Kama mikataba hii ya rasilimali ni siri, mbona mahakama za kimataifa hazifanyi mjadala wa siri? Kwanini watawala waendelee kufanya siri?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
882
4,125
Kuna kaukimya fulani kanatawala hapa nchini kwa watawala wa chama cha mapinduzi kujitenga kabisa na kile kinachotokea mahakama za kimataifa.

Magufuli nakubaliana naye kwamba alichokifanya yeye ilikuwa kutuondoa kwenye hii mikataba ili tuanze upya na mikataba yenye manufaa kwa umma. Wakati huo huo ilikuwa agenda ya CCM; leo tumeanza kupigwa za uso hakuna mwanaccm anayesema hi ni agenda yake.

Kama kufilisiwa siyo agenda ya chama tawala ni agenda ya nchi kwanini issue ya uingiaji mikataba isiwe pia agenda ya nchi? Kwamba kwa kuwa kila mtu atalipa deni basi tukubaliane kwamba kila mkataba wa rasilimali tutaupitisha wote na tukipata hasara tutalipa wote. Tunaingia mikataba kwa siri lakini kwenye kulipa na kujadili hii mikataba siyo siyo. Tuwekeni wazi.

Tumebaki kuulizana nani kavujisha kumbe jambo lenyewe wale siyo siri ni jambo lipo wazi mbele ya mahakama ; nashauri tuweke wazi haya mambo tuachane na maisha ya 1960 kila kitu siri.
 
Profesa mzima anachokonoa meno tena kwa vidole mbele za watu huku akiishika shika hovyo pete yake kiufupi alikua kama tumbiri katikati ya maonesho!

Huyo ni profesa je akina Hamza Johari na mitumbo yao watafanya nini mbele ya meza ya makubaliano?

Hii nchi ina watu wa hovyo sana!
 
Huko mahakamani tunafika maji yakishamwagika. Hapa kabla wanafanya siri ili wapitishe, hata wao nasfi zao zinajua kuwa wanasaini upumbavu. Kuficha aibu wanafanya siri. Alafu leo wanamtuma profesa wa watu akatetee upuuzi, anaishia kujikanyaga tu.
 
Kuna kaukimya fulani kanatawala hapa nchini kwa watawala wa chama cha mapinduzi kujitenga kabisa na kile kinachotokea mahakama za kimataifa...
Uangalie mkataba wa DP ndiyo utajua kwanini ni Siri. Kule Iko wazi kwakuwa wanapaswa kuamua.
 
Back
Top Bottom