Kama MWAKYEMBE na MAGUFULI wanafanya uhuni huu basi CCM imedhamiria kuwazika Watanzania!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama MWAKYEMBE na MAGUFULI wanafanya uhuni huu basi CCM imedhamiria kuwazika Watanzania!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paul Kijoka, Oct 30, 2012.

 1. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni jambo la kusikitisha na kushangaza kuona Watanzania wanashabikia matukio haya mawili la Basi ziendazo Kasi BRT
  (BRT) na uzinduzi wa
  Reli kwa Jiji la Dar es Salaam. Mipango hii yote inaongozwa na watu wanaojitambulisha kuwa kuwa wachapa kazi kina Magufuli na Mwakyembe.
  Ukweli kwamba ni danganya toto kwa sababu zifuatazo:

  1. Tatizo la msongamano wa magari halisababishwi na kuwepo kwa gari za abiria ( public transport) bali ni private cars na maroli.
  2. Msongamano huu unaletwa na kwenye junctions( nodes) mf. Ubungo mataa, Shekilango, Njia panda ya Tabata, Buguruni, Magomeni Mapipa,......
  na suluhisho ni fly overs.
  3. Reli hizi zinaishia pafupi sana na haziondoi au kuzuia watu binafsi kwenda na magari yao.
  4. Hakuna parking Dar na watu wengi hubakia barabarani wakizunguka wkt wengine walionao wanafanya issue zilizowaletra mjini.
  5. Upanuaji Barabara haupunguzi foleni bali hupunguza urefu wake na kutengeneza foleni fupi yenye mistari mingi ya magari mf. barabara ya Mwenge to Ubungo kupita Mcity.
  kwa msisitizo zaidi ni sawa na kuweka maji kwnye mrija wa kunywea soda ukajaa alafu na mengine ukajaza beseni na mtoto akaulizwa maji mengi yako wapi naye akachagua mrija kisa umezidi beseni kwaurefu.

  Sasa hela kubwa inayotumika kutengeneza barabara za BRT na Reli ingefanya yafuatayo kama si ufisadi:
  1. kutengeneza barabara zote mbovu za kupunguza msongamano kwemye Barabara ya Moro kwa kiwango cha lami ili kupunguza kufurika kwa magari Morogoro road mf. Barabara ya Kimara na Mbezi to Uwanja wa Ndege, Kimara na Mbezi to Tegeta........
  2. kuwekeza kwenye Fly Overs kwenye mataa yote.
  3. kuboresha na kupanua barabara hasa vituo amabvyo viko barabarani hasa mf. njia ya Tandare.


  MUHIMU: wATANZANIA tunapenda kushabikia mambo bila kuyachunguza na sasa tusubiri tuone jinsi hii mipango 2 isivyo na tija bali danganya toto.
   
 2. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wewe roho mbaya zitakuua. Mahali pa kusifiwa sifu, na mahali penye utata sema. Ukiwa kila siku negative utakuwa unaboa
   
 3. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,198
  Likes Received: 520
  Trophy Points: 280
  Hujaeleweka na mapenzi yako kwa fly over.

  Kama swala ni kupunguza msongamano unaosababishwa na magari madogo kama ulivyoandika,suluhisho ni kuimarisha usafiri wa jumuia (Public) Treni ni moja ya suluhisho hata kama unalibeza,ni kweli parking ni shida ubungo na mwakanga ? lakini hilo haliondoi ukweli kwamba treni itabeba watu wengi na kutumia nusu saa kati ya ubungo na city centre hivyo wajanja wengi watatafuta parking maeneo ya ubungo na kudandia treni,hivyo kwa namna moja watapunguza idadi ya magari madogo yaingiayo city centre.
  Badala ya kuzungumzia fly overs kwa nini tusiangalie namna ya kutumia bahari kwa kuanzisha speed boat nzuri za kusafirisha watu kwa njia ya bahari,zikiambaa na pwani ya dar es salaam zikianzia maeneo kama mbweni hadi bandalini,sababu maeneo yaletayo magari mengi sana city centre ni yote tatuniayo moro road na Ally H,Mwinyio road.
  wazo la kuimarisha njia mbadala kama mifano uliyotoa hilo ndilo lenye mshiko kuliko hayo ma fly overs.

  HIVI NI LAZIMA WOTE TUANZE KAZI SAA MBILI ASUBUHII ? kama si lazima hata kurekebisha masaa ya kazi kwa kadri ya umuhimu wa mtu na wakati ili kusihitajike watu wengi kutumia barabara kwa wakati mmoja. Wabongo karibu wengi kazi huanza saa mbili hadi saa kumi,je ni wote lazima tuanze kazi saa mbili na kumaliza saa kumi ? TAFAKARI,CHUKUA HATUA

  Umejitahidi lakini...
   
 4. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu mbona hapa we ndo unajionesha ni muhuni ?
   
 5. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,593
  Likes Received: 2,399
  Trophy Points: 280
  Mi nadhani tumpongeze, amethubutu aliahidi na sasa ametekeleza hizo flyover unazosema sidhani kama ni rahisi kama unavyotaka kutuaminisha hapa, reli kwa sasa ndio njia ya haraka kusaidia shida ya usafiri jijini........tumpigieni makofi kidogo DR jamani hata kama ni ya kinafiki.........jamaa ni waukweli.
   
 6. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,192
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  pumba tu, hata kama ni mpinzani sio kupinga kila kitu....!
   
 7. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,213
  Likes Received: 2,077
  Trophy Points: 280
  Ndg mtoa mada, lengo la treni si kupunguza msongamano wa magari mjini tu, ila kusaidia raia wanyonge wanaopata shida ya usafiri asb na jioni (peak hours) kutokana na uchache wa daladala. Muda wa jioni daladala hazifiki mwisho, hukatisha ruti kukwepa foleni, so garimoshi linasaidia kupunguza nakisi hiyo.
   
 8. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hujaelewa hoja hapa. Hizo gari moshi zina route ngapi mpaka uamini hara kwamba zimepunguza msongamano?
  Nadani huja soma posit nzima na hujafanya utafiti lkn kwanini hela iliyotumika hapo isiboreshe barabara kwanza? naseama hivyo kwakujua na kuwa na uhakika kuwa Reli kwa Tanzania bado bado sana. Kama ya kati imetushinda itakuwaje hizi hapa????? Road Transport kwanza.
   
 9. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Yaani nilipoona hiyo title nimeshtuka nilidhani wameshakomba lundo la fedha na kuzipeleka Uswisi, sasa huo uhuni uko
  wapi hapo!!
  Hayo masuala yote uliyopendekeza ni mazuri lakini hayaathiri wala kuathiriwa na mpango wa sasa, hayo ni mambo
  ambayo yapo kwenye plan za baadae!
  Ngoja basi tukiona treni letu limeharibika basi tutajua umeingilia kati mpango wa makomandoo!!
   
 10. K

  Kulya JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 339
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  He hee... We kweli Kijoka aisee... Hivi do u think Rome was built in a day?! Unajua BRT plan ilibuniwa miaka gani?! Kama hujui, ni enzi ya Sykes, akiwa meya wa Jiji, hii ya train ni mpango wa muda tu kukabiliana na msongamano wa magari, flyovers nazo zitajengwa tu mdau... Usitoe kauli za namna hiyo, kuwa hawa jamaa ni wahuni. Na nionavyo mimi wewe ndo blood-MUHUNI
   
 11. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Hizo treni mbili kati kati ya jiji hazina msaada wowote katika kutatua tatizo la msongamano wa magari Dar es salaam, watu wanashabikia na kumfanya mwakyembe popular bila sababu, ifanyike master planning mpya ya usafiri wa umma dar es salaam na suluhisho ni kuwa na trains za kwenda kasi na trams sio hayo mabehewa ya mwaka 1947
   
 12. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama nimeongelea reli tu. Lakini naomba uniambie kwa sasa kuna routes ngapi mpaka sasa sote tuwe kama matete tufuate upepo wa kupongeza? Yaani hapa namaanisha ni utafiti gani umefanywa mpaka ukagundua kuwa pale reli ilipo ndo kuna wanyonge sana na kule kwingineko maisha poa?
   
 13. G

  George Smiley JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Watu wenye mitazamao kama yako humu JF hawafiki 10 sababu kuna wazimu wa ku worship personalities bila sababu zozote za msingi. Watu hawa hawa watakwambia CCM na waliomo ndani yake hawafai next minute watakwambia ohhh lakini Mwakyembe na Magufuli wanafaa.

  Mimi nakubaliana na hoja zako zote sasa kilicho baki ni kuona hawa ma Mwakyembe/Magufuli worshippers watakavyo kuja kukutukana kuwa hoja zako dhaifu lakini usitegemee mtu kuna na analysis yoyote ile.

  Usisahau hawa wapenzi wa Mwakyembe/Magufuli wote ni CHADEMA pia.
   
 14. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Watu mmempaka sana Paul Kijoka, lakini katika undani na mantiki ya hoja yake alikuwa na hoja yenye kuhold water. Hebu someni tena uzi wake "critically" hafu muangalie kama kweli mmemtendea haki huyu kamanda. Hoja zenyewe ni hizi
  1. Mmemtendea haki kweli? Haya aloyasema hayana ukweli au umaana katika utekelezaji? guys, you must always think big and avoid being myopic. Siyo kumshambulia tu mtu bila hoja ya maana badala ya kupangua hoja kwa kutumia hoja!!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  aisee! makundi CCM yatawamaliza, heading na unachoandika havina ushirikiano kabisa,
  sijui hata unachokusudia.............punguza mhemko ndugu.
   
 16. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kumbe ulitegemea kuwa janja haitashtukiwa? lkn pia sio lazima mimi nifikirie kama wewe......!!!! Ila You will tell me after few years to come kuwa hiki ni kiini macho!!!!!!
   
 17. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mkuu hapa umenena vema kabisa na nadhani mtoa mada amekurupuka kutoa lawama zisizo na kichwa wala miguu.Lengo hapa ni kuokoa muda ambao watu wanaotumia public transport wanaupoteza kutokana na msongamano wa magari njiani.Nashangaa kwanini watu hawaishi kuleta majungu hata kwa mambo ambayo yako wazi kabisa.
   
 18. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Unamtetea bure huyo mzushi? nani aliyekuambia hizo treni zina lengo la kupunguza foleni?
   
 19. K

  K.Msese JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,467
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  Acha chuki.....wamethubutu na wameweza.......!
  • Kama una huruma na hela iliyotumika achilia mbali haijaingia mfukoni mwao, kwanini usihoji fedha zilizopo katika mabenki uswis zisirudishwe na wahusika wenyenazo wauwawe?
  • Duniani usafiri wa treni ndio maarufu kama daladala za hapa....London wanatumia achailia mbali miji mikuu kibao kote duniani.
  • Wao wameamua kuanza na hayo walioanza nayo......kama kuna wazo au njia ingine tofauti na hii ya reli na BRT kwanini tusiwape nafasi na kuwapongeza kwa hili la awali.....!
  • Kwanini usitoe wazo kuwa, wizara zinde mikoani na hapa Dar es Salaam zibakie wizara nyeti tu. Mfano; Wizra ya Afya Dodoma, Elimu iende Lindi, Kazi ajira na Vijana Singida, Malia asili na Utalii Zanzbar, Maji Shinyanga, kilimo Kigoma nk. Sasa Tuone wangapi watakaa mjini.

  Wewe mleta huu uzi, ungekuwa jirani yangu lazima ningeku-mabwepande tu. Hao uliowataja ni majembe, hata kama wanaiba kazi tunaona, sio kama ilyekutuma ambaye anaiba 90%, halafu iliobaki ndio anawekeza kwenye mradi uliokusudiwa.

  Kibanga Msese
   
 20. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Yeye alianza vibaya uzi wake! alitakiwa kwanza apongeze juhudi zilizofikiwa halafu atoe changamoto zinazoikabili
  hiyo secta ya usafiri hapo Dar! lakini kaanza kwa kupayuka na lawama tu, ndio ukaona wanajamii wanamzonga!!!
   
Loading...