Unafanya nini kumuandalia future kijana wako?

Braza Kede

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
1,771
3,405
Sasa kila mzazi kazi imekuwa moja tu, dogo aende shule.

Haya wanaenda shule wanamaliza hadi vyuo huko lakini unaambiwa ajira hamna!

Unafanya nn cha kiutofauti kumuepusha dogo na mzunguko huo ambao umeshaonekana kukosa majibu kwa hatima ya badae ya kijana wako?

Au unamwacha tu atakachokutana nacho ndio ichoicho rizki yake?
 
Mpe elimu,mnunulie pori mpandie miti akimaliza chuo atakata mbao atauza apate mtaji wakati huo shamba sio pori tena atakata viwanja auze ajenge investment mfano,stand,frem za kupanga,soko, apartment,shule,guest nk.ajiajiri alichosomea.
Heka kumi TU hakosi billion moja akimaliza chuo.
 
Kipaji tu ....

Kama Ni mwimbaji ...

Kama Ni mchezaji ...

Kama Ni mfanyabiashara ...

Nitahakikisha namuwezesha ....

Kipaji =pesa =maisha ...

Elimu ya darasani kusolve integration na differentiation=umasikini =takataka
 
1. Kila weekend wanaenda kusoma skills kutegemea na nini wanapenda; i.e ufundi kama magari, simu/radio/TV, kushona, guitar, piano, et al.

2. Naleta mwalimu nyumbani wa computer skills; including #coding

3. Kwa sasa nawapa kila aina ya ujuzi naoweza ku-afford gharama zake. Baadae watachagua wenyewe nini wanataka kufanya.

Dongbei
 
Mpe elimu,mnunulie pori mpandie miti akimaliza chuo atakata mbao atauza apate mtaji wakati huo shamba sio pori tena atakata viwanja auze ajenge investment mfano,stand,frem za kupanga,soko, apartment,shule,guest nk.ajiajiri alichosomea.
Heka kumi TU hakosi billion moja akimaliza chuo.
Atakutana na mkurugenzi tapeli atanyang'anywa shamba na kuambiwa liko kwenye eneo la mipango miji. Wakati huo wewe ushakua mbolea aina ya mboji (umeoza kaburini)…
 
Kabla ya kununua unaangalia mpangilio wa mji upoje na unakuwa na documents kabisa
 
Sasa kila mzazi kazi imekuwa moja tu, dogo aende shule.

Haya wanaenda shule wanamaliza hadi vyuo huko lakini unaambiwa ajira hamna!

Unafanya nn cha kiutofauti kumuepusha dogo na mzunguko huo ambao umeshaonekana kukosa majibu kwa hatima ya badae ya kijana wako?

Au unamwacha tu atakachokutana nacho ndio ichoicho rizki yake?
wa kwangu ninamsisitiza ayakabidhi maisha yake kwa Bwana Yesu. AOKOKE! autafute kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake, maana mengine yote atazidishiwa. ni ziada tu. utajiri wa dunia hii inayopita ni ziada tu.

JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Watoto unawekeza kichwani kwa kuwapa Self-investment

MTU mwenye Elimu na maarifa maisha hayawezi kumyumbisha .

Self-investment ndo kitu pekee ntawapa watoto wangu.

Ni ngumu Sana kutoboa na kufika unapoapahitaji ikiwa upstair panashida.

Kati ya watu weusi familia za watu zilizopewa urithi wa nyumba ,biashara leo hii wengi hawana kitu

Wameishia kurogana kuuana , kuchukiana

Hivyo kuwasaidia watoto wangu ntawajenga kiakili ,kiimani , kifalsafa kuhusu upendo, kushirikiana , na kujitambua.
 
wa kwangu ninamsisitiza ayakabidhi maisha yake kwa Bwana Yesu. AOKOKE! autafute kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake, maana mengine yote atazidishiwa. ni ziada tu. utajiri wa dunia hii inayopita ni ziada tu.

JESUS IS LORD&SAVIOR
Them prayers ain't working.
 
Kabla ya kununua unaangalia mpangilio wa mji upoje na unakuwa na documents kabisa
Mheshimiwa Sumaye alikuwa na hati za umiliki wa ekari 33 Mabwepande, lkn jiwe alimnyang'anya kwa hila tu eti kwasbb kahamia upinzani. Nchi ngumu sana hii, hati ni makaratasi tu. Kama viongozi wanavunja katiba watashindwa kuivunja hati ya shamba?
 
Usiwe mwanasiasa TU,asingehamia upinzani asingepokonywa.
Karudi ccm kupata msaada wa kuzikwa kama lowasa
 
Back
Top Bottom