Kama hujayapitia haya maisha, kubali umekosa mengi

Halafu ukitoka hapa unataka ukalale bila kuoga:D:D:D:D!
View attachment 1101150
Huu mpira ni mtamu utotoni,enzi hizo usijaribu kumchokoza mwenye mpira,au kumnyima chochote hauchezi mpira,pia ukiwa na viatu mwenye mpira akiwa hana lazima uvue viatu kwanza ndio mpira uanze,usimchezee rafu mwenye mpira hapo ataushika mpira,mpaka utoke uliyecheza rafu.Mwenye huo mpira alikuwa mfalme,na wachache sana walikuwa na ufundi wa kuishona hiyo mipira,si kama sasa inauzwa mingi sokoni.
 
Doh mtoa Mada kuna Kisa nilikifanya utotoni, nilitumwa dukani kununua vibiriti vitano Muuza duka alinifungia kwenye kagazeti ili nisiangushe sasa na kumbuka tulionywa sana kuchezea vibiriti hivyo hufichwa mbali sana. Nikiwa njiani nilikuwa na shauku kweli kuchezea njiti sasa basi nikakaa sehemu kulikuwa na yard ya magari (Bahari Motors ya Hashimu Rungwe, Makumbusho) nikavitoa vile vibiriti nikawasha njiti ya mojamoja toka kwenye kila boksi, staili ya pili nilichukua njiti moja moja tena naisimamisha then nafyatua kwa kidole ili iruke iwake juu 😂......sikutosheka asee nikatoa tena njiti moja moja na hii ndio ilinitia matatani maana niliwasha njiti then nikagusisha kwenye kila kiboksi vikiwa wazi then nafunga faster ili kujua kifuatacho "itv" 😂😂 matokeo njiti zote za vibiriti ziliwaka zote at once nilivyokuwa wa hovyo nikavirudisha kwenye gazeti. Safari ya home ikaanza ile nafika tu jikoni dada alikuwa nje, nikadump vibiriti juu ya kabati Halafu nikaaga bana, nikaambiwa lete huku niwashe aseee kila akupiga njiti hola na baruti inapukutika tuu, nikabananishwa ww Mbona njiti haziwaki nilijimjibu nimepewa Ivyo ivyo....nilidakwa mkono mpaka dukani ile tunakaribia tu nilikubali niliviwasha 😅😅😅
 
Doh mtoa Mada kuna Kisa nilikifanya utotoni, nilitumwa dukani kununua vibiriti vitano Muuza duka alinifungia kwenye kagazeti ili nisiangushe sasa na kumbuka tulionywa sana kuchezea vibiriti hivyo hufichwa mbali sana. Nikiwa njiani nilikuwa na shauku kweli kuchezea njiti sasa basi nikakaa sehemu kulikuwa na yard ya magari (Bahari Motors ya Hashimu Rungwe, Makumbusho) nikavitoa vile vibiriti nikawasha njiti ya mojamoja toka kwenye kila boksi, staili ya pili nilichukua njiti moja moja tena naisimamisha then nafyatua kwa kidole ili iruke iwake juu ......sikutosheka asee nikatoa tena njiti moja moja na hii ndio ilinitia matatani maana niliwasha njiti then nikagusisha kwenye kila kiboksi vikiwa wazi then nafunga faster ili kujua kifuatacho "itv" matokeo njiti zote za vibiriti ziliwaka zote at once nilivyokuwa wa hovyo nikavirudisha kwenye gazeti. Safari ya home ikaanza ile nafika tu jikoni dada alikuwa nje, nikadump vibiriti juu ya kabati Halafu nikaaga bana, nikaambiwa lete huku niwashe aseee kila akupiga njiti hola na baruti inapukutika tuu, nikabananishwa ww Mbona njiti haziwaki nilijimjibu nimepewa Ivyo ivyo....nilidakwa mkono mpaka dukani ile tunakaribia tu nilikubali niliviwasha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom