Kama kuna uwezekano (kifedha) Kitengo cha CID kiwe taasisi kamili inayojitegemea

Rwanda ni nchi ya kidekteta na polisi wake wanafanya kazi kutokana na matakwa ya wanasiasa waliowekwa na Kagame badala ya weledi.
Ni kweli.....ila hapo kutenganisha polisi na idara ya upelelezi walifanya vyema..........saa mbovu kuna muda huwa sahihi.
 
Ni jambo jema sana.
Ila mkuu wa kwanza wa CID atatokea wapi na wasaidizi wake watatokea wapi ili tuwe na divai mpya na chupa mpya.

Kama boss wao atatokea Polisi hawa na baadhi ya wasaidizi wwkatokea huko, je, changamoto ya uadilifu na 'kutokuoneana aibu' kutakoma.

Pengine nije na wazo fikirishi, kwanini tusiwe na Wizara tofauti kama uwekezaji n viwanda na biashara tuzalishe hela na kuongeza kwenye kikapu ili tunapounda taasisi hizi zinazotumia kodi bila kuzalisha ziweze kuwa well served na mzunguko wa makusanyo ya kodi utokanao na kuzalisha.

Madam SSH ana wazo zuri ila yaweza kuwa ni namna ya kuongeza gharama za kuendesha serikali huku speed ya kuzalisha ili kuongeza makusanyo ya kodi hauko sawia na kugawa taasisi Polisi ili wabaki usalama wa raia na makachero wawe Idara tofauti inayojitegemea.

So far, kila la heri kwenye mchakato huu wa mabadiliko, ila tuimarishe namna ya kuchochea ukuaji wa biashara ambazo zitakuwa sehemu ya kodi na tozo ambazo zitaendesha shughuli za kiserikali ambazo ni huduma kama CID.
 
Labda atokee kanisani na siyo polisi
 
Tume ya haki jinai imeliona hili.

Asante.

Hili lifanyike kwa manufaa mapana ya haki jinai nchini.
 
Hakuna jambo lisilowezekana.

FBI au Scotland Yard zilianzishwa taratibu na kwa makini sana na leo ni taasisi imara zenye nguvu na zenye kuweza kushughulikia kesi zinowahusu wanasiasa na watu wazito.

Kwa mfano FBI ilianzishwa na mwanasheria mkuu ambae ni mkuu wa idara ya mahakama (department of Justice) mwaka 1908.

Mkuu wake alieitwa Charles Bonaparte na alikuwa na kazi ya kuchunguza kesi nyingi zikiwemo wizi wa kalamu na kesi ambazo zilihitaji ujuzi wa hali ya juu. Hivyo akawa akiazima vijana kutoka idara ya ujasusi ( Secret service) kumfanyia kazi hizo.

Tatizo likawa wale vijana badala ya kurudi na taarifa kwake wao wakawa wakiripoti kwa mkuu wa Secret Service moja kwa moja na kisha mkuu huyo (akiishasoma hizo taarifa ) ndo alikuwa akizipeleka kwa Bonaparte.

Bunge la Congress likamwita Bonaparte kumhoji kwanini alikuwa akiazima vijana wa "secret Service" kumfanyia kazi zake za kiuchunguzi jambo ambalo lilikuwa ni kinyume na katiba na hakukuwa na kifungu cha sheria kilichompa uwezo wa kufanya hivyo.

Kwahiyo mwezi Mei mwaka 1908 Bunge likazuia rasmi kutumia secret service kufanya kazi za idara ya mahakama yaani department of justice. Hivyo Bonaparte akawa hana jinsi isipokuwa kuunda kikosi chake cha wachunguzi.

Alichokifanya Bonaparte akawaendea wale vijana alokuwa akiwatumia mwanzoni kutoka "secret service" na kisha akakusanya vijana wengine wapya kabisa wapatao 25 kuunda idara maalum ya upelelezi ambayo ndo ikaja kuwa FBI mpya ilokuwa na vijana 34 ambao walichunguza kesi za idara ya mahakama yaani department of justice.

Hivyo vijana wale wakaitwa "special agents" na bosi wao akaitwa chief examiner na wote wakawa wakiwajibika kwa mwanasheria mkuu wa serikali bwana Charles Bonaparte.

Kwahiyo kama ambavyo nimekuwa nikitoa ushauri kama ule wa kuunda upya idara yetu ya usalama, hapa naunga mkono hoja ya kuundwa idara au taasisi pekee ya kuchunguza kesi za aina zote.

Kesi zipo na tunazo leo kesi kama vile kuhujumu upatikanaji wa umeme nchini, hujuma dhidi ya upatikanaji wa sukari nchini, hujuma dhidi ya uhaba wa fedha za kigeni, hujuma za upatikanaji wa maji nchini na hujuma zingine nyingi tu ambazo kwa mujibu wa sheria hujuma hizi zaweza kabisa kukomeshwa kwa wahusika kufikishwa mahakamani na ikithibitika wahusika na mambo hayo basi kupelekwa jela.

Haya yote yaangukia kwenye makosa ya uhujumu uchumi au "enonomic crimes" na ndo moja ya kesi za kushughulikiwa na taasisi au shirika hilo jipya.

Ukiishaunda idara kama hii unakuwa huna haja ya kuwa TAKUKURU au kikosi cha kupambana na madawa ya kulenya kwani kazi zao zitaingia ndani ya idara hiyo mpya ambapo wakuu wake watakuwa wakiwajibika kwa mkurugenzi mkuu wa taasisi au shirika la uchunguzi.

Hivyo basi, bosi wake au mkurugenzi mkuu atawajibika kwa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali na atateuliwa na raisi wa JMT. Lakini endapo katiba itabadilishwa, huyu DG atapendekezwa na raisi na kisha Bunge litamhoji na kupitisha jina lake au kukataa.

Kisha mkurugenzi yoyote atakaeingia hapo atamudu kwenye kti hicho sambamba na raisi alie madarakani yaani miaka 10 na kisha atataeuliwa DG mwingine.
 
Kisha mkurugenzi yoyote atakaeingia hapo atamudu kwenye kti hicho sambamba na raisi alie madarakani yaani miaka 10 na kisha tataeuliwa DG mwingine.
Naungana na wewe.
 
Kutokana na mfumo wa Jeshi la polisi ulivyo, kitengo Cha CID kipo chini ya jeshi Hilo ambapo mkuu wa kitengo hicho ni mmoja wa wasaidizi wa IGP anayeshughulika na upelelezi wa makosa makubwa ya Kijinai "serious offences/crimes"

Hivyo kiutendaji watumishi katika kitengo hicho wanategemewa kuwa na ujuzi wa ziada katika tasnia ya upelelezi wa makosa ya jinai.

Kwakua kwa hivi karibuni kumetokea na malalamiko ya kubambika na kuchelewa Kwa kesi sio vibaya tukawa na taasisi maalum ambayo inajitegemea itayokuwa na jukumu la kufanya upelelezi wa makosa makubwa ya kijinai yatayofanyika hapa nchini na hata nje ya nchi kama itabidi kuwa hivyo kulingana na mazingira ya kosa litalofanywa nje ya nchi.

Hii itaifanya jeshi la polisi kupunguziwa mzigo mkubwa wa kimajukumu ililonalo Sasa ambalo Naona kama ndio kikwazo Cha baadhi ya kesi kuchukua muda mrefu kukamilika.

Taasisi hii mpya itakuwa na muda na ikiwezeshwa kuwa na wataalam na vifaa itasaidia pakubwa katika kuharakisha upelelezi wa kesi.

Polisi wabakie na jukumu lao mama la Ulinzi wa Raia na Mali zao, pamoja na kuzuia kutendeka Kwa makosa ya jinai, na kuhakikisha kuna utulivu na Sheria zinazingatiwa na Raia.
Naunga mkono hoja.
 
Wazo zuri sana.

Itasaidia kuwe na check and balance ya shughuli za kutoa haki na kesi Tz.

Halafu kuna watu smart bright sana ambao hawangependa kuwa mapolisi ila kuwa wapelelezi sawa. Kama hadithi za Joram Kiango.

Itapendeza kama hicho kitengo kichukue watu toka jeshini na usalama wa taifa kama sehemu kubwa kama sio yoote ya staff wake. Sababu kuepusha kuonekana kwa wananchi tena kama ni sehemu ya polisi.

Itapendeza sana.
 
Wanachelewa sana kuleta hili, umefika wakati Sasa polisi watenganishwe na upelelezi wa makosa ya jinai. Wamepewa hiyo nafasi tangu kuanza Kwa jeshi Hilo na mpaka sasa hawajaweza kuonesha ufanisi unaotarajiwa.
Upelelezi uwe ni professional yenye qualifications zake sio mazoea Wala ukongwe kazini. Vigezo viwe kuanzia diploma na kuendelea huko mbele Ili kupunguza Ile upande wa mashtaka 'kushindwa kuthibitisha pasi na shaka'
 
kama lengo ni kufungua wigo mpana zaidi wa ajira ni sawa,lakini kama lengo ni kupata ufanisi ktk maswala ya haki,tuutathimini kwanza ufanisi uliotoka PCCB,madawa ya kulevya,fire,uhamiaji na taasisi nyingine ambazo zina asili ya upolisi.
kinachosumbu hii nchi ni mfumo wake mbovu,unaohanisi kila jambo lenye asili ya wema na weledi.

leo hii unaomba CID ijitenge na polisi ili ikasimamiwe na malaika au hawa hawa machawa wa ccm watakaoteuliwa??vipi kuhusu mahakamani nako mnafanya jambo gani kuhakikisha haki haipotei??

tukiangalia kwa umakini hata huko nchi zilizoendelea hawajawahi kuitenga division ya upelelezi na polisi kama taasisi,wanachofanya wanaunda organ nyingine ambayo nayo itakuwa inashiriki kazi zile zile za upelelezi lakini kwa lengo la uhakiki,mfano FBI wanashughulika na upelelezi wa matukio makubwa ya usalama kwa maslahi ya marekani lakini hata matukio madogo madogo kama backup ya ushahidi kama CIDs wataonyesha mapungufu.
na sharti ni kwamba lazima waingie wao eneo la tukio ndipo CIDs waingie.
 
Uko sawa lakini unapojadili kuhusu taasisi kama FBI na idara kama CID kuna tofauti kubwa sana kiutaalam na kiutendaji.

FBI ni wachunguzi wa uhalifu wa kupangwa kitaalam kama ujasusi, uhalifu wa kalamu unovuka mipaka, mauaji yanovuka mipaka, uhalifu unotishia usalama wa nchi, madawa ya kulevya yanohusisha makundi makubwa, uuzaji silaha unohatarisha usalama wa nchi hayo ni "very serious crimes".

CID ndani ya polisi bado zipo (wenyewe Marekani ) waita LAPD ni uchunguzi wa uhalifu kama vile watu kuuana au mtu kuua, ubakaji (sexual offences), watu kupigana na kuumizana (assaults), wizi wa kuagiza (steal to order) na kesi hizo uchunguzi wake hushughulikiwa na askari kanzu (detectives).

Sasa hapo tofauti yao ni kwamba watu wa FBI ni majasusi na wenye utaalam wa hali ya juu katika kuchunguza, na kushughulikia uhalifu niloutaja hapo juu lakini wao hutumia SWAT kutekeleza kazi zao.

CID wao ni polisi kitaaluma na mtu wa CID huweza kujiunga na FBI akiwa amejiongeza kielimu na kwa kwenda kozi katika chuo cha FBI.

Sasa sisi tuna CCP Moshi lakini hatuna chuo maalum kama cha FBI ambacho hutoa vyeti baada ya mafunzo ya hali ya juu na maofisa wake huitwa "special agents" na yuko juu ya "police detective".
 
usiweke neno SANA,utofauti uko kwenye mipaka ya kazi zaidi na si kiutaalam ama uwezo,kwanza maofisa wengi wa FBI ni mapolisi hawa hawa waliokuwa humo CID,lengo ni kuifanya FBI kuwa na wataalam wenye uzoefu usio na mashaka.
so ni kama kusema FBI anaongezewa uwanja wa kazi zaidi.
FBI ni wachunguzi wa uhalifu wa kupangwa kitaalam kama ujasusi, uhalifu wa kalamu unovuka mipaka, mauaji yanovuka mipaka, uhalifu unotishia usalama wa nchi, madawa ya kulevya yanohusisha makundi makubwa, uuzaji silaha unohatarisha usalama wa nchi hayo ni "very serious crimes".
yah kama nilivyosema hapo,nia ilikuwa kuunda FBI yaani wapelelezi wa polisi yenye nafasi kubwa zaidi kufanya mambo hayo ya upelelezi,kule CID hata nje ya jimbo lake hatoki.
CID ndani ya polisi bado zipo (wenyewe Marekani ) waita LAPD ni uchunguzi wa uhalifu kama vile watu kuuana au mtu kuua, ubakaji (sexual offences), watu kupigana na kuumizana (assaults), wizi wa kuagiza (steal to order) na kesi hizo uchunguzi wake hushughulikiwa na askari kanzu (detectives).
hii LAPD ni moja wapo na majina ya polisi nyingi ndani ya marekani hii ni ya jimbo la los angeles ,haya matukio yote uliyotaja FBI wanakuwa na report zake hata kwao,lengo sana si kutoa ushahidi mahakamani,hapana.
Sasa hapo tofauti yao ni kwamba watu wa FBI ni majasusi na wenye utaalam wa hali ya juu katika kuchunguza, na kushughulikia uhalifu niloutaja hapo juu lakini wao hutumia SWAT kutekeleza kazi zao.
mkuu,swat na FBI tena🙄🙄🙄.
SWAT ni ni kitengo maalumu cha polisi kinasubiri tu ripoti kutoka eneo la tukio,zitolewe na traffic polisi,sherif ama polisi yoyote vikidhi uhitajika wao wanatimba.
CID wao ni polisi kitaaluma na mtu wa CID huweza kujiunga na FBI akiwa amejiongeza kielimu na kwa kwenda kozi katika chuo cha FBI.
FBI ni polisi kitaalam pia ndio maana wana badge na vest kabisa,ila ni polisi ambaye hajafungiwa eneo alipo tu.
Sasa sisi tuna CCP Moshi lakini hatuna chuo maalum kama cha FBI ambacho hutoa vyeti baada ya mafunzo ya hali ya juu na maofisa wake huitwa "special agents" na yuko juu ya "police detective".
huu ni uzembe tu wa serikali,haijawahi kuwa serious na jamb lolote,ktk mtaala wa polisi umeandikwa kabisa,CID ni taaluma ndani ya polisi,ina kozi yake,kitambulisho chake,malipo yake na uongozi wake pia,ila eh kazi tupu.
 
Uko sawa lakini unapojadili kuhusu taasisi kama FBI na idara kama CID kuna tofauti kubwa sana kiutaalam na kiutendaji.

FBI ni wachunguzi wa uhalifu wa kupangwa kitaalam kama ujasusi, uhalifu wa kalamu unovuka mipaka, mauaji yanovuka mipaka, uhalifu unotishia usalama wa nchi, madawa ya kulevya yanohusisha makundi makubwa, uuzaji silaha unohatarisha usalama wa nchi hayo ni "very serious crimes".

CID ndani ya polisi bado zipo (wenyewe Marekani ) waita LAPD ni uchunguzi wa uhalifu kama vile watu kuuana au mtu kuua, ubakaji (sexual offences), watu kupigana na kuumizana (assaults), wizi wa kuagiza (steal to order) na kesi hizo uchunguzi wake hushughulikiwa na askari kanzu (detectives).

Sasa hapo tofauti yao ni kwamba watu wa FBI ni majasusi na wenye utaalam wa hali ya juu katika kuchunguza, na kushughulikia uhalifu niloutaja hapo juu lakini wao hutumia SWAT kutekeleza kazi zao.

CID wao ni polisi kitaaluma na mtu wa CID huweza kujiunga na FBI akiwa amejiongeza kielimu na kwa kwenda kozi katika chuo cha FBI.

Sasa sisi tuna CCP Moshi lakini hatuna chuo maalum kama cha FBI ambacho hutoa vyeti baada ya mafunzo ya hali ya juu na maofisa wake huitwa "special agents" na yuko juu ya "police detective".
Nikurekebeshe CID ni police detective, LAPD ni jina la police waliopo Los angeles, polisi hao hao ukienda new york unakuta NYPD, so kokote walipo utakuta waanza na jina walipo then PD. Lakini wote ni police wale wale
 
Na Rwanda imekua Ni ya 1 kwa kuongoza in terms of rule of law Kati ya nchi 33 za Sub-Saharan Africa.

Na globally kwny rule of law Rwanda Ni ya 42,kwa Nchi nyingine za huku E/Africa Tz Ni ya 100,Kenya ya 106,Uganda ya 125

Source Ni The World Justice Project(WJP) mwaka 2021.
Rwanda ile ile ya dicteta mla watu Kagame?
 
Back
Top Bottom