Kama na wewe hujui kabila lako, pitia hapa

sic2019

Senior Member
Oct 14, 2018
129
81
Habari zenu wadau wa JF,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza naomba niende moja kwa moja kwenye mada.

Nilipokuwa shule, mara nyingi lilipokuja suala la kutaja kabila huwa nilikuwa napata tabu sana kwa sababu najua kabisa sijui kabila langu muda mwengine nataja tu lolote ili tu ile siku ipite. Mpaka nikawa nachukia sana swali la " wewe ni kabila gani", ni bora mtu aniulize unatokea mkoa gani kuliko kuniuliza kabila langu.

Nimejaribu kuuliza kwa wazee lakini sipewi jibu kamili bali naanza kuelezewa historia ndefu kwamba babu yangu alizaliwa na mzee nani kutoka wapi huko na blah blah nyingi kama hizo mwisho wa siku bado sipati jibu kamili.

Mpaka hivi sasa nimeamua kujichagulia kabila ambalo naliona linafaa na linaendana na mkoa ninaotoka, ili kuepukana na hili swali.

Kama na wewe ni muhanga wa hili jambo kama mimi hebu nipe uzoefu wako uliepuka vipi hii situation?
 
Tuko wengi mkuu,kipindi nikiwa mdogo ilikuwa nikiuliza kabila pale nyumbani ili nijue kabila langu naona watu hawako teyari kujibu swali hilo na wengine hucheka tu. Ila baadaye ndio nikajua babu alitokaga nchi fulani ya jirani,kwahiyo tumechagua kabila fulani ndio kabila letu pale tukiulizwa kabila.

Ila hapo kabla ilikuwa nikulizwa kabila nachagua lolote tu nakutajia,binafsi sipendi kuulizana makabila unakuta mtu umeonana nae mara ya kwanza hata hamjuani vizuri ila anakuuliza kabila.
 
Ukiona mtu anaficha kabila lake kama wazee wako. Jua moja ndoa hiyo haikuwa na mapenzi ya dhati. Labda ilihusisha ubakaji na aibu nyingine. Au kabila la babaako ni la watu wasiowazuri kwani kabila ni la Baba wala si mama
 
Bora hata wewe ulijua sababu
Tuko wengi mkuu,kipindi nikiwa mdogo ilikuwa nikiuliza kabila pale nyumbani ili nijue kabila langu naona watu hawako teyari kujibu swali hilo na wengine hucheka tu. Ila baadaye ndio nikajua babu alitokaga nchi fulani ya jirani,kwahiyo tumechagua kabila fulani ndio kabila letu pale tukiulizwa kabila.

Ila hapo kabla ilikuwa nikulizwa kabila nachagua lolote tu nakutajia,binafsi sipendi kuulizana makabila unakuta mtu umeonana nae mara ya kwanza hata hamjuani vizuri ila anakuuliza kabila.
 
Kama ulitupwa na wazazi wako na ukaokotwa na wasamalia wema na kupelekwa orphanage centre nitakuelewa vema kabisa
 
Back
Top Bottom