Kama Dunia inazunguka jua kwa Spidi kubwa kwanini vyombo vilivyo nje ya dunia haviachwi?

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,154
11,207
Wanasayansi wanasema dunia hulizuguka jua kwa speed ya 1609.344 kilomita kwa lisaa limoja tu, hivyo kumbe dunia ipo katika speed kubwa ya kulizunguka jua ndio maana tunapata usiku na mchana na majira ya mwaka.

Lakini ikumbukwe kuwa nnje ya uso wa dunia wanasayansi wametuma vyombo vingi sana ambavyo vipo katribu na uso wa Dunia kwaajili ya utafiti wa mambo ya anga na vingine kwa ajili ya mawasiliano na miongoni mwa vyombo hivyo ni

•ISS ~INTERNATIONAL SPACE STATION

•SATELLITE

iss-20190131-0001.jpeg


nouvelles-2018-11-29-dragon-id-11441.jpeg


Kama vyombo hivi vimetulia angani nnje ya uso wa Dunia kwa nini huwa haviachwi na Dunia kwa kuwa huwa inazunguka kwa Speed kubwa ya 1609.344 kilomita kwa saa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari mkuu. Naomba nijibu kutokana uelewa wangu kidogo nafikiri hivyo vyombo haviachwi na dunia kwa sababu vipo kwenye anga ya dunia nikiwa namaana kwamba vipo kwenye kani ya mvutano wa dunia (earth's gravitational force).
Pili hivi vyombo huwa vinawekwa kwenye 0 gravity area yaan sehem ambayo kani ya mvutano kati ya mwezi na dunia huwa pako balanced yaan hauwezi kuenda juu au kuenda chini kwani kani ya mvutano kati ya dunia na mwezi ni sawa au ni sifuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari mkuu. Naomba nijibu kutokana uelewa wangu kidogo nafikiri hivyo vyombo haviachwi na dunia kwa sababu vipo kwenye anga ya dunia nikiwa namaana kwamba vipo kwenye kani ya mvutano wa dunia (earth's gravitational force).
Pili hivi vyombo huwa vinawekwa kwenye 0 gravity area yaan sehem ambayo kani ya mvutano kati ya mwezi na dunia huwa pako balanced yaan hauwezi kuenda juu au kuenda chini kwani kani ya mvutano kati ya dunia na mwezi ni sawa au ni sifuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nikuongezee swali tu,
kama ni kwa spidi hiyo mbona hatuhisi kizungu zungu?
Kwa sababu mzunguko ni mkubwa sana,yaani umbali toka kati kati jua ambapo ndio kani ya mvutano inakuwa kama mhimili wake hadi kwenye dunia. Hii inafanya mzunguko kuwa mdogo kias kwamba hatuwezi kuhisi au kuona kizungu zungu au kuhisi kama dunia inazunguka jua na inajizungusha yenyewe kwenye mhimili wake ambao ni usumaku (magnetic axis)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kingine ni kwamba sisi tunazunguka na dunia kwani tupo kwenye uso wadunia sisi pamoja na vitu vingine kama bahari,milima nk hii inatufanya tuzunguke kwa spidi sawa na dunia. Mfano ukiwa kwenye gari unakuwa na spidi sawa na gar na ndio maana dereva akiweka breki lazma abiria atokee kioo cha mbele kwani gari inasimama wakati abiria bado yupo kwenye spidi
IMG_20190131_083427_760.JPG


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kingine ni kwamba sisi tunazunguka na dunia kwani tupo kwenye uso wadunia sisi pamoja na vitu vingine kama bahari,milima nk hii inatufanya tuzunguke kwa spidi sawa na dunia. Mfano ukiwa kwenye gari unakuwa na spidi sawa na gar na ndio maana dereva akiweka breki lazma abiria atokee kioo cha mbele kwani gari inasimama wakati abiria bado yupo kwenye spidiView attachment 1009209

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa, ni kweli dereva hawezi kukiacha kiti cha gari wakati vyote vipo kwenye mwendo. Ila sasa mwezi na jua na mawingu hatuko navyo kwenye mwendo, mbona hatuviachi kwa hiyo speed tajwa?
 
Back
Top Bottom