Kama ndivyo, kuna shida. Kubwa!

Kama ndivyo, kuna shida. Kubwa!

Leo, nimemuona na kumsikia Wakili Msomi mwenzangu Peter Kibatala (kupitia video clip) akizungumzia uhalali wa barua iliyotumika kufungia makanisa yanayoongozwa na Askofu Gwajima.

Kwa mujibu wa Kibatala na muktadha wa mazungumzo yake ndani ya Mahakama Kuu kule Dodoma, Kanisa lililofungiwa lilijaribu kukata rufaa juu ya uamuzi huo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani kwa mujibu wa sheria.

Kibatala akaeleza kuwa Waziri husika ametamka kuwa barua husika, pamoja na mambo mengine, SI HALALI. Waziri amesema kuwa hakuna rufaa ya kuishughulikia kwakuwa barua ni batili na uamuzi uliobebwa humo ni batili.

Barua inayosemwa ni batili/si halali ndiyo iliyotumiwa na mamlaka za kiserikali wakiwemo polisi kutekeleza kinachobebwa na barua hiyo. Makanisa Dar es Salaam na Mbeya (penginepo sifahamu) yamefungwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi.

Tumeona na kusikia kuhusu hili. Sasa, imewezekanaje barua batili/isiyo halali kusababisha kufanyika kwa yote haya? Nani huyu aliyeghushi barua hii na kusababisha yote haya? Amefanya haya kwa faida ya nani?

Kama hivyo ndivyo, tupo kwenye tatizo kubwa. Sana! Serikali itusaidie kubaini jambo hili na kukomesha kujirudia kwa jambo kama hili.
Inawezekana pia mambo mengi ni yakugushi tuchukue hatua

Tanzania tuache kuongoza nchi kwa mfumo wa unyumbu wa kisiasa
 
Hii inatokana na Ile niliandika last time. Msimamo wa Chama, kwamba popote alipo mwanachama awe kiongozi au mfuasi lazima afuate msimamo wa Chama hata kama ni wa kijinga kiasi Gani na hata kama unavunja Sheria na Haki za watu Kiasi Gani, as long as unalinda maslahi ya chama kuendelea kubakia madarakani na huku ukihatarisha usalama wa nchi lazima kila mmoja asimamie Hilo! Kwahiyo wanaccm wamekubaliana kwenye vikao vyao vya ndani, kuuwa, kuteka, kubagaza, na kufungia Ndio njia sahihi!!
Iko hivi
 
Attachments

  • duh.jpg
    duh.jpg
    34.8 KB · Views: 13
  • mwe.jpeg
    mwe.jpeg
    25.7 KB · Views: 12
Very SIMPLE wanaoteka na kuua umewaona popote!?, Gwajima alisema wazi hawana weledi ila wanashirikiana na polisi. Hapahapa jamii forums, barua ya kwanza kabisa kuletwa humu ilikuwa hata sahihi hakuna, tulipohoji ghafla Moderators wakaufuta Uzi ukapotea, baada ya kama nusu saa hivi Uzi ukaachiwa tena ukiwa na barua yenye sahihi. Nilisema humu kuwa Ile barua imetoka kwa wahuni wanaoshirikiana na polisi wenye vyeo, nao wakafata maelekezo bila kujiridhisha. Mwisho wa siku serikali imeikana barua. Hakuna mamlaka yoyote ya kiserikali iliyowahi kujihusisha na Ile barua directly zaidi ya polisi na mkuu wa wilaya walioingizwa mkenge na wahuni. Ile sahihi ni fake.
Uko sahihi mkuu, hata hivyo najiuliza hizo mamlaka husika ilikuwaje zikakaa kimya muda wote wakati mamlaka nyingine zikifanya zuio ambalo si lao? Polisi tumekuwa tukisema wanatumika kulinda watu wasiojulikana lakini jeshi hilo linakataa, cha ajabu wao ndio walitumia nguvu kubwa kuzuia kwenye kanisa lile kwa barua fake!
 
Petro E. Mselewa umepotea Sana siku hizi.

Angalau sasa unaongea lugha ya kidplomasia. Sisi wengine hatuamini kwenye ule msemo wa "zimwi likujualo..." Kwenye kujihusisha na CCM.

Kutokuwepo kwa haki mahali fulani, ni kutokuwepo kwa haki kila mahali". Martin Luther king.

Tatizo kwetu sisi watanzania haki ni ile tu inayotuhusu au dhuluma ni tendo baya dhidi yetu tu ila wakitendewa wengine ni hakuna tatizo!
Yaani tunaishi kwa hisani ya CCM
 
Kama ndiyo, Kibatala naye kaenda kufungua kesi dhidi ya nani na kulalamikia nn iwapo barua siyo halali?
Polisi wanazuia kanisa kufanya ibada kutokana na hiyo barua fake mkuu.
 
Uko sahihi mkuu, hata hivyo najiuliza hizo mamlaka husika ilikuwaje zikakaa kimya muda wote wakati mamlaka nyingine zikifanya zuio ambalo si lao? Polisi tumekuwa tukisema wanatumika kulinda watu wasiojulikana lakini jeshi hilo linakataa, cha ajabu wao ndio walitumia nguvu kubwa kuzuia kwenye kanisa lile kwa barua fake!
Shida ni kwamba hicho kikundi kinachoua na kuteka na ku forge barua kinaogopeka sana. Kama ulimsikiliza vizuri Gwajima ni kwamba hata wakuu wa vyombo vya usalama wanakiogopa hicho kikundi, haki ripoti kwa yeyote, ni kama Rwanda. Wanapokea maelekezo kutoka juu, ila kuna baadhi ya watu wa polisi wanashirikiana nao ndo wanaotuma polisi kwenda makanisani na hawajali wizara inaijua barua au haijui. Ndo maana watu kama Gwajima wanahitaji kupewa support.
 
Nia ya serikali ilikuwa kweli kulifungia kanisa ila walivyoona response mbalimbali za watu wakagundua hii tumeingia cha kike,hivyo kama kawaida yao serikali hii,wanaikana
 
Shida ni kwamba hicho kikundi kinachoua na kuHiteka na ku forge barua kinaogopeka sana. Kama ulimsikiliza vizuri Gwajima ni kwamba hata wakuu wa vyombo vya usalama wanakiogopa hicho kikundi, haki ripoti kwa yeyote, ni kama Rwanda. Wanapokea maelekezo kutoka juu, ila kuna baadhi ya watu wa polisi wanashirikiana nao ndo wanaotuma polisi kwenda makanisani na hawajali wizara inaijua barua au haijui. Ndo maana watu kama Gwajima wanahitaji kupewa support.
Hao akina Gwajima nao si hata wa kuwapa support kivile, maana wakati sheria mpya ya usalama wa taifa inapitishwa alikuwa ndani ya bunge na hakupinga. Ama mkuu umesahau kuna sheria ya usalama wa taifa ambapo unaweza kushughulikia bila watu hao kuwajibishwa popote?
 
Kusema barua ni FAKE huo ni Uongo na wanatafuta Kichaka cha Kujificha, Mpaka IGP ame deploy forces pale kwenda kuhalt operation za kanisa si inamaana alipata ile barua na akatekeleza? Au tafsiri yake ni kuwa hata copy ya IGP nayo ni fake aliyopewa? Ina maana kuna watu wanawez kuwasiliana na Jeshi la Polisi tena Ofisi ya IGP kwa Mawasiliano fake? yani Polisi wameshindwa kufanya authentication ya barua waliyopewa kama ni Legit

Mbona inatisha sasa
 
Tulipokuwa tunasema kuhusu wanaoteka watu na hadi watu wana details zao watu waliona ni maigizo.

Sasa kama mkuu wa wilaya wanavyoitwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya anaulizwa una details za utekaji wa mwananchi wako anajibu" No Comment" sasa nani aulizwe na nani ajue.

Na akiitwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama hataki kabisa kuitwa hivyo .
 
Leo, nimemuona na kumsikia Wakili Msomi mwenzangu Peter Kibatala (kupitia video clip) akizungumzia uhalali wa barua iliyotumika kufungia makanisa yanayoongozwa na Askofu Gwajima.

Kwa mujibu wa Kibatala na muktadha wa mazungumzo yake ndani ya Mahakama Kuu kule Dodoma, Kanisa lililofungiwa lilijaribu kukata rufaa juu ya uamuzi huo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani kwa mujibu wa sheria.

Kibatala akaeleza kuwa Waziri husika ametamka kuwa barua husika, pamoja na mambo mengine, SI HALALI. Waziri amesema kuwa hakuna rufaa ya kuishughulikia kwakuwa barua ni batili na uamuzi uliobebwa humo ni batili.

Barua inayosemwa ni batili/si halali ndiyo iliyotumiwa na mamlaka za kiserikali wakiwemo polisi kutekeleza kinachobebwa na barua hiyo. Makanisa Dar es Salaam na Mbeya (penginepo sifahamu) yamefungwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi.

Tumeona na kusikia kuhusu hili. Sasa, imewezekanaje barua batili/isiyo halali kusababisha kufanyika kwa yote haya? Nani huyu aliyeghushi barua hii na kusababisha yote haya? Amefanya haya kwa faida ya nani?

Kama hivyo ndivyo, tupo kwenye tatizo kubwa. Sana! Serikali itusaidie kubaini jambo hili na kukomesha kujirudia kwa jambo kama hili.
wapiiii litapita kimya kimya kama kesi ya mzee Kibao ilivyoshughurikiwa
 
Ni serikali yenyewe ndiyo wamefanya hivi sema tu wamebainika ndiyo wanakuja na ujinga wa kusingizia watu wengine. Hii serikali ya CCM haina viongozi wenye akili sote twajuwa hili, kama tungekuwa na watu wenye akili tungewaachiaje kina Steve Nyerere, Mwijaku, Baba Levo, na Dotto Magari kuwa wasemaji wa Mama Abdul?
Kwa hiyo mama aliulizwa,Abdul akipotea halafu kesho akaokotwa ametobolewa.,...macho yaani...hakujibu kwa sababu anaongozwa kuongoza?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom