Kalenga: Mbunge Rose Kamili wa CHADEMA ana hali mbaya (kiafya)

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mbunge Rose Kamili aliyetekwa na kundi haramu la Green Guard jana huko Kalenga taarifa zinasema hali yake siyo nzuri.

Mbunge huyo alikuwa katika kikao cha ndani na akina mama wa Chadema ghafla akavamiwa na kundi la Green Guard akapigwa vibaya na kudhalilishwa halafu akapelekwa mpaka Ofisi kuu ya CCM Mkoa.

Mbunge huyo aliendelea kuteswa kiharamia na kundi hilo huku viongozi wa CCM wakishuhudia.Walipoona hali yake inazidi kuwa mbaya waliwaita polisi na kusingizia alikamatwa akigawa Rushwa.

Mbali na kipigo alichopata mbunge huyo aliibiwa vitu mbalimbali zikiwemo simu zake mbili za mkononi na fedha Taslimu ambazo idadi yake haijawekwa wazi.

Taarifa kutoka Kalenga zinasema mbunge huyo anaandaliwa usafiri wa kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya KCMC

Kundi la kihalifu la Greenguard limekuwa likifanya vitendo vingi vya kikatili kwa kisingizio cha siasa bila kuchukuliwa hatua yoyote kama kupiga wapinzani,kutesa, kuharibu mali na hata kuua.

Updates kutoka Radio One:........

Radio one Breaking News wamesema hali yake si nzuri na muda wowote anaweza kuletwa na helkopta KCMC ili kuokoa maisha yake
 
Ni kweli alikuwa akigawa rushwa hilo liko wazi alichokipata ni stahili yake tena wangempiga zaid ili akome..
 
Get well soon Mama yetu.
Ndiomana kila siku nasema kuwa ukiwa CCM ni sharti uukane kwanza utu wako ili uendane na sera za uharamia na ujangiri wa chama. Na hii ni aibu kwa chama kinachojinadi kuwa ni chama cha mapinduzi.
 
DU! alikokamatwa akitoa rushwa, Je hakuna viongozi wa kiserikali wa eneo hilo? Ni lini CCM walianza kupinga na rushwa? Na sijawahi mtoa rushwa anakamatwa na kupelekwa ofisi ya CCM. Nchi imechanganyikiwa kabisa. Watatueleza pia endapo ni halali kumpiga mtoa rushwa? CCM sasa ni TAKUKURU,Polisi, na Mahakama?
 
Siasa za Tanzania sasa zimegubikwa na uongo, uharamia, ujambazi, uchoyo, umimi na kila jambo baya.., imekuwa vigumu kujua ni nani wa kumuamini au ni nani asemaye ukweli au uongo..
 
CCM walishatangaza vita!!!

Hivi mnakumbuka alivyotendewa fatuma kimaro aliyekuwa dc wa igunga na akina tundu lissu kutetea kitendo cha vijana wa chadema kumtia vidole,kumpapasa na kumvua kufuri yule mama mtu mzima ?
 
Back
Top Bottom