa kumfunga mwenyewe? Si kuna mtu anadai ana ushahidi dhidi ya makonda ofisini kwake kwanini asiutoe kwenye mamlaka husika sheria ichukue mkondo wake?Hoja sio nilitaka wafanye nini bali hoja ni kwamba wahalifu wote hutumia hoja ya kudai ushahidi ili kufifisha tuhuma dhidi yao na si kwamba huwa wanadai ushahidi kwavile wanafahamu wapo clean... la hasha!!!
Akabidhi kwa nani na kwa amri ya nani?Kama na yeye ni Mtanzania hakuna hoja ya kujadili. Lakini kama ni Mtanzania hoja ipo. Akabidhi vyeti!
Ndiyo inawezekanaKwahiyo inawezekana raia kwenda polisi au mahakamani kufungua kesi dhidi ya makonda kwa kosa la kufoji vyeti?
Kwanini atoe ushahidi wa kumfunga mwenyewe?! Kama sio fraud hana sababu ya kuhofia kwa sababu ushahidi atakaoutoa hautakuwa na shaka yoyote!!Hivi unategemea mtu atoe ushahidi wa kumfunga mwenyewe? Si kuna mtu anadai ana ushahidi dhidi ya makonda ofisini kwake kwanini asiutoe kwenye mamlaka husika sheria ichukue mkondo wake?
Mimi sio mwana sheria lakini kufungua kesi; sidhani kama inawezekana! Labda useme kupeleka vielelezo kwenye mamlaka lakini sio kufungua kesi! Forgery ni jinai na kesi ya jinai ni ya jamhuri!! Kwahiyo labda useme mtu binafsi anaweza kupeleka vielelezo ili Jamhuri ndio wafungue kesi dhidi ya mtuhumiwa!!
PorojoJamaaa sijui anauchawi gani.kumbuka mama Ane kilango alipokosea akatumbuliwa palepale .yule jamaa wa Tanesco akatumbuliwa .Kitwanga akatumbuliwa na wengine wengi lakini huyu yupo jijini na vyeti feki anadunda na Rais amfanyi chochote na inawezekana kaishapigiwa simu yakumtia jeuri kabisaaa
Nianze kwa kusema tu kuwa mimi ni mbeba maboksi nisiyejua mengi hususan kwenye hiyo fani ya 'wasomi' wabobezi [wanasheria] ambao ndiyo majiniasi wetu wenye kuongea Viingereza hatari lakini salama. Nimeishia kidato cha nne tu. Kwa hiyo msinihoji sana kuhusu elimu yangu. Ni ndogo sana.
Sasa hapa nilipo na ujinga wangu huu najiuliza maswali kadha wa kadha na sipati majibu.
Hivi kinachodaiwa dhidi ya Makonda ni kosa la jinai?
Kama ni kosa la jinai na kama kweli ushahidi upo, tena ambao ni wa kutosha na kuridhisha kabisa, kwa nini hao watu waolizitoa hizo tuhuma hawaendi kumfungulia kesi mahakamani?
Au haiwezekani kwa raia kwenda kufungua kesi mahakamani kwa manufaa ya umma dhidi ya kiongozi?
Manake mpaka sasa kilichopo au niseme ambacho nakijua mimi kupitia hii mitandao ya kijamii ni maneno tu kuwa Paul Makonda si jina lake halisi.
Jina lake halisi ni Daudi Bashite. Lakini sijaona ushahidi wowote ule uliotolewa na hao watuhumu unaothibitisha hizo tuhuma zao.
Sasa maneno tu peke yake si ushahidi wa lolote maana mtu yeyote yule anaweza kuzua lolote lile dhidi ya yeyote yule kwa sababu yoyote ile.
Nyie 'wasomi', hivi kweli haiwezekani kwenda kumfungulia mashitaka huyo Paul Makonda kama kweli ushahidi wa yanayosemwa dhidi yake upo?
Si mumburute tu mahakamani huko akaaibike rasmi. Au ni majungu tu?
We kweli mbeba mabox. Labda nikuulize, kwa nini serikali ilikuwa inakagua vyeti vya wafanyakazi? wengi walikutwa na feki etc, na kufoji, kilichotokea ni nini? waliachishwa kazi etc? etc?
Gwajima keshaonyesha vyeti alivodai anavyo?
we ni mbeba mabox, siwezi kuendelea kukuelewesha.
Basi imefikia wakati wanaomshutumu makonda kufanya hivyo kwa sab mwenyewe kakataa
Tuassume amefoji kweli ndio maana hataki kuonyesha vyeti hadharani ili kumlazimisha aonyeshe yeye mwenyewe lazima mtu aende mahakamani na ushahidi. Inawezekana gwajima amekamatwa in connection with bashite scandal lkn siamini siku zote hizo alikaa na ushahidi bila kuutoa copy na kuhifadhi sehemu nyingine mbali mbali na kama alifanya hivyo mtu mwingine yeyote anaweza kufungua kesi hata gwajima akifungwa maisha mradi ushahidi upo salama haki itatendeka tu wakati umefika sheria imlazimishe kuhakiki vyeti.Kwanini atoe ushahidi wa kumfunga mwenyewe?! Kama sio fraud hana sababu ya kuhofia kwa sababu ushahidi atakaoutoa hautakuwa na shaka yoyote!!
Kwanini anayedai ana ushahidi hajautoa tayari mwenyewe ameshasema anasubiri nini!!! But look, ndo huyo tumeambiwa ameshakamatwa na sijui kama ameshaachiwa!! Hivi kwa akili za kawaida atakuwa amekamatwa kwa kosa lipi? Dawa za kulevya tena?! Hivi hao hao wanaomkatama possibly kwa sababu ile ile bado unaamini ni watu sahihi kuwapelekea huo ushahidi?!!!
Mwenye wajibu wa kuthibitisha tuhuma huwa ni nani kwani?
Mtuhumu au mtuhumiwa?
Nielimishe mie mbeba maboksi aka ex-mla vumbi na mkanyaga tope😀.
Taratibu haziruhusu kuanzisha uchunguzi wa cheti cha mtu kwa sab ya tuhuma za mtandaoni au mtu fulani kupitia mtandaoni.