Hamis Tabasamu, Mbunge wa Sengerema usichokoze hisia za watu

Mkingaleo

Member
May 13, 2021
68
74
Leo wakati Rais wa Tanzania akihitimisha ziara yake mkoani Mwanza, aliongea na kundi muhimu sana katika jamii yoyote ile (vijana)
Mh Rais aliwataka wabunge waliokuepo eneo hilo anhalau watoe salam. Mbunge wa Sengerema ndugu Tabasamu amewaambia vijana eti wasome waelewe ila serikalini hakuna ajira.

Wewe Tabasamu kwani hukusoma ukaelewa mbona uliomba ubunge?

Au hujajua kwamba hao unaowaeleza hayo ndio wamekuajiri. Au hutarudi tena kwao? Tabasamu umetonesha vidonda vya watu.
Muwe mnaandika kwanza halafu mkifika mbele za watu msome maana hamchelewi kutoa boko.

Tabasamu kwakua umesoma ukaelewa uchaguzi ujao kajikalie nyumbani kwako usiwasumbue vijana. Mbona Mh. Rais anatumia lugha ya upole, ustaarabu na inayoeleweka. Wewe kuonge atu dakika moja na robo umechafua hali ya hewa. Ama kweli mwenye shibe, hamjui mwenye njaa.

Hatahivyo, halmashauri ya Sengerema inakabiliwa na ufujaji wa fedha hivyo Mh Rais ameagiza ufanyike ukaguzi ili kubaini tatizo.

Kwa aina ya muwakilishi kama huyo hana jipya sana katika kuishauri halmashauri kupitia baraza la madiwani.
 
Nipo tayari kumuunga mkono yule mbunge ambaye atasimama na kusema mishahara na posho zao zipunguzwe asilimia 50% inayobaki ipelekwe kuwawezesha vijana wajiajiri otherwise nabaki kuwatizama na porojo zao.
Huyo hajazaliwa bado kwenye lile bunge
 
Ukweli mchungu sana huu, Ila mazingira ya sasa hali ya ajira serikalini ni tatzo kubwa hivyo ni bora tu vijana wajiendae mapema japo mazingira pia ya kujiari ni magumu sana kwa nchi hii, mambo mengi yanafanywa kwa propaganda kuliko uhalisia
 
Shida iko hapo.
Lakini wenye uthubutu na kutia nia wanatusua..hakuna chepesi chini ya jua
 
Tabasamu Kanena kweli hadi Rais kampigia makofi.
ni kweli usio pingika kuwa sio rahisi vijana wote wakaajiriwa na serikali, ajira serikalini hazitoshi....huo ndio ukweli, badala yake vinajana yunapaswa tujiajiri wenyewe ktk sekta mbalimbali ili tujikwamue kimaisha.
kama alivyo sema Rais kuwepo na mikopo ya riba nafuu n.k
 
Kuna vijana wamemaliza chuo wamepata connection ya kupeleka mbao dom...si unajua sasa hv serikali ilihamia dom!...naishia hapa...
 
Mbunge wa Sengerema ndugu Tabasamu amewaambia vijana eti wasome waelewe ila serikalini hakuna ajira.
Huyu ndiyo mbunge mkweli kuzidi hata rais aliyewpa vijana ahadi hewa eti mkeka wa ma-DC na ma-RAS ni fursa kwao.

Jamani!! Huyu rais anajua idai ya vijana wa Tanznzania? Hii siyo Zanzibar yenye vijana laki moja.
 
Anawaogopa...so anaona bora adanganye
 
Back
Top Bottom