Jiwe kubwa kudondokea dunia?

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Katika makala kadhaa za baadhi ya wadau wa mambo ya anga niliona moja ikisema kwamba kwa sababu ya Jupiter kukosea njia yake basi kuna mawe yatakuja kuipiga dunia ambayo yataiponyoka Jupiter.

Ukweli ni kwamba, Jupiter haijapotea njia wala haijakaribia Orbit ya mwezi, kinachoonekana Angani Jupiter kukaribia mwezi hiyo ni Alignment ya muonekano tu wa conjunction ya magimba angani ila Jupiter iko mbali sana.

Kuna mawe mengi sana angani, Mamilioni na mabilion ya mawe yanasafiri katika njia mbalimbali huko angani.

Mawe kadhaa huweza kuingia kwenye anga la Dunia mara kadhaa kwa mwaka, Mwezi au hata kila siku, kila dakika, kila sekunde. Mawe kadhaa ambayo huingia kwenye anga la dunia hukutana na kani za dunia mgandamizo wa hewa, joto na umeme kadhaa kwenye anga la dunia ambavyo husababisha mawe hayo kuungua na kuyeyuka.

Majira ya usiku huwa tunaweza kuona baadhi ya mawe ambayo huingia kwenye anga la Dunia yakiwa yanawaka Moto kama vimondo, huwa tunayaita nyota mkia (Comets)

Mara chache sana mawe kuingia kwenye anga la Dunia yakiwa makubwa kiasi kwamba yanaweza kuungua yasiishe na kuweza kutua duniani, mfano wake ni kimondo cha mbozi huko mbeya (nadhani sasa hivi ni Songwe) yanatakiwa kuwa makubwa sana na magumu.

Jiwe liliokuwa linatajwa kuingia kwenye anga la Dunia lina upana wa futi 110 tu likiwa na speed inayokadiriwa kuwa 2500km kwa saa, kwa speed hiyo jiwe hilo linaweza kuunguzwa kwa sekunde 5 tu likiingia kwenye Ionosphere ya Dunia.

Ionosphere ni kipengele cha Atmosphere chenye charge za umeme juu kidogo ya Thermosphere amabayo yenyewe in joto.

Inawezekana ndio likawa limeingia kwenye anga la Dunia lakini limeungua hata kabla ya kufika Thermosphere kilomita karibu 1000 kutoka kwenye uso wa Dunia.

Hata hivyo Dunia ipo kwenye mwendo makali sana ikizunguka Jua, na mara nyingi mawe kwenye anga huwa hayafati njia ya sayari, yenyewe husafiri kwa njia yake, basi inawezekana wakati kimondo kinapita sehemu fulani ambayo ilikadiriwa kuipiga Dunia, Dunia ikawa imeshapita eneo hilo.

Kuna visababishi kadhaa vya kuweza kupishana kwa Sayari na Mawe yanayoweza kupigana huko angani, moja wapo ikiwa ni ukanda wa sumaku ya Sayari jirani au yenye nguvu, mfano Jupiter ina magnetic field ya kuweza kuzuia maelfu ya vimondo yasipige Dunia na Mars.

Gerald
geraldchristopher1@gmail.com
FB_IMG_1667853595876.jpg
 
Dogo elewa kwamba kila kitu unachokiona duniani hakikujiotea tu kama uyoga. Hata wewe kuamka asubuhi hukujiamkia tu, Uliamshwa.

Relax, aliyekuamsha asubuhi hawezi acha hilo jiwe likagonga dunia.

Mind you huko angani there's a lot of comets. And we're still here๐ŸŒน
 
Back
Top Bottom