Kama hujayapitia haya maisha, kubali umekosa mengi

Ivi mbona watoto wa sikuhizi ukipika wali hawashtuki? Hawana ile hamasa kama tuliyo kua nayo?
Nahisi ubwabwa wa siku hizi umechajachuliwa hauna harufu kama ya zamani?
Au watu siku hizi hatujui kupika kama mama zetu ?
Harufu ya ubwabwa ilikua unaikuta km 10

Mkuu huenda ukawa sahihi ,miaka ya nyuma kidogo ulikuwa ukipikwa wali lazima majirani wajue ,kwa sasa naona uenda wamechakachua sana ile mbegu ya kyela .

Huenda pia kwa sababu tumezoea hicho chakula kwa sasa ,ndo tunaona harufu pia hauna . fikiria miaka ya nyuma ulikuwa unafikiria kupata shi 100 ya maandazi tu ,saiv unazo mia nyingi mbona hununui maandazi??

Hizo sababu mbili huenda zikawa na mashiko sana
 
Nakumbuka kwetu Mkoani Kagera..!!

Enzi hizo Matoke (Ndizi banana sio dili)
Tunazikusanya na kuzirundika/kuzichomeka katikati/ndani ya Mpira, kisha tunaingiza Miti miwili ndani yake, kinacho fuata ni wachache wanaweza kujua...!!

Wakati wote ulikuwa unaomba na kufurahia kutumwa, maana si kwa Mwendo kasi wa enzi hiyo...!!
Hii cha mtoto, sisi tulikuwa tunachukua tairi la lori au trekta unaingia hapo katikati unajikunja then wenzio wanakusukuma! Siku ingine wanakusukuma wanapoteza muelekeo wanakuacha upambane na hali yako!
View attachment 1101131
 
Aisee hiyo ya kuingia katikati ya gurudumu sitaki kabisa kuisikia, nusura initoe uhai maana waliniporomosha kwenye mteremko mkali likawashinda speed aisee hadi leo nikikumbuka mwili unasisimuka kwa hofu, ulikua mchezo wa hatari sana.
 
Dah enzi hizo hadi msosi unapotezea kisa michezo.

Ukirudi home mama ananongwa balaa.
Mama yangu ilikuwa ukimiss lunch anakuwekea na share yako ya jion.
Salama yako ule chakula chote, ukibakiza shughuli unayo. Sasa uwe ulikula kwa watu mchana...hakika hata ujitahidi vipi huwezi maliza
RIP mummy. Amenisaidia sana kunilea ktk maadali mema
 
Mkuu huenda ukawa sahihi ,miaka ya nyuma kidogo ulikuwa ukipikwa wali lazima majirani wajue ,kwa sasa naona uenda wamechakachua sana ile mbegu ya kyela .

Huenda pia kwa sababu tumezoea hicho chakula kwa sasa ,ndo tunaona harufu pia hauna . fikiria miaka ya nyuma ulikuwa unafikiria kupata shi 100 ya maandazi tu ,saiv unazo mia nyingi mbona hununui maandazi??

Hizo sababu mbili huenda zikawa na mashiko sana
Dah mimi kuna keki nilikuwa nazipenda balaa zilikuwa zinauzwa sh 9! Yaani nikipata hio hela breki ya kwanza dukani
 
Hatari sana asee, kuna ile ya kuwinda ndege na manati. Sasa sisi tukawa tukimaliza kuwinda ndege tunaanza kujificha ile kama kombolela ukitoa tu kichwa au mwili unapewa jiwe la maana la manati. Sitasahau siku Rafiki yangu aliponibutua manati ya jicho, nilikaa ndani mwezi mzima bila kuonana na mwanga na makofi juu ya bimkubwa.
We jamaa nahisi tunafahamiana.!
Maana nilishawahi kumbutua mtu manati ya jicho utotoni.!
 
Huko nchi za scandinavia wamebadili mitaala ya elimu.. ile elimu ya awali hakuna kusoma.. ni kucheza tuu.. wanaruhusiwa kuzurura maeneo ya shule na kufanya chochote wanacho penda kukiwa na usimamizi kidogo.

Na wanasema imefanya watoto kuwa na ujasiri na ubunifu zaidi..

Naunga mguu hoja.
 
Michezo niliyocheza, Tobo bao, kula mbakishie baba, magari ya mbao, magari ya udongo, magari ya mabati, gololi za kunga'aa, za korosho, za mabetri, kuvua samaki bondeni, bunduki za visoda,mpira wa miguu, safa bwege, kombolela waokoe wenzako, karata za lastcard, kuangalia mikanda ya video na kuigiza ngumi tunazoona,nk
 
Nina mtoto wangu wa kiume miaka 4. Yaani namuomba MUNGU mara mbili mbili,afikishe umri wa kujitambua hajavunjika kiungo,ni mtundu hatari. Ilikuwa bora michezo yetu,hii ya kwao ya kuangalia kwenye computer/tv anaona mtu anamchoma mwingine na yeye anataka eact hivyo hivyo
Hilo tatizo aisee
 
Hii cha mtoto, sisi tulikuwa tunachukua tairi la lori au trekta unaingia hapo katikati unajikunja then wenzio wanakusukuma! Siku ingine wanakusukuma wanapoteza muelekeo wanakuacha upambane na hali yako!
View attachment 1101131
Tulikuwa tunajaza maji kwenye Tairi, na unashika miti miwili huku na huku, babu kinachofuatia ni mbio tuu.... Na break yake ABS YA YUTOUNG aioni kitu....!! Ndio maana watoto was zamani afya zilikuwa shwariiiiii....,,,,,
 
Sema hatuna death rate , unaweza kuta waliopoteza maisha kwa michezo hii ni wengi sana.
Tulikuwa tunajaza maji kwenye Tairi, na unashika miti miwili huku na huku, babu kinachofuatia ni mbio tuu.... Na break yake ABS YA YUTOUNG aioni kitu....!! Ndio maana watoto was zamani afya zilikuwa shwariiiiii....,,,,,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom