Ni mimi sijaelewa au watu wameamua kutazama upande mmoja?
Baada ya waziri kusema sio halali, ametoa maelekezo gani? Ameeleza nini kifanyike? Ameeleza hatua zinazochukuliwa na wizara juu ya hilo?
Kama hakuna alichosema, then hiyo ni punch usoni kwa Kibatala ili kusiwe na rufaa, maelekezo ya barua yaendelee kutekelezwa.
Ndio maana kama barua si hali hivyo hakuna rufaa yakushuhulikia.
Naona watu mmejikita kivingine kabisaa
Rufaa ikifanyika kwa haki itarudishia waumini na kiongozi wao haki yao. Ndio maana imepigwa juu kwa juu.
Kuna mambo kadhaa yanakupiga chenga. Ukiyaelewa, utajua nini kipo nyuma ya upuuzi huu wa serikali;
1. Barua ile inayofanyiwa utekelezaji na DC Albert Msando, Afande Muliro na Polisi wake imekuwa addressed kwenda kanisa linaitwa
The Glory Of Christ Church - GCC (hili sio kanisa linaloongozwa na Askofu Gwajima)...
2. Mpaka sasa kanisa linalodaiwa kufutiwa usajili wake lenye jina la
The Glory Of Christ Tanzania Church - GCTC maarufu kama
"Jumba la Ufufuo na Uzima" (ambalo ndilo kanisa halali linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima) halina barua yenye jina lao lakini wakati huohuo linaathirika kwa adhabu au matokeo yatokayo na barua ile ambayo siyo yao...
3. DC Albert Msando na wengine wanadai kuwa, barua halisi yenye jina la kanisa la Askofu Josephat Gwajima (GCTC) na kusainiwa na Registrar of Civil Society - Wizara ya mambo ya ndani ndugu Emmanuel Kihampa kwa ukamilifu wake wanayo wao kina DC Msando na Muliro na sababu wanayotoa (wasikilize kwa makini wanavyoongea) ni kwa kuwa
uongozi wa kanisa unadaiwa ulikataa kuipokea barua hiyo😕😕
4. At the same time, uongozi wa kanisa la GCTC unakanusha kuwa, hawajawahi kuletewa barua yao kuwataarifu kuwa hawana uhalali tena kisheria kufurahia haki yao ya kikatiba ya kuabudu kwa kuwa wamefutiwa usajili wa taasisi yao achilia mbali kukataa kuipokea hiyo barua.
Lakini kumbuka na liweke hili akilini kuwa, pamoja na yote hayo kanisa linaendelea kuathirika na adhabu wasiyohusika nayo..!!
Maswali yaliyo kwenye vichwa vya wengi ni haya:
•
Kama ni hivyo, kanisa lilienda mahakamani na kufungua kesi kwa base ipi?
• Vivyohivyo lilikata rufaa kwa Waziri kwa msingi upi au kwa kutumia taarifa/barua ipi?
• Lilitumia taarifa ya barua gani maana wao hawajafutiwa usajili..?
MAJIBU YA MASWALI HAYA NI RAHISI SANA:
1. Wewe unafikiri wangefanyeje? Maana Polisi wame trespass kwenye eneo lao, wamezuia shughuli zote zisiendelee kwa madai na taarifa potofu zilizosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vingine vya habari. Obvious huwezi kuanza kupigana nao kimwili na mtu kichaa asiyejua anafanya nini. Ni lazima utaratibu wa kudai haki yako kisheria ufuatwe Ili kuepusha athari zingine..
2. Kwa kuwa Kuna barua inayosambaa mitandaoni na ndiyo inayosemekana kufanyiwa kazi na Polisi na DC Albert Msando, unaichukua hiyo na kuitumia kama kielelezo ili kama sio halali, basi waseme wao..
3. Ndiyo maana Wakili wa kanisa, akakata rufaa kwa Waziri. Jibu la Waziri likawa very clear kuwa, haijui barua na haijatoka wizarani kwake, Kwa hiyo hawezi kuamua rufaa ambayo kesi yake haipo ofisini kwake. Bahari mzuri ni kuwa mahakama nayo imesema hivyo hivyo, kuwa, GCTC ni taasisi halali as it is for now na ambapo maana yake waendelee na shughuli zao kama kawaida...
4. Wakili Kibatala hakuishia hapo, aliwataka wasimamizi wa sheria Polisi waliohusika na vurugu hizo kanisani pamoja Wizara kupitia ofisi ya Msajili wa taasisi za kiraia waitoe barua hiyo inayowapa uhalali wa kufanya hayo wanayoyafanya kisheria..
KWA HIYO:
√ Msingi wa mchakato wote wa kanisa ni barua iliyosambaa mitandaoni na kwenye mainstream medias zote isiyowahusu lakini ikiwaletea athari hasi wao. Kama barua imekanwa na mamlaka za serikali zinazodaiwa kuitoa, basi maana yake kila kilichofanyika ni batili na wote waliofanya hayo kwa kukosa umakini, wawajibike kulipia gharama ya hasara ya mali na muda walioisababishia taasisi
√ Na hili nadhani, Afande Jumanne Muliro RPC wa Kanda maalumu DSM anaweza kuwa kwenye position nzuri zaidi kulitolea ufafanuzi. Kwa kujibu swali moja tu. Polisi wake wanafanya nini kwenye kanisa la GCTC wakati barua inawaelekeza kwenda kwenye kanisa la GCC bila kujali ni halali au siyo halali.?