Kuzika katika makaburi ya Jumuiya ndio mpango sahihi wa binadamu waliostaarabika, sio uduni, umasikini au uswahili

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,681
46,371
Sababu za baadho ya jamii, familia au watu kuamini watu ni wasio na kwao au pesa ndio huzikwa katika makaburi ya Jumuiya ni zipi?

Mtazamo wangu ni kwamba kwa watu wanaofikiria vizuri au wenye akili kubwa kuzika katika eneo la nyumba au kiwanja ndio kulipaswa kuonekana jambo lisilotumia akili, la kijinga, la ubinafsi na kutojali waliobaki.

Waliobaki hai na wengine watakaondelea kuja duniani watakapokuja kutaka kuuza eneo ambapo mahali watu wamezikiwa inakuaje au itakuaje? Si wanakuwa kama wamefungwa mikono tayari na wafu??

Mimi naamini kuzika katika makaburi ya Jumuiya ndio mpango sahihi na unaotakiwa kwa binadamu waliostaarabika.
 
Back
Top Bottom