Khantwe
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 61,180
- 124,849
Habari ya wakati huu Great Thinkers.
Leo naomba niongee kidogo na wadogo zangu wa kike, (kama mtu mzima mwenzangu unafanya haya tafadhali acha mara moja).
Hivi karibuni niliangalia muvi moja hivi ya kiswahili (bongo muvi)....nilijikuta natumia wiki nzima kufikiria kile nilichokiona.
Kwa kifupi ni kwamba alikuwepo huyo mrembo anakwenda kwa jina la Jack, wakatokea wakaka wa mtaani kwao wakawa wanamtongoza, alichokuwa anawajibu sasa, 'huna hadhi ya kuwa na mrembo kama mimi', mkome kunifuatilia nyie vinuka-mkojo, wachafu kuoga' na mengine mengi ya dharau nimeyasahau.
Kifupi maneno hayo yaliwakera sana wale vijana lakini hawakuwa na la kufanya (watafanyaje sasa, shule hawana, pesa inawakimbia).
Ila mmoja kati yao alijua cha kufanya, akaenda kwa mjomba wake kuomba mtaji, akapewa na akazalisha vya kutosha akawa young bilionea.
Alichofanya alitumia kila mbinu (na kusema kweli alitumia nguvu kubwa) hadi akampata yule dada, akatoa posa na tarehe ya ndoa ikapangwa.
Siku chache kabla ya ndoa akamshawishi dada wakazini (bahati mbaya au nzuri mdada wa watu alikuwa bikra) na mimba ikaingia.
Ilipofika siku ya harusi yule kijana hakutokea kumbe amepanda zake ndege, ameenda nje ya nchi kupumzika.
Lengo lake la kumkomoa mdada likawa limetimia.
Sitaelezea mbele ilikuwaje maana siko nilikotaka kuzungumzia.
Kwanza naomba kujifunza kwenu wadada, ni kwa nini huwa mnatumia maneno ya shombo au matusi kukataa watu?
Mbona kuna majibu ya kistaarabu yanayoeleweka? Mdada anamtukana mkaka wa watu hadi anajiona useless yeye,wazazi wake na ukoo wake wote kisa nini?
Msifanye hivyo bwana, kuna watu wana roho za visasi shetani anaomba poo. Sina hakika kama kwenye maisha yetu halisi mtu anaweza kulipa kisasi kwa kiwango hiki ila mimi ninachojua ni kwamba VISASI VIPO!
Mtu anaweza akakomaa na wewe miaka kadhaa kwa lengo la kulipa kisasi tu, akudhalilishe kama wewe ulivyomdhalilisha.
Hata kama mtu yupo below your standards Mjibu kistaarabu tu....mwambie nina mchumba (hata kama huna), ukamweleza kuwa hujavutiwa nae kwa namna ya kiungwana au sababu zingine unazoona wewe zinafaa.
Haya maneno ya dharau yanaweza kukukost ukajuta maisha yote.
Lakini na ninyi kaka zangu niwaambie kitu, mapenzi ya mwanamke yanazaliwa na kukua kulingana na mazingira.
Mwanamke anaweza asikupende wakati unamtokea kwa mara ya kwanza lakini ukafanikiwa kumshawishi akupende.
Mimi nimeona watu huwa wanatukana mitusi ya nguoni (na wanakuwa wanamaanisha kweli) lakini mwisho wa siku wanakuja kuolewa na wanaume haohao tena wakiwa wanawapenda kwa dhati kabisa.
Kama mtu alikutukana baadae akakupenda samehe yaliyopita msonge mbele.
Thanx (Nimekopi hii swaga)