Mbunge aliyefukuzwa CHADEMA aomba ulinzi wa Mahakama, adai ana siri nzito

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,352
8,034
Grace Tendega ambaye ni kati ya Wabunge 19 waliovuliwa Uanachama na chama hicho alitoa ombi hilo mbele ya Jaji Cyprian Mkeha ambaye alimjibu kuwa anatakiwa kujibu maswali kama anavyoulizwa na sio nje ya hapo.

Wabunge hao walifika Mahakamani kuhojiwa kuhusu ushahidi wa Malalamiko ya Viapo baada ya Mawakili wa CHADEMA wakiongozwa na Peter Kibatala kuiomba Mahakama itoe amri ya kuwaita Mahakamani kutetea kesi yao.

Tendega alikiri kupokea barua za wito kutoka kwa katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika kwa WhatsApp na alipoulizwa kuhusu kuthibitisha maelezo ya Kusaini Kiapo alikiri kuwa hakuwa na vielelezo hivyo.

==========================

Mmoja wa wabunge 19 wa viti maalumu waliofukuzwa uanachama katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega jana aliiomba mahakama imlinde wakati akitoa ushahidi wake katika kesi yao ya kupinga kufukuzwa uanachama.

Tendega na wenzake 18, akiwemo Halima Mdee ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), wamefungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama.

Hata hivyo, jopo la mawakili wa Chadema linaloongozwa na Peter Kibatala liliomba mahakama iamuru wabunge hao wanane akiwemo Mdee na Tendega wafike mahakamani kwa ajili ya kuwafanyia mahojiano kuhusiana na ushahidi wao (malalamiko waliyoyatoa kwenye viapo vyao).

Wengine walioitwa kuhojiwa ni Nusrat Hanje, Ester Matiko, Ester Bulaya, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga na Cecilia Pareso.

Wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa jana, Tendega ndiye alifungua pazia la kuhojiwa maswali ya dodoso kutoka kwa mawakili wa Chadema, lakini kabla ya kuanza kuhojiwa aliiomba mahakama imlinde kutokana na yale aliyotarajia kuyasema.

Tendega baada ya kumaliza kuapishwa na wakili Kibatala kuumuliza maswali matatu, ikiwa ni pamoja na mahali alikokuwa Julai 18, mwaka huu wakati aliposaini kiapo chake alichokiwasilisha mahakamani, mbunge huyo aliomba kuuliza maswali.

Hata hivyo, Jaji Mkeha alimjibu kuwa yeye hapaswi kuuliza swali, bali kujibu maswali kutoka kwa mawakili, ndipo Tendega akajieleza alichohitaji kukisema na kuweka wazi kuwa anaomba mahakama imlinde.

“Naomba tu kusema kweli, mimi kama nilivyoapa hapa. Nilikiwa Kiongozi mkubwa tu ndani ya Chadema. Nimeapa kusema ukweli hivyo naomba unilinde kuna mambo mengine ambayo nitayaongea hapa ambayo ni siri,” alidai Tendega.

Hata hivyo, Jaji Mkeha alimueleza kuwa anapaswa kujibu maswali kulingana na atakachoulizwa na si nje ya hayo atakayokuwa anaulizwa. Baada ya maelezo hayo, wakili Kibatala aliendelea kumhoji maswali mbalimbali kuhusiana na madai yake katika kiapo chake ambayo ndiyo msingi wa kesi hiyo.

Katika mahojiano hayo alieleza pamoja na mambo mengine kuwa alipewa barua ya wito kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, Novemba 25, 2020 kwa njia ya mtandao WhatsApp akiwa Dodoma akitakiwa kufika ofisi za makao ya Chadema Novemba 27, saa 2 kupewa maelekezo kuhusu tuhuma zao.

Alidai kuwa utaratibu huo ni kinyume cha taratibu za chama na kwamba baadaye Novemba 27, mchana ndipo alipokea barua nyingine ya Mnyika ya Novemba 26, 2020 ilimwelekeza mahali ambako kikao cha Kamati Kuu kilipanga kufanyika kushughulika tuhuma zao.

Hata hivyo, alipoulizwa kama alikuwa na vilelezo alivyoviwasilisha mahakamani kuthibitisha maelezo yake hayo kuwa Julai 18, alisaini kiapo chake na kupokea barua hiyo kwa njia ya WhatsApp alikiri kuwa hakuwa na vilelezo hivyo.

Pia alipooneshwa na Wakili Kibatala Katiba ya Chadema Toleo la mwaka 2019 kuhusu matumizi ya Tehama katika mawasiliano na shughuli nyingine za chama alikubali kuwa Katiba inaruhusu mawasiliano kwa njia hiyo.

MWANANCHI
 
Huyo Tendega ni mhuni tu kama wahuni wengine.
kama ana siri alikuwa wapi kupeleka mahakamani siku zote?

Nimemkumbuka jinsi alivyogombea ubunge wa Isimani kwenye uchaguzi mdogo.
Nchi imejaa wahuni na walamba asali.
Siri ndo hiyo ya barua wasap
 
Huyo mwanamke alivyoiomba mahakama "imlinde" alidhani mahakama/jaji atamzuia Kibatala kumuuliza baadhi ya maswali kwa kisingizio cha kuwa na siri za kilichokuwa chama chao.

Hawa matapeli wanavunja sheria kila siku kwa kuendelea kuwa bungeni, wameyadharau maazimio ya chama chao kwa kwenda bungeni kuapishwa, ajabu, wanatudanganya "wana siri" kama vile wanakipenda sana kilichokuwa chama chao, wizi mtupu.
 
Grace Tendega ambaye ni kati ya Wabunge 19 waliovuliwa Uanachama na chama hicho alitoa ombi hilo mbele ya Jaji Cyprian Mkeha ambaye alimjibu kuwa anatakiwa kujibu maswali kama anavyoulizwa na sio nje ya hapo.

Wabunge hao walifika Mahakamani kuhojiwa kuhusu ushahidi wa Malalamiko ya Viapo baada ya Mawakili wa CHADEMA wakiongozwa na Peter Kibatala kuiomba Mahakama itoe amri ya kuwaita Mahakamani kutetea kesi yao.

Tendega alikiri kupokea barua za wito kutoka kwa katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika kwa WhatsApp na alipoulizwa kuhusu kuthibitisha maelezo ya Kusaini Kiapo alikiri kuwa hakuwa na vielelezo hivyo.

==========================

Mmoja wa wabunge 19 wa viti maalumu waliofukuzwa uanachama katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega jana aliiomba mahakama imlinde wakati akitoa ushahidi wake katika kesi yao ya kupinga kufukuzwa uanachama.

Tendega na wenzake 18, akiwemo Halima Mdee ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), wamefungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama.

Hata hivyo, jopo la mawakili wa Chadema linaloongozwa na Peter Kibatala liliomba mahakama iamuru wabunge hao wanane akiwemo Mdee na Tendega wafike mahakamani kwa ajili ya kuwafanyia mahojiano kuhusiana na ushahidi wao (malalamiko waliyoyatoa kwenye viapo vyao).

Wengine walioitwa kuhojiwa ni Nusrat Hanje, Ester Matiko, Ester Bulaya, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga na Cecilia Pareso.

Wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa jana, Tendega ndiye alifungua pazia la kuhojiwa maswali ya dodoso kutoka kwa mawakili wa Chadema, lakini kabla ya kuanza kuhojiwa aliiomba mahakama imlinde kutokana na yale aliyotarajia kuyasema.

Tendega baada ya kumaliza kuapishwa na wakili Kibatala kuumuliza maswali matatu, ikiwa ni pamoja na mahali alikokuwa Julai 18, mwaka huu wakati aliposaini kiapo chake alichokiwasilisha mahakamani, mbunge huyo aliomba kuuliza maswali.

Hata hivyo, Jaji Mkeha alimjibu kuwa yeye hapaswi kuuliza swali, bali kujibu maswali kutoka kwa mawakili, ndipo Tendega akajieleza alichohitaji kukisema na kuweka wazi kuwa anaomba mahakama imlinde.

“Naomba tu kusema kweli, mimi kama nilivyoapa hapa. Nilikiwa Kiongozi mkubwa tu ndani ya Chadema. Nimeapa kusema ukweli hivyo naomba unilinde kuna mambo mengine ambayo nitayaongea hapa ambayo ni siri,” alidai Tendega.

Hata hivyo, Jaji Mkeha alimueleza kuwa anapaswa kujibu maswali kulingana na atakachoulizwa na si nje ya hayo atakayokuwa anaulizwa. Baada ya maelezo hayo, wakili Kibatala aliendelea kumhoji maswali mbalimbali kuhusiana na madai yake katika kiapo chake ambayo ndiyo msingi wa kesi hiyo.

Katika mahojiano hayo alieleza pamoja na mambo mengine kuwa alipewa barua ya wito kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, Novemba 25, 2020 kwa njia ya mtandao WhatsApp akiwa Dodoma akitakiwa kufika ofisi za makao ya Chadema Novemba 27, saa 2 kupewa maelekezo kuhusu tuhuma zao.

Alidai kuwa utaratibu huo ni kinyume cha taratibu za chama na kwamba baadaye Novemba 27, mchana ndipo alipokea barua nyingine ya Mnyika ya Novemba 26, 2020 ilimwelekeza mahali ambako kikao cha Kamati Kuu kilipanga kufanyika kushughulika tuhuma zao.

Hata hivyo, alipoulizwa kama alikuwa na vilelezo alivyoviwasilisha mahakamani kuthibitisha maelezo yake hayo kuwa Julai 18, alisaini kiapo chake na kupokea barua hiyo kwa njia ya WhatsApp alikiri kuwa hakuwa na vilelezo hivyo.

Pia alipooneshwa na Wakili Kibatala Katiba ya Chadema Toleo la mwaka 2019 kuhusu matumizi ya Tehama katika mawasiliano na shughuli nyingine za chama alikubali kuwa Katiba inaruhusu mawasiliano kwa njia hiyo.

MWANANCHI
Hii kesi bwana. 😅😅
 
Back
Top Bottom