Kama mambo yenyewe ndio haya bora niitwe bahili tu...

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,011
Habari za usiku huu ndugu.

Kwenye maisha haya ya kiliberali ili yasonge mbele kila mtu anatakiwa aishi vile anavyotaka. Kimjini mjini wanasema kila mti kimpango wake. Yaani unaishi bila kuuliza uliz maswali ya nani anaishi vipi anakukaje. Sasa jama ndio hivi okay poa tusisimbuane.

Hapa nina funzo kwa vijana, wazee mmeshapitia mengi hata ukijifunza leo haisaidii kitu. Kama kupata umeshapata na kukosa ushakosa. Nimekuwa na marafiki wengi wenye msaada na wale wa kupita tu. Mradi maisha yaende. Baadhi tabia zao zinanikera. Mtu anatafuta pesa zake kwa jasho lake, sawa! Ofcourse huwezi kumpangia mtu atumieje.

Akishakupata pesa yake anakula bata, kesho yuko na demu yule. Keshokutwa yuko Beach Hotel. Inafika jumapili anakupigia simu umtoe buku teni ya umeme. unamshangaa huyu vipi? Pesa zake yeye ale bata ila ya umeme umnunulie wewe? Mwingine naye yeye chapombe tu. Tena mwanamke. Ana kazi ya kupata hela daily lakini anapopata mchongo mzuri basi Bar kali kali zitamkoma.

Wakati sisi na maumivu ya tozo na vyuma kukaza chini ya Mh Rais Mama Samia Suluhu Hassan na ajira ngumu tunabajeti ili siku zisonge. Sasa Kodi yake imeisha ameniganda kama ruba. Sipumui. Si hemi utadhani hiyo nyumba yangu. Ofcourse anajua kama nina hela a uwezo wa kumsaidia ninao lakini nawaza.

Mimi zangu nazipata kama anavyopata yeye. Naweza mahesabu natumia kwa vitu vya msingi. Bata napunguza. Pesa zake ake bata ila kodi ya nyumba nimchangie mimi?

Kama ntaitwa bahili sawa tu na wacha ikae hivyo hivyo. Ila ujinga sitakagi mimi.
 
Wanakera hao rafiki,, kuna mmoja alikuja analia kabisa nilivyomkopesha amenipa mgongo kama sijamkopesha kabisa hawana habari hao marafiki,,, jamani hizi pesa tunatafuta kwa jasho na damu

Kwa sasa hivi boro kukosana tu ieleweke tu
 
Najua atakuwa malaya wako tu huyo

Hahah we jamaa, hebu msome tena mwanahisabati...

Jamaa anatupigia stori juu ya washikaji zake walivyo mawaki, wanatumbua pesa halafu wanaishi kama digidigi kwa kuomba hisani ya vitu kama LUKU...

Jamaa ndio anatushauri tuwateme tu wakuda wote wenye uduanzi kama huo
 
Kama ni mwanamke anataka hela ya kodi wewe mpe tu baraka zitakuja huwezi juwa anapitia yapi usiyoyajuwa.

Huo ndo ushikaji mzuri wa kumsaidia wakati wa shida.😉
 
Hasa ndugu huoni njia nyepesi io ya wewe kufanikiwa zaidi, tumia wajinga ambao hawana nidhamu na pesa zao kukuza kipato chako, unataka zari gani la mentali.

Akili kichwani ndugu
Kuna mwanangu alikuaga anabugia sana mapombe na kula pisi kali, akipata mshahara haukai wiki umekata halafu anaishi kama digidigi... Alikua anakuja kwangu kulia lia shida, nikampa conditions awe ananipa ATM card yake halafu mm namkopesha kwa riba, mshahara ukitoka nachomoa ela yangu namrudishia ATM card yake... Nilinufaika sana na kale kautaratibu mpaka alipohama ule mkoa!!!
 
We jamaa unatumia madhaifu ya wenzako kujinufaisha binafsi?
 
Hasa ndugu huoni njia nyepesi io ya wewe kufanikiwa zaidi, tumia wajinga ambao hawana nidhamu na pesa zao kukuza kipato chako, unataka zari gani la mentali.

Akili kichwani ndugu
🤣🤣🤣how?
 
Kama ni mwanamke anataka hela ya kodi wewe mpe tu baraka zitakuja huwezi juwa anapitia yapi usiyoyajuwa.

Huo ndo ushikaji mzuri wa kumsaidia wakati wa shida.😉
Shida hana kwa sababu pesa ya kutosha tu anapata. Ila kiutu uzima huwezi kuanza kumfundisha mtu namna ya kutumia pesa akikutukana utasemaje? Pesa anapata kwa jasho lake.
 
Hahah we jamaa, hebu msome tena mwanahisabati...

Jamaa anatupigia stori juu ya washikaji zake walivyo mawaki, wanatumbua pesa halafu wanaishi kama digidigi kwa kuomba hisani ya vitu kama LUKU...

Jamaa ndio anatushauri tuwateme tu wakuda wote wenye uduanzi kama huo
🤣🤣🤣🤣asante umeniokoa
 
Wanakera hao rafiki,, kuna mmoja alikuja analia kabisa nilivyomkopesha amenipa mgongo kama sijamkopesha kabisa hawana habari hao marafiki,,, jamani hizi pesa tunatafuta kwa jasho na damu

Kwa sasa hivi boro kukosana tu ieleweke tu
Hela imekuwa ngumu mno.
 
Back
Top Bottom