Kama hii ni kweli basi sisi ni wajinga, iko siku litatugharimu

Kama hii ni kweli basi sisi ni wajinga, iko siku litatugharimu

Na chimbuko la hii kauli unaijua ilitoka kweny utawala wa nani?...Na ni kwa nni walengwe watu wa kaskazini?
Wataisoma namba kwa ukabila wao. Mrema alishindwa mwaka 1995 na Lowassa mwaka 2015 kwa sababu hizo hizo!
 
kaskazini si tanzania.ila tu huwa wanavikwa utanzania serikali inapokusanya kodi
 
Usijiaminishe ujinga, kwa kuwa kasema mtoto wa raisi? by then alichaguliwa JK na sio familia yake acheni woga waki lofa. Watanzania kwa ujumla wao ndio wanaamua nani raisi. Mtoa mada yuko clear nyie ni wajinga ma ,mie nimejtoa sio mjinga sababu mtoto wa JK kaSema.

Hujastuka kwamba statement yako ni ya kijinga kupitiliza?Ridhiwani sio tu kwamba ni mpiga kura...alikuwa mtoto wa rais wa nchi hii kwa kipindi cha miaka 10...na baba yake ameondoka ikulu juzi tu...kwa akili yako unadhani statement kama hizo ni busara zitoke ikulu kwa mwana wa rais?
 
Salamus!

Kuna jambo limekuwa likinisumbua muda sasa ila nilitaka nijipe muda kuona Je, linakanushwa ima na serikali au chama tawala lakini mpaka sasa hakuna upande wowote ulio kanusha au kulitolea ufafanuzi. Kwangu mimi jambo hili ni baya na pengine ndilo litakalo nishawishi mimi niingie kwenye siasa ili nipate jukwaa mujarabu kulikema kwa akili zangu zote na kwa nguvu zangu zote kabisa.

Siku moja nilikutana na maneno haya " KAMWE RAIS WA NCHI HII HATAKAA ATOKE KASKAZINI MWA NCHI" ikiwa ni TWEET YA MH RIDHIWANI KIKWETE na baada ya uchaguzi wa 2015 akasisitiza kwa kusema maneno yaleyale akimaanisha kuwa hakukosea ni kweli kwamba Rais wa Nchi hii kamwe hatatoka kaskazini mwa Nchi! In whichever capacity is talking, whether is serious or not, binafsi napenda nichukue nafasi hii kulani kwa nguvu zangu zote kuwa ni wazo baya ambalo halifai kutamkwa na mtu yeyote mwenye akili timamu. Je, ni msimamo wa serikali au chama? Hakuna ajuaye lakini kweli kuwa hakuna upande ulio kanusha wala kulitolea ufafanuzi wowote. KUBAGUA WATU KULINGANA NA MAENEO WANAYO TOKA KWA SABABU YOYOTE ILE NI DHAMBI TENA NI DHAMBI MBAYA SANA.

Mkianza kuwatenga iko siku watatutenga! Halafu hivi haiwezekani karne hii mtu aendelee kuwaza kikaburu na watu wote tukakaa kimya! Unapenda kodi zao kwa ajili ya maendeleo ya Nchi halafu unadhulumu haki yao ya msingi kabisa ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa viongozi wa Nchi?

Wito wangu ni kuwa hekima, umoja, na amani ya Taifa ni bora kuliko mahitaji yenu ya kisiasa, ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda na kudumisha umoja wetu. Tupambane na makaburu weusi kama tulivyo wapinga makaburu weupe, ni walewale.

Kwa Uchaguzi wa mwaka huu hapakuwa na mtu mwenye sifa za kuwa Rais tofauti na Dr. Magufuli.
 
Na hapa ndipo wanapolenga kisa wamepitwa kila mahali sasa kuongelea ukaskazini ka sehemu ya kujipoozea chuki na machungu yao.
Na hii ndiyo shida ya nchi hii ina wana siasa wa kufedhehesha kwani haiingii akilini kwa mtu mwenye uelewa ndani ya chama kama ccm ajitoe akili na kutaka kutumia tofauti ya stadi za maisha ya Watanzania ili kuwafarakanisha kisa eti aendelee kubaki madarakani.
 
Ulisoma jiografia kweli?

Kaskazini mwa Tanzania ni wapi?
Bi dada nadhani umeathiriwa na neno Kanda ya Ziwa ukasahau Map reading na compass direction ya ramani ya nchi yako. Pitia upya.

Moreover anguko la chama chako ulitumie kama funzo la wewe kutumia akili yako kuliko kupelekwa kinyumbu, najua unaweredi sana ila ulikumbwa na ushabiki wa kikanda. Rudi angalia taarifa unazolishwa na kuzitumia je ni sahihi? Hii yenyewe was fake na dogo alikanusha sana lakini mpaka Leo kunamtu asiyefanya tafiti hata kidogo anaianzishia uzi! Full of nonsense lakini utaona watu wanamuunga mkono kinyumbu nyumbu tu.
 
Nasisitiza rais hatoki kaskazini.


Atoke asitoke, nchi nzima ya Tanzania itasubiri saaaaaaaaana kuifikia kaskazini kwa namna yoyote ile kwa maana hiyo utakaa sanaa na kuchuchumaa lakini kaskazini ndio mambo yote! mfano wa Tanzania uko pale wherever!
 
kama ni ubaguzi wa kikanda, vipi kuhusu lowasa alivyoenda kanisani kuomba kura wakati wa kampeni iringa??
huo si ndo ubaguzi wa kidini??
kwamba mwaka huu ulikua wa walutheri kuongoza nchi, maana waislam na wakristo ndo wameongoza miaka yote.
ukitaka kusema angalia kwanza kwenu mnamadudu gani mliyafanya .
 
Ni kweli kabisa Jelly Fish. Kunawakati Mwl Nyerere aliwakemea kwa tabia hizo. Na wengi wao walitimuliwa jeshini na kupelekwa sehemu nyine za kazi. Shuleni, KAMATA, hifadhi ya wanyama nk. Nikeli kabisa. Natusipoikea tuta haribu nchi hii kwa Majimbo yao
 
Ukweli ni kwamba Magufuli si Msukuma, ni Mzinza. Pia Lowassa si Mmasai kwa asili, ni Mmeru kwa baba na mama ila waliloea Umasaini. Kama nimekosea nisahihishe tafadhali.
mkuu, hujakosea. ila ukichunguza sana utagundua kuwa makabila tunayotambuliwa nayo si halisi sana kutokana na kuhamahama au kuoleana. asili ya watanzania wengi ni Ubantu, unailo na ukush. wachache ni khoisan ambao asili yao ni hapahapa Tz. wengine wote ni wahamiaji. miaka mingi ijayo itakuwa vigumu kupata asili ya kabila la mtu. maingiliano yatakuwa yamefuta makabila kwa kiasi kikubwa.
 
JERUSALEMU, usitafute sababu ya kuingia CDM, we ingia tu, ni haki yako ya kikanda.BTW, kanda ya kaskazini ni wao ndio wanajitenga kwenye siasa za Tz na sio wa Tz wanaowabugua.
Maoni yangu yanalenga kuchukua tahadhari ili siku moja tusianze kuulizana nani kasababisha. kwa mbali naanza kuona UKAWA TERRITORY Kwa maana kwamba iko siku hawa wanao baguliwa mkaona wanashinda majimbo yote ya kaskazini kwa maana ya TANGA YOTE, KILIMANJARO YOTE , ARUSHA YOTE NA MANYARA hapo kutakuwa na TANZANIA TENA? Dhambi ya ubaguzi ni mbaya na kila anae taka kutupeleka huko lazima alaaniwe kwa nguvu zote.
 
Haya mambo yalishaisha baada ya uchaguzi.Mbona chokochoko ? Lowasa ameshindwa kwa kura.Na kwenye kanda yake
alishinda kwa kweli isipokuwa kwenye kanda nyingine alipigwa chini.
 
Unatakiwa ufikiri sana kabla ya kuleta mada za chuki tushirikiane kujadili.Kaskazini unakomanisha ni wapi? kwa nini mnauwaza sana urais.Na ndiyo maana mkahamia wote chadema baada ya kukatwa ccm.Stupidy.msitupandikize chuki hapa mkimaliza ukask mtakuja umarangu na ukibosho
 
Kauli hii huenda ni ya kuchonga but jamaa alishawahi kusema hivyo awali, kwa hiyo kinachoendela leo hii ni nukuu tu.

Anyway, labda ana sababu zake za msingi kusema hivyo. Cha ajabu yeye na rafiki zake wamewekeza huko kaskazini. GONGENI NA KULONGA KWA KAULI ZENU. ILA KUWENI MAKINI MSIJE GONGWA SIKU ZA USONI. Mamlaka na mali zina kikomo, pia umma unapochoshwa na chokochoko za hapa na pale hufanya maamuzi sio mazuri na ambayo hayaangalii kipato wala nafasi ya mtu ktk jamii.

HAKUNA UTAWALA UNAODUMU MILELE, ISIPOKUWA UFALME WA MWENYEZI MUNGU TU.
 
By the way ridhiwan ndo nan, watu tushamsahau kitaaambo
Ila ukweli watu wa Arusha/Moshi n wapigaji wakubwa siku wakiupata urais! Nchi itauzwa fasta, ila akitokea muadilifu wa vitendo sina shaka ataukwaa upresidaa

Mkuu naomba tuongee kwa evidence kabisa, nina orodhesha idadi ya kashfa hapa chini then nisaidie wahusika na wanakotoka:-
1. IPTL mwaka 1994.
2. Rada.
3. Ndege ya rais
4. Uuzwaji wa mashirika na makampuni ya serikali kifisadi.
5. Migodi.
6. EPA
7. Richmond/Dowans/Symbion.
8. Escrow
9. Mikataba ya gas.
10. Mwananchi Gold.
11. Tangold
12. Meremeta.
 
Stage One: Kiondoleeni chama chenu makando kando ya ukabila na ukanda ndiyo watu wataanza kuwaelewa. Kipeni chama mwonekano wa kitaifa. Acheni kuwatimua na kuwaChacha Wangwe wanaoleta mawazo critical ndani ya chama. Punguzeni gia za angani na kujiona kuwa nyie ndiyo alpha na omega hapa Tanzania. Vinginevyo hata upewe uenyekiti wa CDM wewe hutaweza kutoa rais kutoka Uchagani kama perception ndiyo hii ya ukabila na ukanda.

Mshikaji goli la mkono mlianza mwaka 2005 kwa Slaa, imejirudia tena na tena....labda ungesema tuache masunduku ya kura yaamue si owananchi walikuwa hawajielel



Stage III. Transparency kwenye matumizi ya pesa za ruzuku na rasilimali nyingine za chama. Madili yapungue! Mnatakiwa kuonyesha mfano katika hili ili kujipambanua

Stage III. Wapiga kura wengi wako vijijini na siyo mijini pekee na JF. Fanyeni juhudi za makusudi kuwafuata huko vijijini. Na siyo Moshi, Kilimanjaro na Mbeya pekee.

Stage IV. Andaeni viongozi wenu wenyewe na siyo kutegemea makapi yanayonuka kutoka CCM.

Stage V. Chama chenu kinahitaji falsafa tambulishi. Baada ya kupoteza ile ya kupinga ufisadi kwa kumkaribisha kingunge wa ufisadi Bongo kama mgombea wenu, sasa chama hakina moral compass na kinaenda tu kama boya katika bahari kuu iliyochafuka. Chama chenu kinasimamia nini? Kwa sasa hakuna anayejua.

Stage VI...

Najua pengine mtatukana kama ilivyo kawaida yenu lakini huu ndo ukweli. Vinginevyo tutawapa PhD ya kulalamika na kupinga kila kitu huku mkidai kuwa mnaonewa as if anyone cares!


Anachukua Napei , Napei anakwenda, kapa anatuliza kifuani, Paaaaasi ndeeefu inamkuta nanii huyu, aaah ni mchezaji mwenye jina la bolisi, bolisi anakwenda...hatari jamani, anagonga mpira kwa kisigino kwenda wake Buvaa, buvaa anajikunjaa kama messi, gooooooooal gooooal,. Naam ajabu ni mkono ndio golim la mkono, refarii anasema mpira kati, naaam mpira umekwisha. Upande wa pili hawaamini kilichotokea mshika kibendera nae kajichangakiwa bado na kibendera juu.
 
Hata mimi nashangaa hapo. Rais wa awamu ya tano Dr. Magufuli anatoka kaskazini, sasa hawa jamaa wanalalamika nini?
Uh siku hizi CHATO ni kanda ya kaskazini....Biharamulo Geita...tusome tena jiografia vizuri
 
Back
Top Bottom