Kama bado hajapimwa, kwanini asipimwe?

Kama bado hajapimwa, kwanini asipimwe?

Hapana mkuu.

Siku hizi hata ukionekana wayumbayumba kuelekea kwenye gari yako basi walokuona wanaweza kupiga simu polisi na kusimamishwa na moja kwa moja ukapimwa kiwango cha pombe.

Mpaka sasa naona ushahidi wote umekwishavurugwa na majeruhi amepelekwa DSM.

Naona kamanda Muroto anapata wakti mgumu kuandaa taarifa za uchunguzi.
Kuna sehemu hata ukiwa unatembea kwenye sidewalk huku unaonyesha dalili zote za kulewa, unaweza simamishwa, ukachunguzwa, na hata kupewa citation.

Kutembea huku unayumbayumba pembezoni mwa barabara kunahatarisha usalama wako.
 
Naona kuna ‘narratives’ mbili zinazokinzana kuhusu kilichomtokea Mwenyekiti wa taifa, CHADEMA.

Wapo waliodokeza kwamba alienda kunywa na wenzake, dizaini akanywa akapitiliza, akalewa chakari

Upande wa makamanda, wao wanadai eti kapigwa na watu wasiojulikana

Sasa sijui protokali za kibunge na za hiyo hospitali aliyopelekwa zikoje

Ila, katika kuutafuta ukweli, mimi napendekeza apimwe blood alcohol level yake

Ni wakati muafaka sasa kuanza kutumia sayansi kukata mizizi ya fitna
Eeeenh, maajabu makubwa hayo.

Mgonjwa apelekwe/aende hospitali kwa utashi wake, aishie kupimwa "blood alcohol"?
Na kama pendekezo la kupima ni baada ya sintofahamu iliyotokea, hiyo "blood alcohol" itakuwa inasubiri tu iwepo hadi ipimwe?

Lakini sijaona pendekezo au dokezo la huyo mgonjwa kupimwa sawia hapo hapo hospitali kuona kama kuna uharibifu sehemu nyingine ya mwili kutokana na kubamizwa kwake chini au na kitu chenye ncha butu au ncha kali!

Sijui kama "protokali" ya hospitali hiyo itakuwa inaishia kupima au kutibu majeraha makubwa yanayoonekana kama hayo ya kuvunjika kwa mguu wa anayedhaniwa kuwa "mlevi chakali". Nina hakika hiyo hospitali wataalam wamefanya kazi yao ipasavyo, kwa hiyo ni kusubiri tu itaeleweka kama ugonjwa unatokana na kushambiliwa, au kulewa chakali.

Lakini hawa wanaotafuta sababu za kujikosha, mbona wana haraka na kihererehere hivi!
 
Kwà ninavyoifahamu DODOMA, Mbowe hakupaswa kabisa kupelekwa huko DCMC na Sijui walitumia Protocal zipi kumpeleka kule Wakati General ipo na Hospitali ya kisasa kabisa Benjamin Mkapa ipo na ina vipimo vya kisasa kabisa na watoa huduma wenye weledi wakutosha kabisa!! Hili suala linafikirisha sana!??
[/QUOTE
Hakika inafikirisha,Dj kaleta taharuki nafikiri akipata nafuu aje atueleze ilikuwaje
 
Hapana mkuu.

Siku hizi hata ukionekana wayumbayumba kuelekea kwenye gari yako basi walokuona wanaweza kupiga simu polisi na kusimamishwa na moja kwa moja ukapimwa kiwango cha pombe.

Mpaka sasa naona ushahidi wote umekwishavurugwa na majeruhi amepelekwa DSM.

Naona kamanda Muroto anapata wakti mgumu kuandaa taarifa za uchunguzi.
Na kama unaenda kulala kwenye gari? Au unaenda kumsubiri designated driver? Na hata kama unaendesha ukiwa umekunywa, unasimamishwa na polisi kwa sababu kuendesha gari ukiwa umekunywa pombe zaidi ya kiwango fulani ( sio lazima uwe umelewa) ni kosa. Nasikia kuna nchi nyingine, polisi wanaweza kufanya random testing ili kuwakamata wale wote wanaovunja sheria ya kutoendesha gari wakiwa wamekunywa pombe kiasi fulani. Ninavyojua mimi KUB alikuwa anaeshwa na dereva kwa hiyo DUI haimhusu. Na kunywa pombe na hata kulewa sio kosa. Ila kuna vitendo unavyoweza kufanya ukiwa umelewa ndio kosa.
Mitazamo kama hii ni kama ile ya kukataa kumsikiliza msichana anaesema amebakwa kwa sababu tu amevaa nguo fupi, ingawa inaonekana wazi imechanwa na ana majeraha. Hivi tunapaswa kumpima kwanza kama kweli amebakwa au tusisitize tuhakikishe kama alikuwa amevaa nguo ya ndani?

Amandla...
 
Umewahi kumtumia pombe boss?
Ulevi unasababisha mengi.

Unaweza ukasababisha mtu kuanguka na kuumia halafu akashindwa kujua kaumiaje na kuanza kudai kapigwa ilhali hajapigwa.

Ulevi unaleta impairment. Hali inayoweza kumfanya mtu aone maruerue. Mfano, mtu aliyelewa anaweza kukikimbia kivuli chake akidhani ni mtu mwingine anayetaka kumtendea ubaya.

Kwa hiyo, suala la ulevi si la upili kama unavyodai wewe. Ni suala la msingi kabisa, hususan katika kuutafuta ukweli.
 
Umewahi kumtumia pombe boss?
Karibu

0407F5B5-9819-4E86-9DA1-EF9A3BE5CC7D.jpeg
 
NAVYOJUA MGONJWA ALIEVUNJIKA AKIFIKISHWA HOSPITAL, LAZIMA DR AMWANGALIE AMEVUNJIKAJE, JE KAVUNJIKA KWA KUPIGWA AU KWA KUANGUKA MWENYEWE AU KWA AJALI? NA KAMA NI KWA KUPIGWA KUNA MAJERAHA MENGINE UTAYAONA YA KUASHIRIA KUPIGWA NA KAMA NI KUANGUKA KUNA MICHUBUKO LAZIMA UTAIONA SEHEMU NYINGINE KAMA MKONONI AU USONI LAZIMA KUTAKUA NA MIKWARUZO FLANI AU MAJERAHA.
SASA HAPA DR NDIO ALITAKIWA ATOE MAJIBU YA MGONJWA WALIBAINI KAVUNJIKA VIPI, ILA NACHOSHANGAA SPIKA KASHAPATA MAJIBU NA KUYATOA BUNGENI KINYUME NA TARATIBU ZA KIAFYA. KIAFYA HAIRUHUSIWI DR KUTOA MAJIBU YA MGONJWA KWA MTU ASIYEHUSIKA NA NI KINYUME NA MAADILI YA KITABIBU, SASA SIJUI LIJUALIKALI NA SPIKA NA MUSUKUMA WALIPATA WAPI MAJIBU YA KUSEMA MBOWE ALIANGUKA BAADA YA KUNYWA FARU JOHN.
PIA KAMANDA WA POLISI ALISEMA HILI JAMBO LISICHUKULIWE KISIASA, ILA MPAKA SASA BUNGENI LIMESHAGEUZWA KISIASA NA HAKUNA ALIYEFANYWA CHOCHOTE NA KAMANDA MUROTO.
JE UNATEGEMEA MAJIBU YA UCHUNGUZI YATAKUWA TENA TOFAUTI NA MAJIBU YA SPIKA NA LIJUALIKALI NA MUSUKUMA?
 
Yule mlinzi wake anayevaa makoti makubwa na miwani nyeusi muda wote alikuwa wapi?
 
Kwà ninavyoifahamu DODOMA, Mbowe hakupaswa kabisa kupelekwa huko DCMC na Sijui walitumia Protocal zipi kumpeleka kule Wakati General ipo na Hospitali ya kisasa kabisa Benjamin Mkapa ipo na ina vipimo vya kisasa kabisa na watoa huduma wenye weledi wakutosha kabisa!! Hili suala linafikirisha sana!??
Ok, kupelekwa huko kusinge sababisha chochote cha tofauti kufanyika nionavyo. Hivi tukio la Lissu halikutosha kuwafundisha????, . Police nao wamepiga marufuku tukio blisifanywe la kisiasa, what if likiwa la kisiasa????.... By the way spiker na baadh ya wabunge wa CCM wa CCM wamepokea report ya vipimo vya mgonjwa mpaka waseme walicho kisema?
 
Binafsi nadhani hakwenda hospital ya Serikali kwa sababu ya Usalama.

Pia walevi hudondoka ila huwa hawavunjiki kama yeye.

Pia angekuwa kalewa asingesema kapigwa
 
Naona kuna ‘narratives’ mbili zinazokinzana kuhusu kilichomtokea Mwenyekiti wa taifa, CHADEMA.

Wapo waliodokeza kwamba alienda kunywa na wenzake, dizaini akanywa akapitiliza, akalewa chakari

Upande wa makamanda, wao wanadai eti kapigwa na watu wasiojulikana

Sasa sijui protokali za kibunge na za hiyo hospitali aliyopelekwa zikoje

Ila, katika kuutafuta ukweli, mimi napendekeza apimwe blood alcohol level yake

Ni wakati muafaka sasa kuanza kutumia sayansi kukata mizizi ya fitna
Uzuri siku hizi PoliceTz wana forensic deparpatment nafikiri ni wazo zuri.
 
Naona kuna ‘narratives’ mbili zinazokinzana kuhusu kilichomtokea Mwenyekiti wa taifa, CHADEMA.

Wapo waliodokeza kwamba alienda kunywa na wenzake, dizaini akanywa akapitiliza, akalewa chakari

Upande wa makamanda, wao wanadai eti kapigwa na watu wasiojulikana

Sasa sijui protokali za kibunge na za hiyo hospitali aliyopelekwa zikoje

Ila, katika kuutafuta ukweli, mimi napendekeza apimwe blood alcohol level yake

Ni wakati muafaka sasa kuanza kutumia sayansi kukata mizizi ya fitna
Blood alcohol level inawezaje kuwa ni final na conclusive kwenye kukata mzizi wa fitina? inawezaje kusema kuwa pasi na shaka Mh Mbowe kavunjika mguu na kapata majeraha kwa kwa sabab ya blood acohol level yake?
 
Kwà ninavyoifahamu DODOMA, Mbowe hakupaswa kabisa kupelekwa huko DCMC na Sijui walitumia Protocal zipi kumpeleka kule Wakati General ipo na Hospitali ya kisasa kabisa Benjamin Mkapa ipo na ina vipimo vya kisasa kabisa na watoa huduma wenye weledi wakutosha kabisa!! Hili suala linafikirisha sana!??
Ni protocal za kawaida tu mkuu mgonjwa na wanaomhudumia mgonjwa wana uhuru wa kumpeleka mgonjwa wao wanapotaka, ni kama yule mwingine mwemye kibetri cha moyo alienda kupata kikombe wakati muhimbili ipo, alienda kuwekewa kibetri ng'ambo maana angebak kuwekewa Bongo angekuwa kuzimu saa nyiiingi, then alikimbia Dar, akaona haitoshi na akakimbia Dodoma akaenda kijijini kwake na akawa anafanyia kazi nyumbani kwake wakati ofisi yake ipo Dodoma/Dar.
 
La msingi ni kujua kama kweli aliumia mwenyewe au aliumizwa. Ikiwa ikionekana kuwa alijiumiza ndio sababu za kwa nini alisema uongo zinatafutwa. Hapo ndipo suala la impact ya ulevi linaingia. Je alisema uongo kuficha aibu ya kuwa alikuwa amelewa au ulevi ndio ulimfanya asahau. Ikithibitishwa kuwa aliumizwa na watu wengine, suala la ulevi linakuwa halina maana.

Amandla...
Upo sahihi kabisa! Hilo ni secondary, lakini kwasababu wanataka wamtreat kama mtuhumiwa badala ya victim, ndo maana wanataka kwenda hiyo route ya kulifanya primary kutaka kumpima kwanza ndo waje na kamovie.

Wajinga kabisa, ina maana hata George Floyd aliuwawa kwasababu ya ulevi. Pumbavu sana hawa viazi.
 
Ndio maana mnauwawa kama nyani huko USA akili zenu hazifikirii zaidi ya ngono
Dah! Mkuu tafadhali usifanye conclusion kwasababu yake. Pamoja na kwamba akili kama zake ni mojawapo ya sababu ya hilo tatizo ulilolitaja hapo juu.
 
Back
Top Bottom