Kama ndivyo, kuna shida. Kubwa!

Kama ndivyo, kuna shida. Kubwa!

Leo, nimemuona na kumsikia Wakili Msomi mwenzangu Peter Kibatala (kupitia video clip) akizungumzia uhalali wa barua iliyotumika kufungia makanisa yanayoongozwa na Askofu Gwajima.

Kwa mujibu wa Kibatala na muktadha wa mazungumzo yake ndani ya Mahakama Kuu kule Dodoma, Kanisa lililofungiwa lilijaribu kukata rufaa juu ya uamuzi huo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani kwa mujibu wa sheria.

Kibatala akaeleza kuwa Waziri husika ametamka kuwa barua husika, pamoja na mambo mengine, SI HALALI. Waziri amesema kuwa hakuna rufaa ya kuishughulikia kwakuwa barua ni batili na uamuzi uliobebwa humo ni batili.

Barua inayosemwa ni batili/si halali ndiyo iliyotumiwa na mamlaka za kiserikali wakiwemo polisi kutekeleza kinachobebwa na barua hiyo. Makanisa Dar es Salaam na Mbeya (penginepo sifahamu) yamefungwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi.

Tumeona na kusikia kuhusu hili. Sasa, imewezekanaje barua batili/isiyo halali kusababisha kufanyika kwa yote haya? Nani huyu aliyeghushi barua hii na kusababisha yote haya? Amefanya haya kwa faida ya nani?

Kama hivyo ndivyo, tupo kwenye tatizo kubwa. Sana! Serikali itusaidie kubaini jambo hili na kukomesha kujirudia kwa jambo kama hili.
Acha ujinga
 
Polisi wetu walikurupuka! Lengo tu ni kuwafurahisha watawala.
 
Kama hivyo ndivyo, tupo kwenye tatizo kubwa. Sana! Serikali itusaidie kubaini jambo hili na kukomesha kujirudia kwa jambo kama hili.
SERIKALI NDIYO INAFANYA HAYA YOTE, ACHA KUJIFANYA HUJUI, ACHA UCHAWA. SERIKLI INAFANYA HAYA OTE. JUZI WAMEPIGA WATU KISUTU, MULILO AKASEMA POLISI HAIJAWAPIGA WAKATI DUNIA NZIMA IMESHUHUDIA WATU WAKIPIGWA. NI SERIKALI
 
Maagizo kutoka ..........?
Hakuna chochote

Filmee imepigwa na gwaji-verse1 hakujua wapo waliomzunguka

Kilq mtu atashangaa, kanisa litafunguliwa, atapigwa surprise nyingine by the time Tunafika December nguvu zote kwisha
 
Nikuombe ufikiri.
Waziri mwenye dhamana, ambae rufaa inakatwa kwake, barua batili imetumika kutekeleza amri batili. Wanaotekeleza amri batili wanaitika ultimately kwake.
Kwakua amegundua ubatili wa barua, alipaswa afanye nini? Amekifanya alichopaswa?
Kitu pekee amefanya ni kukataa kuendelea na rufaa kwasababu ya ubatili wa amri, vipi kuhusu ubatili aliougundua ikiwa yeye ndo waziri mwenye dhamana?

..Waziri wa Mambo ya Ndani na Igp wanapaswa kujiuzulu kutokana na kadhia iliyosababishwa na watendaji walioko chini yao.

..NRNE!!
 
Kama ndiyo, Kibatala naye kaenda kufungua kesi dhidi ya nani na kulalamikia nn iwapo barua siyo halali?
Ulijipa nafasi ya kumsikiliza Kibatala?
Kama SIVYO jipe nafasi ya kumsikiliza kidogo Ndio uje ucomment! Nchi imekua banana republic, Yale Yale aliyoyasema Josephat Gwajima Ndio hayo hayo yametokea.

Kwakua Jeshi la Polisi lilijinasibu Kwa mbwembwe na pia mkuu wa Wilaya alijinasibu Kwa mbwembwe kusimamia maagizo yaliyotolewa na serikali, Kwa maana ya kulifungia kanisa, walijiona wako sahihi, Kwa kuwa hakuna clear coordination sababu ya kufanya mambo bila kuzingatia utawala Bora.

Kibatala hajashitaki sehemu yoyote au mtoto yoyote. Muliro alikaza fuvu na kusema kwamba ikiwa kama kanisa inahisi haijaridhika na maamuzi ya serikali kufunga kanisa na wao askari kulizingira kanisa basi wakate rufaa Kwa aliyeweka zuio ambaye ni waziri Kwa mujibu wa barua iliyokua in circulate kwenye mitandao.

Kibatala kama wakili ndiye aliyepewa jukumu Hilo, na Kwa kuzingatia kwamba polisi wanashuoaza shingo na Msando naye anashupaza kipara kwamba kanisa lilikua served with a letter of suspension of services, Kibatala aliomba hiyo barua Ili aitumie kukata rufaa kuonesha kutokurudhika na maamuzi yaliyotolewa na Msajili.

Kwakua barua ya kwanza haikua na sahihi, ya pili haikua na sahihi Ila haikutaja majina ya kanisa Kwa ukamilifu na usahihi, na aibu inayoendelea kulikumba taifa kutokana na wajinga kushika madaraka, waziri wa mambo ya ndani ya nchi haraka amekana barua hiyo kwamba haijatokea wizarani kwake hivyo Kibatala kuonekana anakata rufaa ya hukumu au agizo ambalo halipo.

Kama nchi inaweza kuwa na kikundi Cha wajinga na wapumbavu ambao wanaweza kuandika barua yenye official seal of the state tena yenye Amri, na polisi na mkuu wa Wilaya wakaifanyia utekelezaji bila kuhoji au kujiridhisha it's authenticity, ujue Hilo taifa mambo yake katika uongozi yanaenda arijojo.

Watu wajinga walioshika madaraka hufanya mambo ya kijinga kuonesha kwamba Wana nguvu na madaraka.
 
Ni mimi sijaelewa au watu wameamua kutazama upande mmoja?
Baada ya waziri kusema sio halali, ametoa maelekezo gani? Ameeleza nini kifanyike? Ameeleza hatua zinazochukuliwa na wizara juu ya hilo?
Kama hakuna alichosema, then hiyo ni punch usoni kwa Kibatala ili kusiwe na rufaa, maelekezo ya barua yaendelee kutekelezwa.
Ndio maana kama barua si hali hivyo hakuna rufaa yakushuhulikia.

Naona watu mmejikita kivingine kabisaa
Rufaa ikifanyika kwa haki itarudishia waumini na kiongozi wao haki yao. Ndio maana imepigwa juu kwa juu.
Afadhali umesema we nikichwa panzi huelewi
 
Ulijipa nafasi ya kumsikiliza Kibatala?
Kama SIVYO jipe nafasi ya kumsikiliza kidogo Ndio uje ucomment! Nchi imekua banana republic, Yale Yale aliyoyasema Josephat Gwajima Ndio hayo hayo yametokea.

Kwakua Jeshi la Polisi lilijinasibu Kwa mbwembwe na pia mkuu wa Wilaya alijinasibu Kwa mbwembwe kusimamia maagizo yaliyotolewa na serikali, Kwa maana ya kulifungia kanisa, walijiona wako sahihi, Kwa kuwa hakuna clear coordination sababu ya kufanya mambo bila kuzingatia utawala Bora.

Kibatala hajashitaki sehemu yoyote au mtoto yoyote. Muliro alikaza fuvu na kusema kwamba ikiwa kama kanisa inahisi haijaridhika na maamuzi ya serikali kufunga kanisa na wao askari kulizingira kanisa basi wakate rufaa Kwa aliyeweka zuio ambaye ni waziri Kwa mujibu wa barua iliyokua in circulate kwenye mitandao.

Kibatala kama wakili ndiye aliyepewa jukumu Hilo, na Kwa kuzingatia kwamba polisi wanashuoaza shingo na Msando naye anashupaza kipara kwamba kanisa lilikua served with a letter of suspension of services, Kibatala aliomba hiyo barua Ili aitumie kukata rufaa kuonesha kutokurudhika na maamuzi yaliyotolewa na Msajili.

Kwakua barua ya kwanza haikua na sahihi, ya pili haikua na sahihi Ila haikutaja majina ya kanisa Kwa ukamilifu na usahihi, na aibu inayoendelea kulikumba taifa kutokana na wajinga kushika madaraka, waziri wa mambo ya ndani ya nchi haraka amekana barua hiyo kwamba haijatokea wizarani kwake hivyo Kibatala kuonekana anakata rufaa ya hukumu au agizo ambalo halipo.

Kama nchi inaweza kuwa na kikundi Cha wajinga na wapumbavu ambao wanaweza kuandika barua yenye official seal of the state tena yenye Amri, na polisi na mkuu wa Wilaya wakaifanyia utekelezaji bila kuhoji au kujiridhisha it's authenticity, ujue Hilo taifa mambo yake katika uongozi yanaenda arijojo.

Watu wajinga walioshika madaraka hufanya mambo ya kijinga kuonesha kwamba Wana nguvu na madaraka.
Hakika nimeamini sifa kubwa ya kuwa mwanaccm ni kujitoa akili kabisa na kuwa zuzu, Albert Msando ni mwanasheria na wakili msomi lakini kwa vile yuko CCM ameamua kuuweka makalioni usomi wake na kukubali kutumika kindezi ili kumfurahisha mteuzi.
 
Hii inatokana na Ile niliandika last time. Msimamo wa Chama, kwamba popote alipo mwanachama awe kiongozi au mfuasi lazima afuate msimamo wa Chama hata kama ni wa kijinga kiasi Gani na hata kama unavunja Sheria na Haki za watu Kiasi Gani, as long as unalinda maslahi ya chama kuendelea kubakia madarakani na huku ukihatarisha usalama wa nchi lazima kila mmoja asimamie Hilo! Kwahiyo wanaccm wamekubaliana kwenye vikao vyao vya ndani, kuuwa, kuteka, kubagaza, na kufungia Ndio njia sahihi!!
 
Very SIMPLE wanaoteka na kuua umewaona popote!?, Gwajima alisema wazi hawana weledi ila wanashirikiana na polisi. Hapahapa jamii forums, barua ya kwanza kabisa kuletwa humu ilikuwa hata sahihi hakuna, tulipohoji ghafla Moderators wakaufuta Uzi ukapotea, baada ya kama nusu saa hivi Uzi ukaachiwa tena ukiwa na barua yenye sahihi. Nilisema humu kuwa Ile barua imetoka kwa wahuni wanaoshirikiana na polisi wenye vyeo, nao wakafata maelekezo bila kujiridhisha. Mwisho wa siku serikali imeikana barua. Hakuna mamlaka yoyote ya kiserikali iliyowahi kujihusisha na Ile barua directly zaidi ya polisi na mkuu wa wilaya walioingizwa mkenge na wahuni. Ile sahihi ni fake.
Police wanatakiwa kushtakiwa ,kwa kushirikiana na wahuni kughushi nyaraka za serikali na kufanya mambo ya hovyo na kutesa wananchi bila sababu /kosa lolote ,hata kama sio leo mbeleni huko, lazima waje washitakiwe kwa matumizi mabaya ya ofisi ,kumbu kumbu zitunzwe tu
 
Kinachofanyika ni kuwapaka matope police, ili hata siku yakitokea mabadiliko wa kushtakiwa wawe police
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom