Kama Makonda alikupora mali zako, unasubiri nini kwenda Mahakamani?

Fundi Madirisha

Senior Member
Jun 30, 2020
184
987
Huyu bwana alipokuwa mfalme wa jijini kila mtu alilia kilio chake hasa matajiri wa mjini, tulisikia kuna waliolazimishwa kutoa sehemu ya mali zao ili waendelee ku-survive, kuna waliobishana naye wakaukimbia mji.

Badala ya kumwambia Mama amkamate wakati tunajua kila kitu ni ma-evidences, mama siyo mamlaka yake kukamata na kufunga watu bali ni wale waliohisi kuonewa na wana ushahidi wana haki kwenda mahakamani ili watendewe haki zao. Mamlaka zinafanyia kazi ushahidi na siyo kauli au orders za mkuu wa nchi ambaye yeye ni mhimili mwingine kabisa na siyo mahakama.

Tunajua wengi sana wenye ya moyoni wakiwemo wale jamaa wa kituo station ya maneno ya Mawingu, wapo wafanyabishara mbali mbali mjini waliokumbana na kadhia za Bwanamdogo kwa sababu tu alipewa mamlaka, ni wajibu wao kwenda na ushahidi wao mahakamani ili hatua stahiki zishuke mkondo wake.

Ifike mahali kila mtu avune alichopanda ili tujifunze kuishi katika utawala wa sheria aliiacha marehemu baba wa taifa.
 
Inaonekana wengi bado wana lile wazo la "analindwa na mamlaka" hata wakati huu ambao hayupo tena kwenye system.

Wengi watakuwa wanasubiri akamatwe kwanza, ndio wajitokeze kupeleka ushahidi wa madhila aliyowafanyia kama ilivyokuwa kwa Sabaya.
 
Tatizo wengi wa hao walioporwa sio watu wasafi. Sasa mtu ni drug dealer, umeporwa pesa unaenda kulalamika wapi?
 
Back
Top Bottom