Kama hujayapitia haya maisha, kubali umekosa mengi

Hii cha mtoto, sisi tulikuwa tunachukua tairi la lori au trekta unaingia hapo katikati unajikunja then wenzio wanakusukuma! Siku ingine wanakusukuma wanapoteza muelekeo wanakuacha upambane na hali yako!
View attachment 1101131
Ahahaaaaa....! Tumekoswa koswa hiyo. Dogo mmoja tyre liko speed akachomoka,tyre likaendelea speed na yeye akaendelea speed mhemo wa kwanza alienda kuupatia ICU
 
Nina mtoto wangu wa kiume miaka 4. Yaani namuomba MUNGU mara mbili mbili,afikishe umri wa kujitambua hajavunjika kiungo,ni mtundu hatari. Ilikuwa bora michezo yetu,hii ya kwao ya kuangalia kwenye computer/tv anaona mtu anamchoma mwingine na yeye anataka eact hivyo hivyo
 
Watoto wanahitaji ulinzi sana , ikiwezekana hakikisha tv analyo iangalia ji ya nyumbani au shuleni..

Na nyumbani hakilisha anaanglia katuni tuu , ndio maana wenzetu wanakua na tv 2 au 3..

Tatizo linakuja wadada wa kazi.. kama hutakuta mtoto ana mpiga busu mtoto mqenzake eti kaona kwenye TV.
 
Ulikua ujinga..

Nakumbuka mnaenda kwenye majani wavulana na wasichana mnaanza kuonyeshana vikojeleo, na kuchekana eti ona vifupi wengine ona virefu.. mnafunika na mnaendelea kucheza ...
Watoto wa siku izi ukiwaacha dk 2 nyingi washamaliza.si tulikuwa tunapiga vya nguo nguo
 
Nina mtoto wangu wa kiume miaka 4. Yaani namuomba MUNGU mara mbili mbili,afikishe umri wa kujitambua hajavunjika kiungo,ni mtundu hatari. Ilikuwa bora michezo yetu,hii ya kwao ya kuangalia kwenye computer/tv anaona mtu anamchoma mwingine na yeye anataka eact hivyo hivyo
Aisee enzi zetu kuna dogo aliruka balcony huku anaimba super maaaaaan....alivunjika mikono yote!
 
Sasa hivi nimejiuliza starehe ya kuzungurushwa na lile gurudumu ni nini hata sina jibu!
ILIKUWA INAKUSAIDIA SANA SEMA HUKUJUA TUU, KUNA WATOTO MPAKA WAMEKUA WATU WAZIMA WAKIPANDA GARI AU NDEGE LAZIMA WATAPIKE SABABU YA KIZUNGU ZUNGU, ILA KAMA ULICHEZA UTOTONI MICHEZO HIYO HUWEZI KUPATA HILO TATIZO NA NDIO SABABU SHULE NYINGI HIZI ZA ENGLISH MEDIUM ZINA MICHEZO YA AINA HIYO SABABU WANAJUA WATOTO WA SIKU HIZI HAWACHEZI NYUMBANI.
 
Jion umepikwa ubwabwa sheria ilikuwa Siku ya ubwabwa watoto wote muwe mshaoga
Siku hiyo nimeingia bafuni nilikuwa na staili ya kufungua bomba (huku mikoani tunaita bomba la mvua sijui huko dar) afu unakaa pembeni tu afu unaloweka dodoki unajipangusa afu unaibuka nje, kumbe mshua kazunguka nyuma ya bafu kwenye kadirisha kadogo ananichora tu

Kwa mkwala nikaingia mezani kula dingi akaibuka we umeoga? Maza kawahi eeh kaoga tayari katoka bafuni saiv dingi kanivua shati kucheki mgongoni duh kama mashineni mpauko wa hatari nikapigwa kadi nyekundu ubwabwa ukapita hv
 
Nakumbuka niligongwa na baiskeli hadi kuzimia. Nakuja kuzinduka niko home wanajiandaa kunipeleka zahanati.
Nilikuwa naendesha gari ya vigaloni vya bati barabarani. Nikawa nahamahama upande wa barabara mara kulia mara kushoto hamadi paa.
Suti yangu yote ilikuwa damu tupu
😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Jion umepikwa ubwabwa sheria ilikuwa Siku ya ubwabwa watoto wote muwe mshaoga
Siku hiyo nimeingia bafuni nilikuwa na staili ya kufungua bomba (huku mikoani tunaita bomba la mvua sijui huko dar) afu unakaa pembeni tu afu unaloweka dodoki unajipangusa afu unaibuka nje, kumbe mshua kazunguka nyuma ya bafu kwenye kadirisha kadogo ananichora tu

Kwa mkwala nikaingia mezani kula dingi akaibuka we umeoga? Maza kawahi eeh kaoga tayari katoka bafuni saiv dingi kanivua shati kucheki mgongoni duh kama mashineni mpauko wa hatari nikapigwa kadi nyekundu ubwabwa ukapita hv
 
Ivi mbona watoto wa sikuhizi ukipika wali hawashtuki? Hawana ile hamasa kama tuliyo kua nayo?

Nahisi ubwabwa wa siku hizi umechakachuliwa hauna harufu kama ya zamani?

Au siku hizi hatujui kupika kama mama zetu ?

Harufu ya ubwabwa ilikua unaikuta km 10
Kulikuwa kukipikwa wali tunazunguka jiko uumuke ,uwe mwingi .Dah! nikikumbuka nacheka sana
 
Mimi nakumbuka kujifunza kuruka sarakasi au sambasoti, aisee niliangukia shingo iliuma wiki mbili....
Ilibidi nibaki na chandimu tuu ili maisha yaende
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom