JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,156
- 3,628
Salamus!
Kuna jambo limekuwa likinisumbua muda sasa ila nilitaka nijipe muda kuona Je, linakanushwa ima na serikali au chama tawala lakini mpaka sasa hakuna upande wowote ulio kanusha au kulitolea ufafanuzi. Kwangu mimi jambo hili ni baya na pengine ndilo litakalo nishawishi mimi niingie kwenye siasa ili nipate jukwaa mujarabu kulikema kwa akili zangu zote na kwa nguvu zangu zote kabisa.
Siku moja nilikutana na maneno haya " KAMWE RAIS WA NCHI HII HATAKAA ATOKE KASKAZINI MWA NCHI" ikiwa ni TWEET YA MH RIDHIWANI KIKWETE na baada ya uchaguzi wa 2015 akasisitiza kwa kusema maneno yaleyale akimaanisha kuwa hakukosea ni kweli kwamba Rais wa Nchi hii kamwe hatatoka kaskazini mwa Nchi! In whichever capacity is talking, whether is serious or not, binafsi napenda nichukue nafasi hii kulani kwa nguvu zangu zote kuwa ni wazo baya ambalo halifai kutamkwa na mtu yeyote mwenye akili timamu. Je, ni msimamo wa serikali au chama? Hakuna ajuaye lakini kweli kuwa hakuna upande ulio kanusha wala kulitolea ufafanuzi wowote. KUBAGUA WATU KULINGANA NA MAENEO WANAYO TOKA KWA SABABU YOYOTE ILE NI DHAMBI TENA NI DHAMBI MBAYA SANA.
Mkianza kuwatenga iko siku watatutenga! Halafu hivi haiwezekani karne hii mtu aendelee kuwaza kikaburu na watu wote tukakaa kimya! Unapenda kodi zao kwa ajili ya maendeleo ya Nchi halafu unadhulumu haki yao ya msingi kabisa ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa viongozi wa Nchi?
Wito wangu ni kuwa hekima, umoja, na amani ya Taifa ni bora kuliko mahitaji yenu ya kisiasa, ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda na kudumisha umoja wetu. Tupambane na makaburu weusi kama tulivyo wapinga makaburu weupe, ni walewale.