Lamsingi kuelewa hapa ni kuwa kuna vitu viwili;
1.KUNUKA:Ni kuwa harufu yake Inakera, Haivutii, Haimpi mahanjamu mwenzi wako.
2.KUNUKIA: Maana yake-Harufu ya mwenzako inavutia, Haikeri, Inahamasisha.
Mwanamke kiasili anayo harufu yake anayonukia ambayo ni muhimu (Harufu ya kike inaitwa) na inamhamasisha mwanamme.
Vivyo hivyo kwa mwanamme nae ipo harufu ambayo mwanamke wake anaisikia.
Sizungumzii vikwapa lakini au kunuka kufuli lako-Huo ni Uchafu.
Wawili mliopo kwenye mahusiano kama hampo makini kwenye kujiswafi inakuwa ni sheedar kwa mwingine ila wengi huwa tunavumiliana na kujaribu kusaidiana kwa kurekebishana.
ANGALIZO:
Ni uongo uliotukuka mtu kusema eti katika mishe za kimahusiano eti hujawahi kukumbana na mwenye harufu isiyokuwa rafiki na kama imekutokea hiyo ni bahati yako kwelikweli.