Kama hii ni kweli basi sisi ni wajinga, iko siku litatugharimu

Kama hii ni kweli basi sisi ni wajinga, iko siku litatugharimu

Salamus!

Kuna jambo limekuwa likinisumbua muda sasa ila nilitaka nijipe muda kuona Je, linakanushwa ima na serikali au chama tawala lakini mpaka sasa hakuna upande wowote ulio kanusha au kulitolea ufafanuzi. Kwangu mimi jambo hili ni baya na pengine ndilo litakalo nishawishi mimi niingie kwenye siasa ili nipate jukwaa mujarabu kulikema kwa akili zangu zote na kwa nguvu zangu zote kabisa.

Siku moja nilikutana na maneno haya " KAMWE RAIS WA NCHI HII HATAKAA ATOKE KASKAZINI MWA NCHI" ikiwa ni TWEET YA MH RIDHIWANI KIKWETE na baada ya uchaguzi wa 2015 akasisitiza kwa kusema maneno yaleyale akimaanisha kuwa hakukosea ni kweli kwamba Rais wa Nchi hii kamwe hatatoka kaskazini mwa Nchi! In whichever capacity is talking, whether is serious or not, binafsi napenda nichukue nafasi hii kulani kwa nguvu zangu zote kuwa ni wazo baya ambalo halifai kutamkwa na mtu yeyote mwenye akili timamu. Je, ni msimamo wa serikali au chama? Hakuna ajuaye lakini kweli kuwa hakuna upande ulio kanusha wala kulitolea ufafanuzi wowote. KUBAGUA WATU KULINGANA NA MAENEO WANAYO TOKA KWA SABABU YOYOTE ILE NI DHAMBI TENA NI DHAMBI MBAYA SANA.

Mkianza kuwatenga iko siku watatutenga! Halafu hivi haiwezekani karne hii mtu aendelee kuwaza kikaburu na watu wote tukakaa kimya! Unapenda kodi zao kwa ajili ya maendeleo ya Nchi halafu unadhulumu haki yao ya msingi kabisa ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa viongozi wa Nchi?

Wito wangu ni kuwa hekima, umoja, na amani ya Taifa ni bora kuliko mahitaji yenu ya kisiasa, ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda na kudumisha umoja wetu. Tupambane na makaburu weusi kama tulivyo wapinga makaburu weupe, ni walewale.

Ccm haipo kwa maslahi ya wananchi ipo kwa maslahi ya wakubwa tu kujinafsisha rasilimali za nchi tu. Leo unaitwa mtanzania lakini cha ajabu utaambiwa huwezi kuwa rais au kiongozi wa juu kwasababu unatoka kaskazini tu.
 
Uh siku hizi CHATO ni kanda ya kaskazini....Biharamulo Geita...tusome tena jiografia vizuri
Wewe mburula hapa tunazungumza kuhusu jiografia na sio hizo "kanda" zako za kusadikika.
 
kama ni ubaguzi wa kikanda, vipi kuhusu lowasa alivyoenda kanisani kuomba kura wakati wa kampeni iringa??
huo si ndo ubaguzi wa kidini??
kwamba mwaka huu ulikua wa walutheri kuongoza nchi, maana waislam na wakristo ndo wameongoza miaka yote.
ukitaka kusema angalia kwanza kwenu mnamadudu gani mliyafanya .

Ni tabora sio iringa mkuu
 
Watanzania tunafanya mizaha mizaha na matamko ya kibaguzi ya aina hiyo lakini iko siku yatatugharimu sana na wimbo wetu hu wa AMANI AMANI. Rwanda ukisema maneno kama hayo ni kosa la jinai, Tatizo mbona Ridhiwani haonywi hata na Babayake kama Baba? Mbona CCM haikanushi na kumwonya. Wanamsingizia Nyerere alisema maneno hayo si Kweli Nyerere alikuwa na busara na mwangalifu sana na matamko yake haswa kauli za kibaguzi. Alipigia kelele sana TUSIBAGUANE. Namshauri Ridhiwani Kikwete atoke aombe msamaha na afute hiyo kauli.
 
Anachukua Napei , Napei anakwenda, kapa anatuliza kifuani, Paaaaasi ndeeefu inamkuta nanii huyu, aaah ni mchezaji mwenye jina la bolisi, bolisi anakwenda...hatari jamani, anagonga mpira kwa kisigino kwenda wake Buvaa, buvaa anajikunjaa kama messi, gooooooooal gooooal,. Naam ajabu ni mkono ndio golim la mkono, refarii anasema mpira kati, naaam mpira umekwisha. Upande wa pili hawaamini kilichotokea mshika kibendera nae kajichangakiwa bado na kibendera juu.
Ndiyo siasa hizo. Ni mchezo wa kuzidiana ujanja. We kalia kumlalamikia refa au mshika kibendera itakula kwako. Hata Maradona INASEMEKANA aliwahi kufunga goli la mungu tena kwenye kombe la dunia...Ha ha haaaaaa !!!
 
Usihofu, ni maneno ya wanasiasa tu hayo. Mbona hao wa kaskazini huwaita wanaoichagua ccm wajinga, wasiojitambua? Ukweli ni kwamba akitokea mtu kaskazini muadilifu, mchapa kazi, asiye na ndimi mbili, asiye mdini, asiye endekeza ukabila au ukanda, asiye tumia fedha kutafuta uongozi, anayeweza kukemea rushwa na ufisadi hadharani, asiye na rubani anayebadili gia angani, mwenye afya njema, msomi, kwanini asichaguliwe? Bado hajatokea. Upo?

Halfan kikwete anaweza kukujibu ccm milele hata akitokea malaika ni ccm tu!! Hapo umeongea propaganda ila sio ukweli!!
 
Wao Wakisema kaskazini wanamaanisha Rais awe mchagga suala ambalo halitatokea kamwe.

Inawezekana akaja kuwepo rais mchaga kizazi chetu kikiwa hakipo!! Unanishangaza kumbe kadhambi ka ukabila kanakutembelea, tukianza kuangalia na kuchaguana kulingana na makabila tutaanza kuchinjana na nyerere aliikemea dhambi hii kwanguvu sana! Mungu ibariki tanzania na watanzani tuepushie hawa wanaoanza kuangalia wenzao kwa makabila wape moyo wa kujua ss sote ni watanzani!!!! Amen
 
JERUSALEMU, usitafute sababu ya kuingia CDM, we ingia tu, ni haki yako ya kikanda.BTW, kanda ya kaskazini ni wao ndio wanajitenga kwenye siasa za Tz na sio wa Tz wanaowabugua.

Sipend attitude na trait za ridhiwani,but what you have said is true,kaskazin wao ndio wanajitenga..they are trying to come up with what we call syndicate,sio kitu kizuri
 
Last edited by a moderator:
Kwani Ridhiwani ni msemaji wa Chama kipi mpaka kauli yake ichukuliwe kama msimamo wa hicho chama?Yaani chama kiwe kinakanusha kila uharo wa wanachama wake tena waliouandika kwenye mitandao ya kijamii?Nyie jamaa mmebaki na vihoja vya kuokoteleza tu visivyo hata na mashiko.

Tuangalie maslai mapana ya taifa kinacho andikwa na mtoto wa rais pili ni mmbunge anaeingia bungeni!! Kupuuza kupo ila akiwa km kioo cha jamii hapaswi kuongea mambo hayo kwenye hadhara aonge ndani na mkewe ila hadharani kauli hizo hazijengi bali zinaanza kubomoa akili za watu ambazo nyerere alizijenga miaka mingi iliyopita na akili za watu wanaosoma au kusikia maneno ya watoto wa aliyekuwa raisa wakijitapa zinaa kupata ufa usipozibwa ukuta utaanguka siku wasioijua!! Mungu ilinde tanzania na amani yake tuondolee wenye maneno ya makufuru wanaojaribu kuumiza akili za watanzani tupe uvumilivu na upendo wa kweli!!!!! Ameni
 
Msisahau na joshua nassari wakati wa kampeni mkoani Arusha aliwahi kutamka kwamba kama vipi kaskazini ijitenge na kujitangazia uhuru! Mbowe alipopewa nafasi ya kuzungumza akayakana maneno ya nassari akisema ni maneno yake mwenyewe, sio msimamo wa chadema.

Hawa wote ridhiwan, halfan na nassari wanapaswa kuchukuliwa hatua na dola ili iwe fundisho kwa wale wote wanaoleta chokochoko ili kuvuruga ustaarabu wa Taifa.

Hatua tutachukuliwa ss makajamba nani huku sema ww uone!!! Utapotea ka kaushuzi ka yusufu
 
JERUSALEMU, usitafute sababu ya kuingia CDM, we ingia tu, ni haki yako ya kikanda.BTW, kanda ya kaskazini ni wao ndio wanajitenga kwenye siasa za Tz na sio wa Tz wanaowabugua.

Ushauri wangu kwa hao watu wanaoitwa wa kanda ya Kaskazini ni kama wanaweza wajitenge kwa kuwa inaonekana kanda nyingine zimewatenga. Inaonekana kuna chuki kubwa sana kwa hao watu. Na sababu kubwa ni kwamba wamekuwa mwiba kwa siasa za CCM hata kabla ya utaratibu wa vyama vingi kuanza.
 
Last edited by a moderator:
Ingekuwa kweli kasema kina mzee msuya hawangekaa kimya,hata hivo rizone ni mtu mmoja tu,sio sera ya nchi rais asitoke uchagani

kama nimemuelewa vizuri mtoa mada, walau TAMKO au ONYO litoke kwa hiyo kauli. Litoke serikalini au ccm.
 
Mbona hata Halfan Kikwete alisema dhahir tena kwa sauti "kwamba wao ndiyo Tanzania na wao ndiyo dola na kwamba watatawala milele, na atakaeyewapinga atapigwa na kudhalilishwa kwa kuwa nchi hii ni ya kikwte na familia yake?

Mbona maneno haya yangetamkwa kwa nchi zenye binadamu wenye akili kikwete alitakiwa atoe ufafanuzi kama ana hatimiliki ya nchi hii kama vile familia yake ilivyosema.

Hii familia ilijiona na kujisikia sana uraisi ulikuwa wa kifamilia na sio taasisi! ndio maana kila kitu kilikuwa kinakwenda kindugu,urafiki, na kujuana.Ndio maana tumerudi chuma ya pale awamu ya 3 ulipotuacha ILA KWA SASA KAMWE RAISI HATATOKA TENA UKANDA WAO.
 
Hii familia ilijiona na kujisikia sana uraisi ulikuwa wa kifamilia na sio taasisi! ndio maana kila kitu kilikuwa kinakwenda kindugu,urafiki, na kujuana.Ndio maana tumerudi chuma ya pale awamu ya 3 ulipotuacha ILA KWA SASA KAMWE RAISI HATATOKA TENA UKANDA WAO.

Ukanda huo piga ua hatatokea raisi tena. Wapumbavu sana wametuharibia na chama chetu.
 
nitajieni mawaziri wateule kutoka Kilimanjaro,arusha na Manyara ndo nichangie,
 
Asante cyberspace ndg Bavaria umeona jibu hilo malidhawa! North or South it depend the location you're.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom