Kama Kanisa Katoliki hawatakemea huu Ujinga nitashangaa sana

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,500
86,042
Polisi wa Tanzania wanaendeleza dhihaka kwa Kanisa kubwa kabisa nchini na duniani RC kwa kuvamia kila mara kwenye ibada zake na kukamata waumini tena ibadani.

Cha kushangaza haya hayatokei SDA wala Lutheran wala kwenye haya makanisa kama ya akina Gwajima.

Hii ni dharau na dhihaka kubwa sana, Polisi hawajaitwa kuwa pengine kuna uvunjifu wa amani, sasa kiherehere cha kwenda kukamata waumini kisa wanafanya maombi kinatoka wapi?

Huku kuwashwawashwa kwa Polisi wa Tanzania kutatupeleka kubaya soon.

Wakumbuke, nawakumbusha aliyekuwa Mkurugenzi wa Itigi na baadhi ya Askari Wanyamapori wako gerezani Singida hadi leo kwa kesi ya mauaji Kanisani.

Tumieni akili kidogo acheni kudharau imani za watu

Jumla ya viongozi na wanachama 20 wa CHADEMA kanda ya Viktoria wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la polisi baada ya kukamatwa jana kanisani.

Kwa mjibu wa OCD anadai kuwa wanachama hao wa CHADEMA walifanya vurugu kanisani.

Askofu Nkwande amekanusha kuwa kulikuwa na vurugu
 
Polisi wa Tanzania wanaendeleza dhihaka kwa Kanisa kubwa kabisa nchini na duniani RC kwa kuvamia kila mara kwenye ibada zake na kukamata waumini tena ibadani...
Ni sawa kabisa. nawapongeza Jeshi la Polisi Tanzania kwa hatua hiyo.

Yaani mnataka mfanye uhalifu halafu mkimbilie Kanisani na Polisi wawatizame tu? Msituchafulie kanisa, Msituchonganishe na Jeshi la Polisi Tanzania.

Kama ni muhalifu utakamatwa popote utakapokuwepo.
 
Tumefundishwa kuvumiliana. Na hakuna kitu hatari kama kudharau imani,dini,kanisa ama dhehebu la mwingine. Ndo maana yapo tofauti ili kila mtu kwa imani yake achague pakwenda.
So ni bora tukabebeana madhaifu ya kiimani kuliko kuanza kuchokonoana.
Kazi ya kanisa nini?
 
Polisi wa Tanzania wanaendeleza dhihaka kwa Kanisa kubwa kabisa nchini na duniani RC kwa kuvamia kila mara kwenye ibada zake na kukamata waumini tena ibadani.

Cha kushangaza haya hayatokei SDA wala Lutheran wala kwenye haya makanisa kama ya akina Gwajima.

Hii ni dharau na dhihaka kubwa sana, Polisi hawajaitwa kuwa pengine kuna uvunjifu wa amani, sasa kiherehere cha kwenda kukamata waumini kisa wanafanya maombi kinatoka wapi?

Huku kuwashwawashwa kwa Polisi wa Tanzania kutatupeleka kubaya soon.

Wakumbuke, nawakumbusha aliyekua Mkurugenzi wa Itigi na baadhi ya Askari Wanyamapori wako gerezani Singida hadi leo kwa kesi ya mauwaji Kanisani.

Tumieni akili kidogo acheni kudharau imani za watu
Mbowe yupo Ukonga, waende huko wakamuombee. Hili la kujikusanya kila Jumapili kwenda makanisani na hayo majezi yao eti wanakwenda kumuombea Mbowe sidhani kama ni sahihi, mahali pale si mahali pa siasa na kuna watu wa itikadi tofauti tofauti wao wasiwalazimishe watu wengine kuwaunga mkono bali waiachie Mahakama itaamua
 
Back
Top Bottom