Kama hujayapitia haya maisha, kubali umekosa mengi

Hahahaha. Wa mijini haya mambo hawayajui
We acha tu mkuu, yaani kipindi hicho kama hauko faster enough, kitendo cha kumbwela kidogo tu ushakula jiwe la maana. Yaani ilikua ni Policy kwamba tukitoka kuwinda kama hatujapata ndege/njiwa basi tunaanza kuwindana.
 
Huko nchi za scandinavia wamebadili mitaala ya elimu.. ile elimu ya awali hakuna kusoma.. ni kucheza tuu.. wanaruhusiwa kuzurura maeneo ya shule na kufanya chochote wanacho penda kukiwa na usimamizi kidogo.

Na wanasema imefanya watoto kuwa na ujasiri na ubunifu zaidi..

Haha..sana...Watoto wa siku hizo naona kama wako bizy sana na maisha...kama watu wazima yaani...Nahisi na mitandao hii na simu..Wee unakuta kitoto kidogo cha miaka miwili tayari kinalilia kishinde na simu...hatar sana
 
Hii cha mtoto, sisi tulikuwa tunachukua tairi la lori au trekta unaingia hapo katikati unajikunja then wenzio wanakusukuma! Siku ingine wanakusukuma wanapoteza muelekeo wanakuacha upambane na hali yako!
View attachment 1101131
Nilifanya uwo ujinga wakasukuma tyre kumbe mbele kuna gari inakuja bahati yangu dreva alikwepa lile tyre leo ningekuwa marehemu.
 
I
Huko nchi za scandinavia wamebadili mitaala ya elimu.. ile elimu ya awali hakuna kusoma.. ni kucheza tuu.. wanaruhusiwa kuzurura maeneo ya shule na kufanya chochote wanacho penda kukiwa na usimamizi kidogo.

Na wanasema imefanya watoto kuwa na ujasiri na ubunifu zaidi..

Mi nilikuwa najiuliza, kabla sijaenda sekondari tulikuwa tunatengeneza gari na usukani kiasi kwamba unaweza kupiga honi(kuna vitu tulikuwa tunaviunganisha.

Tumefika sekondari vipaji/ubunifu ziii.
Huwa sielewi ubunifu na kupaji vinapoteaje kadri mtu anavyozidi kusoma
 
Nadhani hakuna mwendelezo..
 
Huenda mtaala wetu wa elimu haujatoa kipaumbele kuibua vipaji toka nursery.

Ila tulifaidi ile michezo.
Hapo hujazungumzia zile baikeli za miti
Kuna siku head teacher aliamuru wote wenge baskeli zam wazilete shule ili zipasuliwe maana baadhi walikua wanatoroka shule na unatakiwa kuileta ikiwa nzima.

Shule ili jaa vile ibaskeli hadi mwalimu akaghairi kuzopasua maana wengine walionyesha ubunifu wa hali ya juu
 
Hii cha mtoto, sisi tulikuwa tunachukua tairi la lori au trekta unaingia hapo katikati unajikunja then wenzio wanakusukuma! Siku ingine wanakusukuma wanapoteza muelekeo wanakuacha upambane na hali yako!
View attachment 1101131
Ahahahhaa aiseeeeee umenikumbusha mbali sana.

Umeshawahi kukalia kuti alafu kuti linakaa juu ya kisuguu unawekea na nyasi kidogo sehemu ambazo litapita lile kuti ili kuwe la low friction alafu unaachia kuti(gubi zima lile la mnazi)basi unaseleleka nalo linaenda mpaka chini.huu mchezo huko kusini tumeucheza sana na yulishachana sana suruali engo za matakoni ila tunashkuru hakuna ambae alikosa njugu(pumbuh)

Ungine ni sarakasi kwa wale wanachingwea watakumbuka kwa mzee namadila kuna makana mengi tunaweka tairi kubwa la gari alafu tunaruka sarakasi hapo,siku moja kichwa choye kilizama kwenye makana hatari.

Tulikuwa tunaenda kuogelea kwenye sehemu flani flani hivi huko home sasa ikawa tunakunya humo humo yaaani staili ya kunya ni moja tuu.
Yaani unazama majini alafu unakunyaa ukiwa chini ya maji sasa mavi hayazami yanaelea na kutawanyika flani hivi..sasa kifuatachooo

unatakiwa upige chini kwa chini ukaibukee penginee kwa sababu ukiibuka hapo hapo unayavaa mavi yako yaani yanakua kofia(yapo kichwani) na kipindu pindu tulikuwa tunakiskia kwa jirani tu,rafiki zako wwoteeee tuliokuwa tunaoga nao hakuna hata mmoja aliekufa kwa kipindu pindu Mungu ashukuriwe sanaa

Enzi hizo wadada wakubwa bhana walikuwa wananimaindi sana mpaka ikafkia hatua wananiiba wanajigegedesha kwangu,ila saivi wakiniona wananisalimia tuu.

Waliiii wa sherehe tulikuwa tukitia mifukoni kabisaa unaepa nao huyooooo.

Nimecheza sana rede na mdako al manusra nigeuke shogaa ila washkaji wakanitonya mana nilikuwa najifanya mwana falsafa tokea utotoni,wakiniambia michezo nayocheza ya kike nawaambia hapana hakuna mchezo wa kike wala wa kiumee kwani kunya mchezo wa kike au wa kiume? Basi wanaduwaa ila baadaae nikaona mchezo hauna wanaume kabisa nikaacha falsafa zangu za kifwala.
 
Similar Discussions

24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom