Kama hii ni kweli basi sisi ni wajinga, iko siku litatugharimu

Kama hii ni kweli basi sisi ni wajinga, iko siku litatugharimu

Mtoto wa Kikwete amerekodi video kutoa tamko la familia yao kuwa wao ndiyo Tanzania.
 
Wamekutisha tu, very soon raisi atatoka Kaskazini. Don't fear them ✊✊
 
Msisahau na joshua nassari wakati wa kampeni mkoani Arusha aliwahi kutamka kwamba kama vipi kaskazini ijitenge na kujitangazia uhuru! Mbowe alipopewa nafasi ya kuzungumza akayakana maneno ya nassari akisema ni maneno yake mwenyewe, sio msimamo wa chadema.

Hawa wote ridhiwan, halfan na nassari wanapaswa kuchukuliwa hatua na dola ili iwe fundisho kwa wale wote wanaoleta chokochoko ili kuvuruga ustaarabu wa Taifa.
 
Mwazoni kabisa ilisemwa kuwa makabila makubwa hayawezi toa rais. makabila yaliyolengwa yalikuwa Wasukuma, Wachaga, Wahaya na Wanyakyusa. sasa Magufuli anatoka kabila kubwa.
wakati wa kampeni ukaskazini ulipigwa vita kumlenga Lowasa. Kusema kweli wamasai walikuwa na heshima kubwa hasa kupitia Sokoine. Hapa waliokataliwa sana ni wachagga. sasa wasingeweza kusema wachaga sababu Lowasa hakuwa mchaga. Siasa za ukanda na ukabila ni siasa mufilisi kupita kiwango.
 
Nafikiri nyote mnajua kwa kawaida mtu akishavimbiwa ni nini kinachofuata.
 
"Tukubali tukatae, nchi inapata uhuru, kilimanjaro ina shule zaidi ya 100 ilhali mkoani kwako kuna shule hazizidi 10.
Kwa hali hiyo lazima mtakuwa na wivu na chuki zisizo na mantiki na watu wa Kaskazini".
Pamoja na shule nyingi hivyo, mbona Nyerere aliwazidi kete kwa kuwa Rais wa Kwanza Tanganyika ambaye hakutokea huko!
 
Hata mimi nashangaa hapo. Rais wa awamu ya tano Dr. Magufuli anatoka kaskazini, sasa hawa jamaa wanalalamika nini?
Kaskazini aliyoimaanisha huyo kijana ni mikoa mitatu tu, yaani Arusha, Manyara na Kilimanjaro. Hiyo ndiyo mikoa anayoichukia na ameazimia kuhakikisha kwamba haitoi kiongozi wa nchi. Yeye hana shida na Mara, Mwanza,Kagera, etc.
 
Hata mimi nashangaa hapo. Rais wa awamu ya tano Dr. Magufuli anatoka kaskazini, sasa hawa jamaa wanalalamika nini?
Duh, au nilifeli Jeografia. Pombe ni wa North!, sasa magharibi ya tz ni wapi!?
 
Mandela angekata tamaa asingefanikisha kuwakomboa watu aliokusudia kuwakomboa.
 
Mwazoni kabisa ilisemwa kuwa makabila makubwa hayawezi toa rais. makabila yaliyolengwa yalikuwa Wasukuma, Wachaga, Wahaya na Wanyakyusa. sasa Magufuli anatoka kabila kubwa.
wakati wa kampeni ukaskazini ulipigwa vita kumlenga Lowasa. Kusema kweli wamasai walikuwa na heshima kubwa hasa kupitia Sokoine. Hapa waliokataliwa sana ni wachagga. sasa wasingeweza kusema wachaga sababu Lowasa hakuwa mchaga. Siasa za ukanda na ukabila ni siasa mufilisi kupita kiwango.

Ilisemwa kipindi cha mfumo wa chama kimoja. Hata hivyo neno la J.K.Nyerere sio sheria! Au unaweza kuonesha ni kifungu gani kwenye katiba kinachosema rais asitoke kwenye hayo makabila?
 
Mwazoni kabisa ilisemwa kuwa makabila makubwa hayawezi toa rais. makabila yaliyolengwa yalikuwa Wasukuma, Wachaga, Wahaya na Wanyakyusa. sasa Magufuli anatoka kabila kubwa.
wakati wa kampeni ukaskazini ulipigwa vita kumlenga Lowasa. Kusema kweli wamasai walikuwa na heshima kubwa hasa kupitia Sokoine. Hapa waliokataliwa sana ni wachagga. sasa wasingeweza kusema wachaga sababu Lowasa hakuwa mchaga. Siasa za ukanda na ukabila ni siasa mufilisi kupita kiwango.

Ukweli ni kwamba Magufuli si Msukuma, ni Mzinza. Pia Lowassa si Mmasai kwa asili, ni Mmeru kwa baba na mama ila waliloea Umasaini. Kama nimekosea nisahihishe tafadhali.
 
Salamus!

Kuna jambo limekuwa likinisumbua muda sasa ila nilitaka nijipe muda kuona Je, linakanushwa ima na serikali au chama tawala lakini mpaka sasa hakuna upande wowote ulio kanusha au kulitolea ufafanuzi. Kwangu mimi jambo hili ni baya na pengine ndilo litakalo nishawishi mimi niingie kwenye siasa ili nipate jukwaa mujarabu kulikema kwa akili zangu zote na kwa nguvu zangu zote kabisa.

Siku moja nilikutana na maneno haya " KAMWE RAIS WA NCHI HII HATAKAA ATOKE KASKAZINI MWA NCHI" ikiwa ni TWEET YA MH RIDHIWANI KIKWETE na baada ya uchaguzi wa 2015 akasisitiza kwa kusema maneno yaleyale akimaanisha kuwa hakukosea ni kweli kwamba Rais wa Nchi hii kamwe hatatoka kaskazini mwa Nchi! In whichever capacity is talking, whether is serious or not, binafsi napenda nichukue nafasi hii kulani kwa nguvu zangu zote kuwa ni wazo baya ambalo halifai kutamkwa na mtu yeyote mwenye akili timamu. Je, ni msimamo wa serikali au chama? Hakuna ajuaye lakini kweli kuwa hakuna upande ulio kanusha wala kulitolea ufafanuzi wowote. KUBAGUA WATU KULINGANA NA MAENEO WANAYO TOKA KWA SABABU YOYOTE ILE NI DHAMBI TENA NI DHAMBI MBAYA SANA.

Mkianza kuwatenga iko siku watatutenga! Halafu hivi haiwezekani karne hii mtu aendelee kuwaza kikaburu na watu wote tukakaa kimya! Unapenda kodi zao kwa ajili ya maendeleo ya Nchi halafu unadhulumu haki yao ya msingi kabisa ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa viongozi wa Nchi?

Wito wangu ni kuwa hekima, umoja, na amani ya Taifa ni bora kuliko mahitaji yenu ya kisiasa, ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda na kudumisha umoja wetu. Tupambane na makaburu weusi kama tulivyo wapinga makaburu weupe, ni walewale.

Yalikua maneno tu yale ambayo kwa wanasiasa wenyewe wala hayawatii presha kama wafuasi wao. Ukisikiliza hotuba za Maalim Seif dhidi ya Kikwete utafikiri labda wakikutana mmoja anaweza kumla nyama mwenzake but recently tumeona live wanaongea na kucheka hadi meno 32 karibu yote yanaonekana. Ukitaka kuamini kwamba wanasiasa wanacheza za akili za mashabiki wao tumia sekunde kadhaa kuzipima kauli za EDO kabla ya kukatwa ccm na kauli za sumaye kabla ya kupitishwa mgombea wa ccm then tafakari nini kilitokea kati ya wawili hao. Kauli za wanasiasa ukizibeba kama zilivyo unaweza kupata ugonjwa wa moyo wakati wenyewe maisha yanakwenda kama kawaida. kauli za wanasiasa zichukulie kama maneno yanayoandikwa JF!!!! Maneno mengi ni mzaha mtupu na ya kuondolea stress
 
Kaskazini aliyoimaanisha huyo kijana ni mikoa mitatu tu, yaani Arusha, Manyara na Kilimanjaro. Hiyo ndiyo mikoa anayoichukia na ameazimia kuhakikisha kwamba haitoi kiongozi wa nchi. Yeye hana shida na Mara, Mwanza,Kagera, etc.
Hiyo ni tafsiri yako. Sina shida nayo.
 
Mi naamini issue ya ukaskazini haina uhusiano na hayo ila ni style ya maisha ya hao jamaa mnaowaita wa kaskazini.Utamaduni wao wa maisha ya uwekevu,Nidhamu yao katika shughuli zao na ile economic base

Na hapa ndipo wanapolenga kisa wamepitwa kila mahali sasa kuongelea ukaskazini ka sehemu ya kujipoozea chuki na machungu yao.
 
"Tukubali tukatae, nchi inapata uhuru, kilimanjaro ina shule zaidi ya 100 ilhali mkoani kwako kuna shule hazizidi 10.
Kwa hali hiyo lazima mtakuwa na wivu na chuki zisizo na mantiki na watu wa Kaskazini".
Pamoja na shule nyingi hivyo, mbona Nyerere aliwazidi kete kwa kuwa Rais wa Kwanza Tanganyika ambaye hakutokea huko!

Na chimbuko la hii kauli unaijua ilitoka kweny utawala wa nani?...Na ni kwa nni walengwe watu wa kaskazini?
 
Back
Top Bottom