Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,635
- 40,790
Kutokana na mfumo wa Jeshi la polisi ulivyo, kitengo Cha CID kipo chini ya jeshi Hilo ambapo mkuu wa kitengo hicho ni mmoja wa wasaidizi wa IGP anayeshughulika na upelelezi wa makosa makubwa ya Kijinai "serious offences/crimes"
Hivyo kiutendaji watumishi katika kitengo hicho wanategemewa kuwa na ujuzi wa ziada katika tasnia ya upelelezi wa makosa ya jinai.
Kwakua kwa hivi karibuni kumetokea na malalamiko ya kubambika na kuchelewa Kwa kesi sio vibaya tukawa na taasisi maalum ambayo inajitegemea itayokuwa na jukumu la kufanya upelelezi wa makosa makubwa ya kijinai yatayofanyika hapa nchini na hata nje ya nchi kama itabidi kuwa hivyo kulingana na mazingira ya kosa litalofanywa nje ya nchi.
Hii itaifanya jeshi la polisi kupunguziwa mzigo mkubwa wa kimajukumu ililonalo Sasa ambalo Naona kama ndio kikwazo Cha baadhi ya kesi kuchukua muda mrefu kukamilika.
Taasisi hii mpya itakuwa na muda na ikiwezeshwa kuwa na wataalam na vifaa itasaidia pakubwa katika kuharakisha upelelezi wa kesi.
Polisi wabakie na jukumu lao mama la Ulinzi wa Raia na Mali zao, pamoja na kuzuia kutendeka Kwa makosa ya jinai, na kuhakikisha kuna utulivu na Sheria zinazingatiwa na Raia.