Kalamu Yenye Siri ya Damu

Chilojnr

Senior Member
Jul 5, 2012
141
500
Mwandishi: Nyemo Chilongani.
0718069269.

Sehemu ya 01

“I need to see his picture,” (Ninahitaji kuiona picha yake) alisikika mwanaume mmoja kwa hasira, aliongea kwa sauti ya juu kiasi kwamba kila mmoja ofisini alishtuka, hakuamini kama ingetokea siku moja bosi wao angeongea kwa hasira kama alivyofanya siku hiyo.
Ilikuwa ni ndani ya makao makuu ya Shirika la Kijasusi la Kimarekani, CIA (Central Intelligence Agency) yaliyokuwa huko Langley, jijini Virginia nchini Marekani.

Mkononi mwake alikuwa na kifaa kidogo kiitwacho kindle ambacho hutumika kusomea vitabu mbalimbali, na wakati huo alikifungua kitabu kiitwacho There Is No God At All kilichomaanisha Hakuna Mungu Kabisa kilichoandikwa na mwandishi aliyejulikana kwa jina la Williams McCannon.

Mitaani kitabu hicho kilikuwa gumzo, kila mtu alikuwa akikizungumza, kwa watu ambao hawakuwa wamekisoma, haraka sana wakaingia kwenye tovuti ya Amazon na kuanza kukitafuta na kukinunua kwa dola 20 ambazo zilikuwa ni zaidi ya shilingi elfu arobaini na tano kwa pesa za Kitanzania.

Kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter na sehemu nyingine ni jina lake tu ndilo lililokuwa likitawala. Kwenye televisheni, alikuwa akizungumziwa yeye na kitabu chake kilichokuwa na nguvu kubwa ya ushawishi.

Kila mtu aliyekisoma kitabu hicho cha simulizi alimwambia mwenzake. Kilikuwa kitabu kizuri, kilichokuwa na mvuto hata kwa kukiangalia kwa nje na ndani, kwa jinsi matukio yake yalivyokuwa yamepangwa, yalivyoelezewa kwa undani hapakuwa na mtu aliyeamini kama kungekuwa na mwandishi aliyekuwa na uwezo wa kuandika kitabu kizuri kama hicho kwani waliamini waliokuwa wakiandika vitabu vya namna hiyo walikufa miaka mingi iliyopita akiwemo William Shakespeares.

Kwa siku mbili tu, tayari kulikuwa na watu milioni moja ambao walikinunua kitabu hicho kwenye tovuti hiyo kitu kilichowashangaza hata wamiliki wa tovuti hiyo, walihisi kitabu hicho kilikuwa na kitu kikubwa sana hivyo hata nao kukichukua na kuanza kukisoma.
Mwandishi hakuwa akijulikana ila hakuwa mgeni katika tovuti hiyo. Watu walimtafuta humo, walihitaji kumjua, walitaka kujua huyo mwandishi aliyeandika vitu hivyo alifananaje, alikuwa na muonekano gani lakini kwa bahati mbaya, hakukuwa na picha yake yoyote ile kitu kilichomhuzunisha kila mmoja.

Kitabu hicho kilimzungumzia kijana mdogo, mwenye umri wa miaka ishirini na mbili ambaye alipotezana na mpenzi wake, alimpenda tangu walipokuwa wadogo kabisa, walipanga kuoana na kuwa pamoja lakini baada ya msichana huyo kusafiri na kwenda Marekani kusoma, kila kitu kikabadilika.

Msichana huyo wa kwenye simulizi aliyeitwa kwa jina la Esta hakuonekana tena, ilisemekana kwamba alifariki dunia katika shambulio la majengo pacha ya WTC (World Trade Center) ambayo yalishambuliwa mwezi Septemba mwaka 2001 huko New York nchini Marekani.
Kijana huyo ambaye aliachwa nchini Nigeria, akaamua kuondoka kwa njia za panya kuelekea nchini Marekani. Huko njiani alipitia vikwazo vingi mpaka kuingia, alipopata uhakika kwamba mpenzi wake aliuawa kwenye majengo hayo ndipo akaanza kufanya uchunguzi wa juu kuhusu shambulio hilo.

Kwa jinsi Williams alivyouelezea uchunguzi uliofanywa na mhusika huyo kwenye kitabu hicho ndicho ambacho maofisa wa CIA walipoamua kumtafuta mwandishi huyo.

Walijua kabisa kulikuwa na mengi aliyokuwa akiyafahamu, kusingekuwa na urahisi wa kuyazungumzia matukio hayo kwa kina zaidi na wakati alikuwa mwandishi tu na inawezekana hakuwahi kuishi nchini Marekani au hata kwenye nchi za Kiarabu.

Mkurugenzi wa shirika hilo, Bwana Peter O’Brain alichanganyikiwa, aliwapanga vijana wake, aliwaambia wafanye kila liwezekanalo kuhakikisha mwandishi wa kitabu hicho anapatikana haraka sana kwa kuwa walihitaji kufahamu mambo mengi zaidi kuhusu yeye, kwa nini aliamua kuandika simulizi hiyo ambapo kulikuwa na vyanzo mbalimbali, vile ambavyo wao kama wapelelezi hawakuwa wakivifahamu kabisa.

Walipata mawasiliano yake, namba zake zilionyesha alikuwa akiishi nchini Nigeria. Walichokifanya ni kuwatuma wapelelezi huko kwa lengo la kumtafuta mwandishi huyo kimyakimya.

Walifika huko na kuanza msako wao kwa kutumia namba zilezile. Waliuliza sana, kila kona lakini hawakufanikiwa kumpata na kitu kilichowashangaza zaidi, hata Wanigeria wenyewe walisema hakukuwa na Mnigeria aliyekuwa na uwezo wa kuandika hadithi ya namna ile, inawezekana alikuwa ni Mmarekani ambaye hakutaka kugundulika.

“Mnigeria aandike hadithi ya namna ile, yenye vyanzo vya siri kiasi kile! Hakuna Mnigeria huyo,” alisema jamaa mmoja, alipinga kabisa, kwa jinsi kitabu kile kilivyokuwa kimeelezewa, ilikuwa ni vigumu kuamini kama kungekuwa na Mwafrika yeyote ambaye angekuwa na uwezo wa kuandika namna ile.

Namba zile hazikupatikana. Hilo halikuwa shida, maofisa hao wa CIA wakaondoka na kuelekea katika kampuni ya simu za mkononi ya MTN na kuulizia kuhusu namba hizo.

Haraka sana meneja wa kampuni hiyo akawachukua na kuwapeleka kwa vijana wa IT na kuwaambia kuhusu namba hizo, haraka sana vijana hao wakaanza kuangalia kwenye system zao kuangalia usajili wa namba hizo lakini kitu cha ajabu kabisa system ilionyesha namba hizo hazikuwa zimeanza kutumika.

“Unasemaje?”

“Hizo namba hazijaanza kutumika. Mna uhakika kwenye kitabu zimeandikwa namba hizo?” aliuliza kijana mmoja na hivyo ofisa mmoja kumuonyeshea kupitia simu yake.

“Hii ndiyo maana ya mwandishi. Huyu jamaa ni genius,” alisema jamaa mmoja miongoni mwa wale IT.

Maofisa wale wakaondoka, walichanganyikiwa, hawakuwa na mategemeo yoyote yale ya kumpata mwandishi huyo. Hawakujua alikuwa mahali gani lakini zaidi, kubwa kuliko yote ni kwamba hawakujua alifananaje kwa kuwa kwenye kitabu hicho cha mtandaoni hakukuwa na picha yake yoyote ile.

Haraka sana wakapiga simu nchini Marekani na kuwaambia kile kilichotokea, kwamba hawakufanikiwa kabisa kumpata mtu huyo na hata zile namba ambazo ziliwekwa kwenye kitabu kile hazikuwa zimeanza kutumika, ilimaanisha kuwa mwandishi huyo alijua dhahiri alikuwa akienda kutafutwa baada ya kukitoa kitabu kile na ndiyo maana aliamua kutokuandika namba zake halisi.

“Ila kuna barua pepe, kwa nini tusiidukue na kuangalia humo?” aliuliza ofisa mmoja.

Kwa jinsi walivyokuwa wamchanganyikiwa hakukuwa na mtu aliyelifikiria hilo. Haraka sana wakaingia kwenye barua pepe yake kwa njia ya udukuzi na kuanza kuangalia kile kilichokuwa kikiendelea.

Waliona jinsi jamaa huyo alivyokuwa amejisajili kwenye tovuti ya Amazon, alivyowasiliana nao na hatimaye kukiweka kitabu chake hicho.

Hakikuwa cha kwanza, waligundua kulikuwa na kitabu kingine ambacho alikiweka huko, hicho kiliitwa ‘The Blood City’ yaani kikiwa na maana ‘Jiji la Damu’.

Haraka sana wakakinunua na kuanza kuangalia tena namba zake. Zilikuwa humo, walijaribu kuzifananisha na zile ambazo ziliandikwa kwenye kile kitabu kipya.

Hazikuwa na utofauti, zilikuwa zilezile, kilichowaumiza kichwa ni kwa sababu gani mwandishi huyo aliamua kuandika vitabu hivyo na kuweka namba ambazo hazikuwa zikitumika?

“NI lazima tuwasiliane na Amazon kwanza! Kuna kitu nimewaza,” alisema jamaa mmoja, huyo aliitwa Sincliar, alikuwa na kipara, mmoja wa watu waliokuwa katika kitengo cha wale waliokuwa wakifikiria sana katika shirika hilo.

“Kitu gani?”

“Kitabu chake kinauzwa kwenye tovuti, si ndiyo?”

“Ndiyo!”

“Pesa si zitakuwa zinakwenda kwenye akaunti yake benki? Basi ni lazima tuijue hiyo akaunti kwanza,” alisema Sinclair.

Alichokisema kilikuwa sahihi kabisa, hakukuwa na muda wa kupoteza, haraka sana wakaondoka na kuelekea makao makuu ya Amazon yaliyokuwa huko Seattle, Washington.

Walipofika huko, wakaomba kuonana na meneja ambaye baada ya kusikia alikuwa akiitwa na maofisa wa CIA, haraka sana akawaita ofisini kwake na kuanza kuzungumza nao.

Alijua walichokuwa wakihitaji kuongea naye! Alisikia mambo mengi kuhusu kitabu kile, kilinunulika sana na katika siku ya nne tayari kulikuwa na watu milioni sita walipakua kitabu kile huku wengine wakiendelea kumiminika kila siku.

Walimwambia kuhusu jambo lao, walihitaji kumfahamu mwandishi ambaye aliandika kitabu kile kwani kwa jinsi ilivyoonekana, mtu huyo alikuwa akifahamu mambo mengi mno yaliyokuwa yametokea na hata yale ambayo yangeweza kutokea, ilikuwa ni lazima wayasimamishe hayo na njia nzuri ya kufanikiwa katika hilo ni kumtafuta mwandishi huyo.

“Hakutuma picha yake,” alisema meneja.

“Tunajua!”

“Ila si kuna namba zake za simu!”

“Hazipo duniani!”

“Unamaanisha nini?”

“Hazijawahi kutolewa!”

“Mh! Sasa mmekuja hapa kutafuta nini?”

“Kuangalia akaunti yake ya benki! Pesa zinaingizwa kwenye akaunti ipi,” alisema ofisa mmoja.

Kisheria hawakuruhusiwa kuziweka wazi namba za mteja wao ila kwa sababu watu waliofika mahali hapo walikuwa ni wa usalama wa taifa, hakuwa na jinsi, akatafuta na kuwapa watu hao.

Wakaichukua na kuondoka nazo. Walipofika makao makuu wakaanza kutafuta ni akaunti ya benki gani iliyokuwa ikitumika. Kwenye kufuatilia, ilionekana ni Benki ya Barclays kwenye tawi lake moja nchini Nigeria ndipo ambapo mwanaume huyo alifungulia akaunti yake hiyo na wakati huo kulikuwa na kiasi cha pesa cha dola milioni nne, zaidi ya shilingi bilioni nane zilizokuwa zimeingizwa humo kutokana na mauzo ya kitabu.

“Wasilianeni na hawa Barclays wa Nigeria!” alisema O’Brain.

Haraka sana maofisa waliokuwa nchini Nigeria wakaondoka na kuelekea kwenye tawi la benki hiyo na walipofika, kitu cha kwanza kilikuwa ni kujitambulisha na kutaka kuonana na meneja wa benki hiyo.

Hakukuwa na tatizo lolote lile, wakaonana naye na kumwambia kile walichokuwa wakikihitaji. Hapakuwa na tatizo, mwanaume huyo akawachukua na kuwapeleka katika ofisi ya mhusika wa kile walichokuwa wakihitaji na kuwaonyeshea.

“Mtu mwenye akaunti ni huyu hapa,” alisema mfanyakazi huyo.

“Anaitwa nani?”

“Juma Hiza!”

“Juma Hiza? Mbona kwenye kitabu anajulikana kwa jina la Williams McCannon?” aliuliza ofisa mmoja huku akimwangalia meneja wa benki.

“Hata sisi hatujui! Nadhani ni kwa sababu ya kulenga soko la wasomaji!” alijibu.

“Mmh!”

Hawakutaka kupoteza muda, haraka sana wakaondoka mahali hapo na kurudi hotelini. Wakawasiliana na wenzao na kuwaambia kuhusu jambo hilo.

Walisema wazi kwamba walishangazwa, jina la mwandishi ambalo liliwekwa kwenye kitabu lilikuwa tofauti na lile lililokuwa likionekana kwenye akaunti yake ya benki.

“Mnamaanisha nini?”

“Anaitwa Juma Hiza!”

“Na picha yake?”

“Tunaituma!” alisema.

Haraka sana picha ya mwandishi huyo ikatumwa mpaka nchini Marekani ndani ya makao makuu ya CIA.

Picha ile ikapokewa na kuwekwa kwenye screen kubwa na kila mtu kuanza kuiangalia. Hakukuwa na mtu aliyeamini kama kijana yule mdogo, aliyeonekana kuwa na umri usiozidi miaka ishirini ndiye ambaye alikuwa ameandika kitabu kile.

Kwa kumwangalia tu, alionekana kutokuwa na uwezo mkubwa wa kuandika namna ile, ilikuwaje sasa atoe kitabu kilichouzwa kwa kasi na kumuingizia kiasi kikubwa cha pesa?

“Mna uhakika huyu ndiye aliyeandika kitabu hiki?” aliuliza O’Brain.

“Huo ni kwa mujibu wa picha kwenye akaunti yake ya benki!” alijibu jamaa mmoja.

“Ila mbona mdogo?”

“Kwa mtazamo, ila kiakili ni mkubwa mno!”

“Hii picha sambazeni kila kona, ninataka ndani ya saa kadhaa tujue yupo wapi, tunamtaka kijana huyu, hebu achaneni na kila kitu, tushughulikieni suala la huyu mtu kwanza,” alisema O’Brain huku akionekana kuchanganyikiwa, inawezekana kabisa kumpata Hiza ingekuwa moja ya mafanikio yake kujua ni kitu gani hasa alikijua kuhusu shambulio hilo ambalo liitemesha Marekani na nchi nyingine.

Je, nini kitaendelea?
IMG-20201016-WA0012.jpg
 

share

JF-Expert Member
Nov 22, 2008
5,679
2,000
Sawa. Tutasoma baada ya Uchaguzi Mkuu tarehe 28 Oktoba 2020 tutakapolipwa nyongeza za mishahara na Serikali mpya ya Uhuru, haki, na Maendeleo ya Watu. Sasa hivi tumechoka bro. Hatuna nguvu kusimama wala kukaa. Jiwe katufilimba kweli kwa miaka 5. Tukisoma Uzi mrefu hivi hatuelewi braza. Akili inawaza matembele na dagaa.
 

Chilojnr

Senior Member
Jul 5, 2012
141
500
Riwaya: Kalamu Yenye Siri ya Damu

NYEMO CHILONGANI.
0718069269

Sehemu ya 02.

“Mmefikia wapi?” lilikuwa swali moja lililoulizwa na mwanaume mwenye ndevu nyingi, alivalia kanzu, alikalia kiti cha kamba, kichwani alivalia kilemba na ndevu zake hizo zilipakwa hina.

“Tunamfuatilia huyu mwandishi!”

“Ninawapeni siku tatu awe amepatikana, haiwezekani ajue baadhi ya mambo ambayo tuliamini ni siri kubwa, na tunahisi anajua mengi kuhusu udhaifu wa Marekani, hakikisheni mwandishi huyo anapatikana haraka iwezekanavyo,” alisema mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Omar Bin Sharifu, mmoja wa magaidi wa kimataifa wa Kundi la Al Qaida, gaidi aliyekuwa akitafutwa kwa udi na uvumba duniani kote.

Mwili wake tu ulikuwa na thamani ya dola milioni themanini endapo tu angepatikana akiwa amekufa na dola milioni mia mbili kama tu angepatikana akiwa hai.

Marekani kupitia Shirika la Kijasusi la CIA walijaribu kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha mwanaume huyo anapatikana lakini walishindwa kumpata. Waliwatumia baadhi ya Waarabu ambao walikuwa vibaraka vyao lakini pia kulikuwa na ugumu kumpata mwanaume huyo.

Kila siku waliumiza vichwa vyao, huyo Omar hakutakiwa kuwa hai, kama kila mtu alitamani kuiona dunia kuwa sehemu salama basi mtu wa kwanza ambaye alitakiwa kuuawa alikuwa mwanaume huyo.

Alikuwa na akili kubwa, alijua kuwasumbua Wamarekani na nchi nyingine za Ulaya. Kila walipokuwa wakijipanga kwa ajili ya kumkamata, hawakuwa wakifanikiwa.

Kuna wakati waliambiwa mwanaume huyo alikuwa ndani ya mgahawa fulani huko Saudi Arabia, walipokuwa wakienda, walimuona lakini la ajabu alipokuwa akinyanyuka na kuelekea chooni, walipofika huko, mwanaume huyo hakuonekana.

Kulikuwa na tetesi nyingi juu yake kuonekana mahali fulani lakini kila walipokuwa wakienda kumkamata, waliambiwa aliondoka, yaani dakika moja iliyopita, waliambiwa mpaka gari alilokuwa amelipanda na walipokuwa wakilifuatilia, hakuwa akionekana.

Watu walikufa kwa mabomu ya kujitoa mhanga, hilo liliwachanganya Wamarekani, vichwa viliuma, walizidi kutuma watu na cha ajabu kabisa kila kibaraka wao alipokuwa akigundulika, alichinjwa hadharani kama kuku.

Mbali na wao kumtaka huyo Juma Hiza, pia Omar alimtaka mwandishi huyo, ilikuwa ni lazima ampate, alihisi alikuwa akifahamu mambo mengi kwani kupitia stori yake aliyoandika, alijua kulikuwa na mengine ambayo hakuwa ameyafafanua, kama yangefafanuliwa aliamini Marekani lisingekuwa taifa tishio tena, ilikuwa ni lazima kulimaliza taifa hilo.

Naye akaingia katika vita ya kumtafuta mwandishi huyo ambaye mpaka kipindi hicho hapakuwa na mtu aliyejua mahali alipokuwa.

***
Kitabu cha There is no God At All kilieleza mambo mengi, ni kama kulikuwa na siri kubwa ambazo humo ziliwekwa wazi na kujulikana na kila mtu.

Kundi la Al Qaida halikuwa na amani, walikuwa na mipango mingi ya kufanya, waliweka mikakati ya kuzishambulia nchi za Magharibi kama moja ya njia ya kuwaonya kuingia katika nchi zao lakini kitu cha ajabu kabisa, mipango yote ambayo walikuwa nayo ilikuwa ndani ya kitabu kile.

Walichanganyikiwa, walijua dhahiri mwandishi wa kitabu hicho alifahamu mambo mengi, walihitaji kumtafuta na kumpata na ndiyo maana kiongozi wao, Omar akawatuma waondoke na kwenda kumfuatilia.

Ilikuwa vigumu kwenda wao kama wao bali walichokifanya ni kumtumia bilionea mmoja wa Kiarabu aliyeitwa kwa jina la Shakoor Issa ambaye yeye alikuwa na watu wengi waliokuwa na uwezo wa kufanya kitu chochote kile.

Alipoambiwa kuhusu mwandishi wa kitabu hicho aliyejulikana kwa jina la Williams McCannon na mambo aliyokuwa ameyaandika alishangaa sana kwani hakuwa na uhakika kama kungekuwa na mtu ambaye angejua mambo mengi kuhusu magaidi na maofisa wa CIA kama alivyofanya.

Hakutaka kuchelewa, alipata fununu mtu huyo alikuwa barani Afrika hivyo akawatuma watu kuelekea huko. Kitu cha kwanza alichokiangalia ni jina, mara nyingi majina kama hayo yalikuwa yakipatikana nchini Liberia.

Nchi hiyo ndiyo ilikuwa na majina mengi ya Kizungu kwa sababu kwenye historia ya Afrika ilisema baada ya watumwa kupelekwa nchini Marekani na Uingereza kwa ajili ya kufanyishwa kazi, walipoonekana kuwa goigoi, walirudishwa barani Afrika na kutupwa ndani ya nchi hiyo.

Hiyo ndiyo ambayo ilipelekea nchi hiyo kuwa na majina mengi ya Kizungu kama hayo lakini ndiyo sababu hata bendera ya nchi hiyo kufanana na Marekani kwa kuwa wao kila siku wanahisi ni Wamarekani weusi waliokwenda kutupwa nchini Liberia na hata lafudhi ya Kiingereza chao nchi nzima wanaongea kama Wamarekani weusi.

Hiyo ndiyo ilikuwa sababu iliyomfanya Shakoor kuwatuma vijana wake kuelekea huko. Hawakuchukua siku nyingi, wakafika na kuanza kufuatilia huko.

Walijifanya kama watalii kutoka Dubai ambao walikwenda huko kwa ajili ya kuangalia makumbusho ya nchi hiyo kipindi kile kilichokuwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Walifanya uchunguzi wao kwa chini sana huku wakiwafuatilia watu wa nchi hiyo kuhusu ufuatiliaji wa kitabu kile. Kwa kipindi hicho, dunia nzima gumzo lilikuwa kitabu hicho tu, kilikuwa ni kitabu hatari sana, kitabu kilicholeta ukombozi kwa baadhi ya watu lakini pia kilikuwa kwenye hatua za kuwazika watu wengine.

Kilikuwa moja ya vitabu sumu sana kiasi kwamba maofisa wa CIA walishinikiza kitolewe katika Tovuti ya Amazon lakini wenyewe walikataa kwa sababu ndicho ambacho kilikuwa kikiwaingizia pesa sana kipindi hicho.

Waarabu hao waliotumwa walikuwa na kazi kubwa mno, hawakuona kama wangeweza kufanikiwa kwa sababu tu hawakuwa na picha ya mwandishi huyo, yaani walikuwa wakienda sehemu kumtafuta mtu ambaye hata hawakuwahi kukutana naye kwenye maisha yao.
Walipoanza kuulizia jina la Williams McCannon, walijitokeza watu wengi waliokuwa na jina hilo kiasi kwamba iliwachanganya na kuona kabisa kulikuwa na ugumu mkubwa.

Hawakutaka kuficha, wakampigia simu Shakoor na kumwambia kilichokuwa kikiendelea, wasingeweza kufanya kazi hiyo kwa sababu kulikuwa na ugumu mkubwa mno mbele yake, yaani kulikuwa na watu wengi waliokuwa na jina hilo, hivyo isingewezekana hata kidogo kumpata mwanaume huyo.

Shakoor akachoka. Moyoni mwake alijiona kuwa na mzigo mzito, alikuwa akifanya mambo mengi kwa lengo la kumfurahisha Omar kwa kuwa mwanaume huyo alikuwa mtu hatari sana, hivyo ilikuwa ni lazima afanye kila liwezekanalo kuhakikisha anampata mwandishi huyo.

Haraka sana akawasiliana na watu wake wa karibu waliokuwa nchini Marekani, tena wale waliokuwa kwenye vitengo vya siri kabisa na kuanza kuzungumza nao.

Aliwauliza kuhusu mwandishi wa kitabu kile, Williams McCannon, walimwambia ukweli mtu huyo hakuwa akiitwa jina hilo, kwa taarifa za chini ambazo nao walizinyaka ni kwamba mwandishi halisi aliitwa Juma Hiza na inasemekana alikuwa akiishi nchini Nigeria.

“Walimjuaje?” aliuliza Shakoor.
“Hawa CIA ni shida sana. Wewe jua hilo, cha msingi kama unamtafuta mwandishi huyo, tafuteni kwa jina hilo,” alisikika jamaa kutoka nchini Marekani.
“Na hana picha kweli au uongo?”
“Picha yake imepatikana!”
“Ipo wapi?”
“Ngoja nifanye mchakato niipate, nitakutumia ndani ya saa moja,” alisema mwanaume huyo na kukata simu.

Kidogo hilo likamfurahisha Shakoor, moyoni mwake akajisikia amani na furaha kurudi tena kwani alikuwa na uhakika endapo angeipata picha ya mwandishi huyo basi ingekuwa kazi nyepesi sana kwao kufanikisha kile alichokuwa akikihitaji.

Alisubiri kwa nusu saa ndipo akatumiwa picha ya mwandishi huyo. Alipoiona, akashtuka, hakuamini kijana mdogo kama huyo angeweza kuandika kitabu kilichokuwa na mambo makubwa kama hayo.

Aliiangalia picha ile, akakisoma kidogo kitabu kile, kwake vilikuwa vitu viwili tofauti kabisa ambavyo havikumuingia akilini.
“Una uhakika ni huyu?” aliuliza Shakoor, alihisi kama alikuwa akidanganywa vile.

“Ndiyo! Hiyo picha hata CIA wanayo na ndiyo wanamtafuta muda huu. Kama kweli unamtaka, mtafuteni huyo huko Nigeria,” alisema mwanaume huyo na kukata simu.

Kitendo cha kupata picha ie yalikuwa ni mafanikio makubwa mno, hakutaka kusubiri, ili aonekane alikuwa ameifanya kazi yake, picha ile akamtumia Omar ambaye naye baada ya kuipokea na kuiangalia, alishangaa kama ambavyo watu wengine walishangaa.

“Hii picha ya nani? Unasema ndiyo ya yule mwandishi?” aliuliza Omar, tena akasimama kutoka kwenye kiti chake na kuipandisha kanzu yake juu.
“Ndiye yeye!”
“Hapana! Haiwezekani!”
“Mimi nimetumiwa picha hiyo! Hebu kwanza tumtafuteni huyo mtu halafu ndiyo mambo mengine yaendelee,” alisema Shakoor kitu ambacho Omar alikubaliana nacho. Hivyo vijana wengine wakatumwa kuelekea nchini Nigeria.

Je, nini kitaendelea?

Tukutane Jumanne hapahapa.
 

Chilojnr

Senior Member
Jul 5, 2012
141
500
NYEMO CHILONGANI
KALAMU YENYE SIRI YA DAMU
0718069269
SEHEMU YA 03

Bwana Peter O’Brain alikuwa ofisini mwake, alichanganyikiwa, kile kilichokuwa kikiendelea kilimuumiza kichwa kupita kawaida. Aliliandika jina la Juma Hiza kwenye karatasi ndogo na kuiweka juu ya meza yake.
Muda wote alikuwa akiliangalia jina hilo, alikuwa kwenye hali ya utulivu kuliko kawaida, aliamini endapo angetulia na kuliangalia jina hilo mara kwa mara angepata ufafanuzi juu ya kitu ambacho alitakiwa kufanya.
Humo ofisini, hasa kwa kipindi kama hicho hakuhitaji usumbufu wowote ule, aliamua kutulia kwa sababu aliamini kazi ambayo ilikuwa mbele yake ilikuwa kubwa kupita kawaida.
Baada ya dakika kadhaa, akahisi kupata jibu juu ya kitu aliachotakiwa kufanya. Jina la Juma lilionekana kuwa maarufu barani Afrika na katika baadhi ya nchi za Kiarabu ambao huliandika Jumaar.
Alihitaji kujua undani wa jina lililobaki la Hiza. Haraka sana kama mtu aliyekuwa amekurupuka, akakaa vizuri, akaiwasha kompyuta yake na kufungua Google kisha kuliandika jina hilo.
Walikuja watu wengi waliokuwa na jina hilo na alipowafuatilia watu hao, wote walikuwa na uraia wa Tanzania. Alishtuka kidogo, aliona jina hilo likiwa sana nchini Tanzania na hakukuwa hata na Mnigeria mmoja ambaye alikuwa na jina hilo.
Hapo akahisi kitu, aliamini kabisa huyo mwandishi alikuwa mtu mwenye akili nyingi, hivyo kubadilisha muonekano wa uraia wake lilionekana kuwa jambo jepesi mno, hivyo kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuwatuma watu huko Tanzania.
Wakati alipotaka kuchukua simu yake ya mezani kwa lengo la kuwapigia watu wake na kuwaambia kumfuatilia kijana huyo nchini Tanzania, wazo moja likamjia kichwani mwake.
Akaanza kujiuliza kama kweli mwandishi huyo alijulikana kwa jina la Juma Hiza, je, lisingekuwa jambo jepesi kuwa na akaunti yake katika Mtandao wa Kijamii wa Facebook? Jibu ambalo lilipatikana ni kwamba lingekuwa suala jepesi sana hivyo kuingia kwenye mtandao huo na kuanza kutafuta jina la Juma Hiza.
Walikuja wengi, kama kumi hivi, akaanza kuwapitia mmoja baada ya mwingine na baadaye kabisa akampata mtu ambaye alihisi ndiye mwenyewe. Akamfungua, kitu alichokutana nacho ni hadithi mbalimbali ambazo ziliandikwa na mwandishi huyo.
“I got you,” (Nimekupata) alisema O’Brain huku akitoa tabasamu.
Akachukua kalamu na karatasi na kuanza kuandika pembeni maelezo yote ambayo alikuwa akiyahitaji, hakuishia hapo, akaelekea kwenye posti zake na kuanza kuangalia comments, alihitaji kujua baadhi ya vitu, alijua kulikuwa na ugumu wa kumpata mwandishi huyo ila kama kulikuwa na mtu ambaye alicomment sana huku akionekana kuwa karibu na mwandishi huyo, basi ilikuwa ni lazima waanze kudili naye ili kumpata mhusika.
“Latifa Ntanga,” alijisemea mara baada ya kuona kwenye kila simulizi za Juma Hiza msichana huyo alikuwa akicomment sana, hivyo akahisi kabisa wawili hao walikuwa wakifahamiana.
Haraka sana akachukua maelezo ya msichana huyo, alikuwa akiishi jijini Tanga, aliolewa na kingine zaidi ambacho kilikuonekana kuwa cha maana kabisa ni picha ambazo alikuwa ameziweka kwenye akaunti yake.
Baada ya kuchukua maelezo yote hayo, akawapigia simu vijana wake na kuwaambia waondoke nchini Nigeria, mtu ambaye walikuwa wakimtafuta hakuwa huko bali alikuwa nchini Tanzania.
“Tanzania?” aliuliza jamaa mmoja, alionekana kushtuka mno.
“Ndiyo! Nendeni huko, nawatumia maelekezo. Kuna msichana anajiita Latifa Ntanga kwenye akaunti moja huko Facebook, mtafuteni huyo, atakuwa na maelezo kuhusu mwanaume huyo. Ingieni huko mkamuone na kuchukua mnachotaka. Mkimpata, muulizeni maswali yote mpaka awaambie huyu Juma yupo wapi,” alisema O’Brain na kukata simu.
Vijana ambao walikuwa nchini Nigeria hawakutaka kupoteza muda, haraka sana wakaondoka na kuelekea nchini Tanzania ambapo baada ya kufika jijini Dar es Salaam wakapanda ndege na kuelekea jijini Tanga.
Walijifanya kuwa watalii ambao walikwenda huko kuangalia mapango ya Amboni kumbe walikuwa na jambo jingine kabisa walilotaka kulifanya. Hawakuchukua muda mrefu wakaingia Tanga huku ikiwa ni usiku mnene.
Wakachukua chumba hotelini na kukaa huko. Usiku mzima siku hiyo walikuwa wakimfuatilia huyo mtu aliyejiita Latifa Ntanga, waliidukua akaunti yake na kuingia kwenye inbox yake na kuangalia mawasiliano yake na Juma Hiza, hapo wakagundua hata msichana huyo alikuwa mwandishi wa simulizi.
“She knows everything we need to know,” (Anajua kila kitu tunachohitaji kujua) alisema jamaa mmoja aliyeitwa kwa jina la Chris.
Kwenye hizo chatting zao za inbox, Latifa alimtumia namba Juma Hiza kwa ajili ya kuwasiliana kama waandishi na kusaidiana katika vitu vidogo. Hiyohiyo namba ndiyo ambayo waliichukua kwa lengo la kutaka kumpigia simu siku inayofuata na kujua mahali alipokuwa.
“Hatutotakiwa kumpigia simu, tutatakiwa kumfuatilia na kujua mahali alipo kupitia simu yake,” alisema jamaa mwingine aliyeitwa kwa jina la Jericho.
“Sawa. Ni wazo zuri pia,” alisema Chris.
Siku iliyofuata, asubuhi sana wakaanza kazi ya kumfuatilia huyo Latifa. Walichukua kompyuta yake na kuiweka namba ya msichana huyo, walipata maelekezo ambayo waliihamishia kwenye kifaa chao kidogo kilichoandikwa GPS kwa juu ambayo mnara ukasoma mpaka mahali msichana huyo alipokuwa.
Wakaanza kumfuatilia kimyakimya. Kwenye kifaa hicho kulikuwa na kinukta chekundu ambacho kilikuwa kikionyesha jina Latifa alivyokuwa akitembea kwani nacho kilikuwa kikienda mbele.
Walimfuatilia mpaka walipofika katika Mtaa wa Barabara ya Tano ambapo hapo waliwaona wasichana watatu wakiwa wamevalia madela, mmoja miongoni mwao alikuwa huyo Latifa waliyekuwa wakimtafuta.
“Sasa pale Latifa ni yupi?” aliuliza Chris.
“Inawezekana yule mwembamba mweusi!” alijibu Jericho.
“Kwa nini asiwe yule mnene au wa saizi ya kati?” aliuliza Chris.
“Hebu subiri nimpigie simu!” alisema Jericho.
Hapohapo akachukua simu yake na kumpigia Latifa. Msichana mnene aliyekuwa katikati akaanza kupekua kwenye mkoba wake na kutoa simu yake na kuipeleka sikioni.
“Halo!” alisikika Latifa, Jericho akakata simu.
“Tumempata!” alisema mwanaume huyo.
Waliwafuatilia wale wasichana, walikuwa wakitembea kwenda barabara kuu, hawakutaka kuwa na presha, walihitaji kumchukua Latifa katika staili ambayo kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angefahamu kama msichana huyo alitekwa.
Wakamtafuta dereva teksi ambaye walimuweka chini na kumwambia kuhusu Latifa, walimfuatilia kwenye mitandao ya kijamii, waliona namna alivyokuwa akiandika hadithi tamu hivyo walihitaji kuonana naye ili awe mmoja wa watunzi katika kampuni yao ambayo ilikuwa beneti na Kampuni ya Universal ambaye ilikuwa maarufu Marekani kwa upigaji wa muvi mbalimbali.
Dereva teksi alisikiliza maelezo ya watu hao, akakubali kuwasaidia na hivyo kumfuata Latifa ambaye alikuwa akisubiri daladala na wenzake.
Alipomfikia, akamsalimia na kumwambia kulikuwa na Wazungu wawili walikuwa wakimuulizia walikuwa kwenye gari lake.
Latifa akashtuka, hakuamini kama angeambiwa kitu kama hicho, alimuuliza maswali mwanaume yule, alimwambia ukweli kwamba walisoma simulizi zake kwenye Mtandao wa Facebook.
“Walisoma simulizi zangu?” aliuliza Latifa huku akionekana kushtuka, furaha aliyokuwanayo haikuweza kuelezeka.
“Ndiyo! Wanakutafuta sana!”
“Ni Wazungu kweli au Wazungu koko?”
“Ni Wazungu kabisa. Tena wanaonekana wana pesa,” alisema dereva yule.
Latifa alichanganyikiwa. Hakutaka kulemba, haraka sana akaondoka na kuelekea kwenye ile teksi ambapo Jericho akateremka na kumwangalia Latifa huku uso wake ukionekana kuwa na tabasamu pana.
“The best writer in Africa, madam Latifa,” (Mwandishi bora Afrika, Latifa) alisema Jericho huku akitabasamu, akamsalimia Latifa.
Akaanza kuongea na Latifa, alimsifia sana kwa kazi alizokuwa akizifanya, zilikuwa kazi bora kabisa ambazo hazikuwahi kuonekana sehemu yoyote ile.
Kwa uwezo mkubwa aliokuwanao hakutakiwa kuendelea kuishi nchini Tanzania bali alitakiwa kuchukuliwa na kuelekea nchini Marekani kwani kichwa chake kilikuwa pesa nyingi mno.
“We need to talk about this,” (Tunatakiwa kulizungumzia hili) alisema Jericho.
“No problem,” (Hakuna tatizo) alisema Latifa, kwa jinsi alivyosifiwa sana, hakutaka kuhisi vibaya, akaamini moja kwa moja kwamba watu hao walikuwa watu wa filamu na hata alipoambiwa aingie ndani ya gari, hakutaka kujiuliza, akaingia na dereva teksi kuambiwa kuliondoa gari hilo na kuelekea katika hoteli nzuri kwa lengo la kuongea.
“Mkonge Hotel is the nice place,” (Mkonge hoteli ni sehemu nzuri) alisema dereva na kuanza kuelekea huko huku Wazungu hao wakiendelea kuzungumza na Latifa ambaye aliwaambia hakuwa na kazi hizo tu, alikuwa na nyingine nyingi na ndoto yake kubwa ilikuwa ni kuandika filamu nchini Marekani.
“Your dreams have come true, you are going to get rich and famous,” (Ndoto zako zimetimia, utakuwa tajiri na maarufu mkubwa) alisema Jericho maneno yaliyomfanya Latifa kuwa na furaha kubwa mno.

Je, nini kitaendelea?
Endelea kufuatilia simulizi hii mpaka mwisho hapahapa.
Utajifunza mengi ambayo hukuwa ukiyafahamu na changamoto wanazopitia waandishi.
Ni vizuri sana kama waandishi wenyewe wakaja kujifunza hapa wakutane na mitego mbalimbali ambayo hawakuwa wakiifahamu.

Je, nini kiliendelea?
Usikose sehemu ijayo.
 

Chilojnr

Senior Member
Jul 5, 2012
141
500
NYEMO CHILONGANI
KALAMU YENYE SIRI YA DAMU
0718069269

Sehemu ya 04.

“Your dreams have come true, you are going to get rich and famous,” (Ndoto zako zimetimia, utakuwa tajiri na maarufu mkubwa) alisema Jericho maneno yaliyomfanya Latifa kuwa na furaha kubwa mno.
Hawakuchukua dakika nyingi wakafika katika hoteli hiyo. Muda wote huo Latifa hakuamini kama maisha yangekuwa rahisi kama yalivyokuwa, yaani Wazungu waje kutoka nchini Marekani na kumwambia alitakiwa kwenda kuandika filamu nchini Marekani.
Hapo hotelini, Jericho na Chris walionekana kuwa wachangamfu mno, waliongea na Latifa huku wakijifanya kuwa watu wema kabisa.
Waliagiza chakula, wakala na kunywa kiasi kwamba msichana huyo alizidi kuamini ni kweli watu hao walihitaji kufanya naye kazi.
“Ulianza kuandika hadithi mwaka gani?” aliuliza Chris.
“Ni kipindi kirefu sana! Nilianza kama utani lakini leo hii nimefika hapa,” alisema Latifa huku mkononi akiwa na paja la kuku akiendelea kula.
“Oh! Sawa! Sasa itabidi tupate waandishi wengine pia, tunahitaji waandishi watano, kuna wengine ambao unawafahamu tuanze kufanya nao kazi?” aliuliza Jericho huku muda wote uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana.
“Yeah! Kuna mmoja anaitwa Chilo Chilongani, Halfani Sudi, Stallone Joyful, Juma Hiza na wengineo,” alijibu msichana huyo.
“Safi sana! Nadhani tutatakiwa kumtafuta huyo Juma, anaishi wapi?” aliuliza Chris.
“Dar! Hao wote wapo Dar!” alijibu.
“Na una namba zake za simu?”
“Ndiyo! Ila siku hizi hapatikani,” alijibu.
“Hebu naziomba,” alisema Jericho.
Latifa hakutaka kujisumbua ni kwa sababu gani Wazungu hao walimuulizia sana Juma Hiza zaidi ya waandishi wengine, ilikuwa hivyo kwa sababu alitokea kuwaamini kwa kila kitu walichokuwa wakikisema mbele yake.
Akawapa namba hiyo ya Juma, ilikuwa ileile ambayo nao walikuwanayo na haikuwa ikipatikana. Walimwambia haikuwa ikipatikana hivyo kama ingekuwa rahisi kwao basi wamtafute mwandishi ambaye angekuwa akipafahamu na kwenda huko kumtafuta.
Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, Latifa aliwaambia walitakiwa kwenda jijini Dar na kuonana na mwandishi aliyeitwa kwa jina la Chilo Chilongani ambaye huyo alipafahamu mpaka alipokuwa akiishi Juma.
Hakukuwa na tatizo tena na hawakutaka kupoteza muda, siku hiyohiyo wakachukua ndege na kuondoka kuelekea jijini Dar kwa lengo la kuonana na Chilo ili awapeleke alipokuwa akiishi Juma.
Walipofika, kitu cha kwanza kilikuwa ni kumpigia simu O’Brain na kumwambia kilichotokea. Mwanaume huyo aliwapongeza kwani kwa hatua waliyofikia, ilikuwa kubwa na kulikuwa na matumaini makubwa kwamba huyo Juma Hiza angeweza kupatikana.
Baada ya kupanga mipango yao, simu ikapigwa mpaka kwa Chilo. Kwanza alipogundua alikuwa akiongea na Wazungu, alishtuka, hakuwahi kufikiria kupigiwa simu na watu hao na kuambiwa walitaka kuonana naye.
Alihisi kitu lakini kwa kuwa hakuwa na tatizo lolote lile, akakubaliana nao na kwenda kuonana nao. Walijitambulisha kama walivyojitambulisha kwa Latifa, mwandishi huyo alibaki akiwatazama tu kwa macho yaliyoonyesha ni kwa jinsi gani alikuwa na wasiwasi juu yao.
“Mmesema mmetoka Universal?” aliuliza Chilo huku akiwaangalia.
“Ndiyo!”
“Ooh! Vizuri sana. Tuwekeni mambo sawa kwanza. Naomba vitambulisho vyenu nijiridhishe, mnajua sasa hivi matapeli wengi sana,” alisema Chilo huku akitoa tabasamu, alijua alilokuwa akilifanya, kuna mambo mengi alijua kuhusu Hiza, misala yote aliyokuwanayo hivyo hakutaka kumwamini mtu yeyote yule.
Wazungu hao walijipanga, wakatoa vitambulisho na kumuonyeshea Chilo ambaye aliridhika na kuwaambia wamwambie alichokitaka.
“Tunahitaji kufanya kazi na waandishi wa Tanzania,” alisema Jericho.
“Waandishi wa Tanzania, mna maana gani?” aliuliza.
“Kwamba mkaandike muvi katika kampuni yetu!” alijibu Jericho huku akimwangalia mwandishi huyo kwa tabasamu pana.
“Kwa hiyo mmetoka huko mbali kwa lengo hilo tu?” aliuliza.
“Ndiyo!”
“Sawa! Hakuna shida!”
“Na tulikutana na mwandishi anaitwa Latifa, alituunganisha na wewe ila akasema na wewe utatuunganisha na Juma Hiza,” alisema Jericho.
“Ooh!”
“Sasa sijui naye tutampataje?”
“Juma Hiza? Kwani Latifa hakuwaambia?” aliuliza Chilo.
“Kwamba?”
“Alifariki dunia wiki iliyopita!”
“Alifariki?”
“Yaap!”
“Kivipi yaani?”
“Kwani kufariki kupo vipi?” aliuliza Chilo huku akiwaangalia, kwa jinsi muonekano wake ulivyokuwa, alionekana kufahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
Wazungu hao walikuwa kimya, walimwangalia Chilo, walijua kabisa walikuwa wakidanganywa lakini alijitahidi kuonyesha muonekano wake usiokuwa na shaka hata kidogo.
Aliendelea kuwaambia watu hao kwamba Juma Hiza alifariki wiki iliyopita baada ya kuugua ghafla malaria. Hakuishia hapo tu bali akawachukua na kuwapeleka katika makaburi ya Temeke na kuwaonyesha kaburi ambalo kwa juu liliandikwa Juma Hiza, lilikuwa na tarehe na mwaka aliofariki, ni kweli ilikuwa wiki iliyopita.
Wote wawili walichoka, hawakuamini kama walishindwa kumpata mtu huyo kwa sababu tayari alifariki. Baada ya kuliona kaburi hilo Chilo akaanza kuwaambia bila Juma Hiza hakuna kilichoharibika, hivyo mipango yao ilitakiwa kuendelea, apelekwe mpaka nchini Marekani kwa lengo la kuandika hizo filamu.
“Tutarudi mwezi ujayo na kuwachukua!”
“Yamekuwa mwezi ujayo tena?”
Chilo hakuzungumza kitu chochote kile, akakubaliana nao na hivyo kuondoka. Haraka sana Jericho akampigia simu O’Brain na kumwambia kila kitu kilichotokea.
Alimwambia kuhusu Chilo, alivyowaambia Juma Hiza alifariki wiki iliyopita na hakuishia hapo, aliwapeleka mpaka kwenye kaburi alipozikwa ambapo kwa juu kuliandikwa Juma Hiza.
Hilo likamchosha O’Brain, alihisi kabisa kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea. Aliwauliza kuhusu Chilo, muonekano wake wakati alipokuwa akiongea nye.
Alimwambia kila kitu na mwisho kabisa O’Brain kusema kwamba huyo Juma Hiza hakufa na kulikuwa na kila uwezekano huyo Chilo alikuwa akifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
“Kwa hiyo?”
“Fukueni kaburi kuhakikisha,” alisema O’Brain na kukata simu.
Hilo lilitakiwa kufanyika haraka sana, usiku wa manane kwenda huko kaburini na kufanya kazi hiyo. Wakanunua vifaa vyote vilivyokuwa vikihitajika na usiku wa siku hiyo wakaenda huko kaburini na kuanza kufukua kaburi lile.
Ilikuwa ni lazima wajue ukweli wa kila kitu kilichokuwa kimetokea. Walifukua na kufukua, hawakukutana na mwili. Waliendelea kufukua zaidi ya kile kipimo cha kuchimbwa kaburi lakini napo hawakufanikiwa kuuona huo mwili.
Walijua huo ulikuwa mchezo mchafu uliokuwa umechezwa na vijana hao. Ilikuwa ni lazima atafutwe huyo Chilo, iliwezekana kabisa alifahamu kuhusu Juma Hiza, na alijua mahali alipokuwa na hakutaka kuwaambia ukweli.
“Kuna namba zao za simu, hakikisheni mnadukua kila kitu na kufuatilia mawasiliano yao, kuna barua pepe, mawasiliano yao kwa njia ya WhatsApp tutakwenda kuwaomba wenyewe na watuambie ni kwa jinsi gani tutaweza kuwapata hao vijana, hili ni suala nyeti sana ambalo linahitaji kufanyiwa kazi haraka mno,” alisema O’Brain huku kwa jinsi sauti yake ilivyokuwa ikisikika tu, alionekana kuchanganyikiwa.
“Kwa hiyo tuna watu wawili, Chilo na Juma Hiza?”
“Ndiyo! Hakikisheni hao vijana wanapatikana. Tayari nimehisi kuna jambo moja kubwa, na kama halitofanyiwa kazi, kuna siku mtakuja kusikia Urusi na Al Qaida wamejua siri za jeshi letu kupitia kitabu kingine ambacho inawezekana Juma Hiza akakiandika,” alisema O’Brain.
“Na huyu Chilo anahusika vipi sasa na wakati hajawahi hata kutoa kitabu na kuweka Amazon?” aliuliza Chris.
“Sijajua! Ila moyo wangu unaniambia huyo mtu anaweza kuwa hatari sana kama mwenzake. Siku zote ndege wanaofanana huruka pamoja, fanyeni kila liwezekanalo hao watu wawili wapatikane haraka sana,” alisema O’Brain na kukata simu.
Kazi ikabaki kwa maofisa hao wa CIA kuanza kuwatafuta vijana hao wawili ambao walihisi wangekuwa hatari sana kwa usalama wa taifa kubwa kama Marekani. Walihitaji siri zao ziendelee kuwa siri milele.

Je, nini kitaendelea?
Sehemu ijayo tutaanza kuangalia mwanzo kabisa mambo haya yalipoanzia mpaka kufikia hapo.
 

moneytalk

JF-Expert Member
Jan 23, 2017
5,294
2,000
NYEMO CHILONGANI
KALAMU YENYE SIRI YA DAMU
0718069269

Sehemu ya 04.

“Your dreams have come true, you are going to get rich and famous,” (Ndoto zako zimetimia, utakuwa tajiri na maarufu mkubwa) alisema Jericho maneno yaliyomfanya Latifa kuwa na furaha kubwa mno.
Hawakuchukua dakika nyingi wakafika katika hoteli hiyo. Muda wote huo Latifa hakuamini kama maisha yangekuwa rahisi kama yalivyokuwa, yaani Wazungu waje kutoka nchini Marekani na kumwambia alitakiwa kwenda kuandika filamu nchini Marekani.
Hapo hotelini, Jericho na Chris walionekana kuwa wachangamfu mno, waliongea na Latifa huku wakijifanya kuwa watu wema kabisa.
Waliagiza chakula, wakala na kunywa kiasi kwamba msichana huyo alizidi kuamini ni kweli watu hao walihitaji kufanya naye kazi.
“Ulianza kuandika hadithi mwaka gani?” aliuliza Chris.
“Ni kipindi kirefu sana! Nilianza kama utani lakini leo hii nimefika hapa,” alisema Latifa huku mkononi akiwa na paja la kuku akiendelea kula.
“Oh! Sawa! Sasa itabidi tupate waandishi wengine pia, tunahitaji waandishi watano, kuna wengine ambao unawafahamu tuanze kufanya nao kazi?” aliuliza Jericho huku muda wote uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana.
“Yeah! Kuna mmoja anaitwa Chilo Chilongani, Halfani Sudi, Stallone Joyful, Juma Hiza na wengineo,” alijibu msichana huyo.
“Safi sana! Nadhani tutatakiwa kumtafuta huyo Juma, anaishi wapi?” aliuliza Chris.
“Dar! Hao wote wapo Dar!” alijibu.
“Na una namba zake za simu?”
“Ndiyo! Ila siku hizi hapatikani,” alijibu.
“Hebu naziomba,” alisema Jericho.
Latifa hakutaka kujisumbua ni kwa sababu gani Wazungu hao walimuulizia sana Juma Hiza zaidi ya waandishi wengine, ilikuwa hivyo kwa sababu alitokea kuwaamini kwa kila kitu walichokuwa wakikisema mbele yake.
Akawapa namba hiyo ya Juma, ilikuwa ileile ambayo nao walikuwanayo na haikuwa ikipatikana. Walimwambia haikuwa ikipatikana hivyo kama ingekuwa rahisi kwao basi wamtafute mwandishi ambaye angekuwa akipafahamu na kwenda huko kumtafuta.
Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, Latifa aliwaambia walitakiwa kwenda jijini Dar na kuonana na mwandishi aliyeitwa kwa jina la Chilo Chilongani ambaye huyo alipafahamu mpaka alipokuwa akiishi Juma.
Hakukuwa na tatizo tena na hawakutaka kupoteza muda, siku hiyohiyo wakachukua ndege na kuondoka kuelekea jijini Dar kwa lengo la kuonana na Chilo ili awapeleke alipokuwa akiishi Juma.
Walipofika, kitu cha kwanza kilikuwa ni kumpigia simu O’Brain na kumwambia kilichotokea. Mwanaume huyo aliwapongeza kwani kwa hatua waliyofikia, ilikuwa kubwa na kulikuwa na matumaini makubwa kwamba huyo Juma Hiza angeweza kupatikana.
Baada ya kupanga mipango yao, simu ikapigwa mpaka kwa Chilo. Kwanza alipogundua alikuwa akiongea na Wazungu, alishtuka, hakuwahi kufikiria kupigiwa simu na watu hao na kuambiwa walitaka kuonana naye.
Alihisi kitu lakini kwa kuwa hakuwa na tatizo lolote lile, akakubaliana nao na kwenda kuonana nao. Walijitambulisha kama walivyojitambulisha kwa Latifa, mwandishi huyo alibaki akiwatazama tu kwa macho yaliyoonyesha ni kwa jinsi gani alikuwa na wasiwasi juu yao.
“Mmesema mmetoka Universal?” aliuliza Chilo huku akiwaangalia.
“Ndiyo!”
“Ooh! Vizuri sana. Tuwekeni mambo sawa kwanza. Naomba vitambulisho vyenu nijiridhishe, mnajua sasa hivi matapeli wengi sana,” alisema Chilo huku akitoa tabasamu, alijua alilokuwa akilifanya, kuna mambo mengi alijua kuhusu Hiza, misala yote aliyokuwanayo hivyo hakutaka kumwamini mtu yeyote yule.
Wazungu hao walijipanga, wakatoa vitambulisho na kumuonyeshea Chilo ambaye aliridhika na kuwaambia wamwambie alichokitaka.
“Tunahitaji kufanya kazi na waandishi wa Tanzania,” alisema Jericho.
“Waandishi wa Tanzania, mna maana gani?” aliuliza.
“Kwamba mkaandike muvi katika kampuni yetu!” alijibu Jericho huku akimwangalia mwandishi huyo kwa tabasamu pana.
“Kwa hiyo mmetoka huko mbali kwa lengo hilo tu?” aliuliza.
“Ndiyo!”
“Sawa! Hakuna shida!”
“Na tulikutana na mwandishi anaitwa Latifa, alituunganisha na wewe ila akasema na wewe utatuunganisha na Juma Hiza,” alisema Jericho.
“Ooh!”
“Sasa sijui naye tutampataje?”
“Juma Hiza? Kwani Latifa hakuwaambia?” aliuliza Chilo.
“Kwamba?”
“Alifariki dunia wiki iliyopita!”
“Alifariki?”
“Yaap!”
“Kivipi yaani?”
“Kwani kufariki kupo vipi?” aliuliza Chilo huku akiwaangalia, kwa jinsi muonekano wake ulivyokuwa, alionekana kufahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
Wazungu hao walikuwa kimya, walimwangalia Chilo, walijua kabisa walikuwa wakidanganywa lakini alijitahidi kuonyesha muonekano wake usiokuwa na shaka hata kidogo.
Aliendelea kuwaambia watu hao kwamba Juma Hiza alifariki wiki iliyopita baada ya kuugua ghafla malaria. Hakuishia hapo tu bali akawachukua na kuwapeleka katika makaburi ya Temeke na kuwaonyesha kaburi ambalo kwa juu liliandikwa Juma Hiza, lilikuwa na tarehe na mwaka aliofariki, ni kweli ilikuwa wiki iliyopita.
Wote wawili walichoka, hawakuamini kama walishindwa kumpata mtu huyo kwa sababu tayari alifariki. Baada ya kuliona kaburi hilo Chilo akaanza kuwaambia bila Juma Hiza hakuna kilichoharibika, hivyo mipango yao ilitakiwa kuendelea, apelekwe mpaka nchini Marekani kwa lengo la kuandika hizo filamu.
“Tutarudi mwezi ujayo na kuwachukua!”
“Yamekuwa mwezi ujayo tena?”
Chilo hakuzungumza kitu chochote kile, akakubaliana nao na hivyo kuondoka. Haraka sana Jericho akampigia simu O’Brain na kumwambia kila kitu kilichotokea.
Alimwambia kuhusu Chilo, alivyowaambia Juma Hiza alifariki wiki iliyopita na hakuishia hapo, aliwapeleka mpaka kwenye kaburi alipozikwa ambapo kwa juu kuliandikwa Juma Hiza.
Hilo likamchosha O’Brain, alihisi kabisa kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea. Aliwauliza kuhusu Chilo, muonekano wake wakati alipokuwa akiongea nye.
Alimwambia kila kitu na mwisho kabisa O’Brain kusema kwamba huyo Juma Hiza hakufa na kulikuwa na kila uwezekano huyo Chilo alikuwa akifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
“Kwa hiyo?”
“Fukueni kaburi kuhakikisha,” alisema O’Brain na kukata simu.
Hilo lilitakiwa kufanyika haraka sana, usiku wa manane kwenda huko kaburini na kufanya kazi hiyo. Wakanunua vifaa vyote vilivyokuwa vikihitajika na usiku wa siku hiyo wakaenda huko kaburini na kuanza kufukua kaburi lile.
Ilikuwa ni lazima wajue ukweli wa kila kitu kilichokuwa kimetokea. Walifukua na kufukua, hawakukutana na mwili. Waliendelea kufukua zaidi ya kile kipimo cha kuchimbwa kaburi lakini napo hawakufanikiwa kuuona huo mwili.
Walijua huo ulikuwa mchezo mchafu uliokuwa umechezwa na vijana hao. Ilikuwa ni lazima atafutwe huyo Chilo, iliwezekana kabisa alifahamu kuhusu Juma Hiza, na alijua mahali alipokuwa na hakutaka kuwaambia ukweli.
“Kuna namba zao za simu, hakikisheni mnadukua kila kitu na kufuatilia mawasiliano yao, kuna barua pepe, mawasiliano yao kwa njia ya WhatsApp tutakwenda kuwaomba wenyewe na watuambie ni kwa jinsi gani tutaweza kuwapata hao vijana, hili ni suala nyeti sana ambalo linahitaji kufanyiwa kazi haraka mno,” alisema O’Brain huku kwa jinsi sauti yake ilivyokuwa ikisikika tu, alionekana kuchanganyikiwa.
“Kwa hiyo tuna watu wawili, Chilo na Juma Hiza?”
“Ndiyo! Hakikisheni hao vijana wanapatikana. Tayari nimehisi kuna jambo moja kubwa, na kama halitofanyiwa kazi, kuna siku mtakuja kusikia Urusi na Al Qaida wamejua siri za jeshi letu kupitia kitabu kingine ambacho inawezekana Juma Hiza akakiandika,” alisema O’Brain.
“Na huyu Chilo anahusika vipi sasa na wakati hajawahi hata kutoa kitabu na kuweka Amazon?” aliuliza Chris.
“Sijajua! Ila moyo wangu unaniambia huyo mtu anaweza kuwa hatari sana kama mwenzake. Siku zote ndege wanaofanana huruka pamoja, fanyeni kila liwezekanalo hao watu wawili wapatikane haraka sana,” alisema O’Brain na kukata simu.
Kazi ikabaki kwa maofisa hao wa CIA kuanza kuwatafuta vijana hao wawili ambao walihisi wangekuwa hatari sana kwa usalama wa taifa kubwa kama Marekani. Walihitaji siri zao ziendelee kuwa siri milele.

Je, nini kitaendelea?
Sehemu ijayo tutaanza kuangalia mwanzo kabisa mambo haya yalipoanzia mpaka kufikia hapo.
shukran mkuu
 

Chilojnr

Senior Member
Jul 5, 2012
141
500
NYEMO CHILONGANI
KALAMU YENYE SIRI YA DAMU
0718069269
SEHEMU YA 05

MIAKA KADHAA NYUMA

Walikuwa ni marafiki wawili wakubwa waliokutana katika mtandao wa Facebook. Walikuwa waandishi wa simulizi zilizokuwa zikipendwa sana katika mtandao huo.
Mtu wa kwanza kuandika simulizi hizo alijulikana kwa jina la Chilo Chilongani. Alikuwa mwanaume mweusi, sura pana kidogo na kidevuni mwake alikuwa na vijindevu fulani vilivyokuwa vikionekana kila alipokuwa akisimama mbele za watu.
Alipendwa, maandishi yake yakawa maarufu kupita jina lake, kila mwandishi aliyekuwa akichipukia kipindi hicho alitamani kuandika kama Chilo, ama kumkaribia au kumpita kabisa. Simulizi zake zilikuwa za kusisimua mno, alikuwa akiziandika kwa hisia kali, alipohitaji ucheke, ulicheka bila kupenda, alipohitaji unune, ulinuna kweli na hata alipotaka ulie, ilikuwa ni lazima ulie kama mtu aliyekuwa amefiwa.
Simulizi zake ilikuwa kubwa kuliko muonekano wake, kichwa chake kilikuwa kikifahamu mambo mengi duniani, inawezekana zaidi ya waandishi wengine, alikuwa mtaalamu wa kuandika simulizi za kila namna, alipoandika simulizi kuhusu mapenzi, ilikuwa ni rahisi sana kujua jamaa aliwahi kupendwa ama kupenda kuliko mtu mwingine duniani kwani alikuwa akiandika kwa hisia kali mno.
Alipokuwa akiandika simulizi kuhusu hospitali basi ilikuwa ni rahisi kuhisi jamaa alikuwa na digrii ya utabibu aliyoichukua katika Chuo Kikuu cha Mumbai na kuwa daktari katika Hospitali ya Ganga nchini India.
Alikuwa akifahamu mambo mengi duniani, alipoamua kuandika kuhusu mambo ya sheria na kesi za mahakamani wala haikuwa kazi kuhisi jamaa alikuwa mmoja wa mawakili waliokuwa na akili kubwa mno, na hata alipoamua kuandika kuhusu upelelezi, ilikuwa ni rahisi kusema alikuwa mmoja wa maofisa kutoka katika kitengo cha kipelelezi Tanzania, TISS.
Alikuwa ni mwandishi aliyekamilika, aliyekuwa akiandika mambo ya kichawi kama alikwishawahi kwenda kuwanga ama kukutana na wachawi huko Gamboshi, kila kitu alichokuwa akikiandika Chilo alikiandika kwa asilimia mia moja bila kuleta maswali yoyote yale.
Mbali na kuwa na urafiki na waandishi wengi wa simulizi kama Ally Katalambula, Stallone Joyful lakini Chilo alikuwa rafiki mkubwa wa Juma Hiza. Wawili hao walikuwa wakitembeleana na kubadilishana mawazo mara kwa mara.
Urafiki wao ulikuwa mkubwa kiasi cha familia zao kufahamiana, wote walikuwa na ndoto moja vichwani mwao, kuwa waandishi wakubwa wa simulizi hapo baadaye.
Baada ya kukaa kwa miaka kadhaa ndipo wazo moja likajengwa kichwani mwa Chilo. Aliandika simulizi nyingi, zilizofurahisha, kufundisha na hata kuburudisha. Alikuwa na uwezo wa kumjenga mhusika kuonekana kuwa na akili kubwa ya kufanya jumlisha ionekane kama msalaba ama alama ya kuzidisha ionekane kama herufi x.
Wazo kubwa alilokuwanalo kichwani mwake ilikuwa ni lazima kumshirikisha Juma, waonane na kuzungumza kuhusu suala hilo, hakutaka kubaki kimya, haraka sana akampigia simu na kuomba kuonana naye.
“Tuonane tena? Kwa nini tusiongee kwenye simu braza?” alisikika Juma akiuliza.
“Ni jambo muhimu sana! Huu mpango hautakiwi kugundulika na mtu yeyote yule kwani utatufanya tuwe mabilionea wakubwa,” alisema Chilo.
“Sawa! Kwa hiyo nije wapi?”
“Home hapa!”
“Haina noma!” alisema Juma na simu kukatwa.
Chilo akatulia kitandani kwake, kichwa chake kilikuwa na mawazo tele, alikuwa na mambo mengi ya kufanya lakini kubwa zaidi lilikuwa ni kupata pesa, ila iwe kwa njia halali.
Kila alipokaa na kufikiria, kichwani mwake kulikuja majina ya watu watatu, Robert, Robinson na Richard aliowaandika katika kitabu cha riwaya cha Dili la Dola Bilioni Nne.
Vijana hao walifanya mambo makubwa, walianzia sifuri mpaka kuwa mabilionea. Kama yeye ndiye aliyewatengeneza watu hao na kuonekana kuwa na akili kubwa, kwa nini yeye asiwe na akili hiyo?
Hakuwa akijua sana teknolojia kama uwezo aliompa Robinson, hakuwa na sura nzuri ya kuwavutia wasichana kama aliyompa Richard ila aliamini alikuwa msuka mipango mizuri zaidi ya alivyokuwa Robert na ndiyo maana akaamua kumpigia simu Hiza na kutaka kuonana naye.
Ni ndani ya nusu saa, Juma alikuwa nyumbani kwa Chilo kwa lengo la kuzungumza naye, kitu cha kwanza alichokifanya mwanaume huyo ni kumpa kitabu chake cha Dili la Dola Bilioni Nne kitu kilichomfanya Juma kushangaa.
“Kuna nini tena mbona unanipa kitabu?” aliuliza Juma huku akimwangalia Chilo.
“Humo kuna vijana watatu! Mmoja aliitwa Robinson, huyo jamaa alikuwa mtaalamu wa kompyuta, yaani kwenye masuala ya kompyuta hapakuwa na kitu kilichokuwa kikimshinda,” alisema Chilo huku akimwangalia Juma.
“Sawa. Nimeisoma! Lengo lako ni nini bro?” aliuliza Juma, mpaka muda huo hakujua Chilo alikuwa na maana gani.
“Ukiachana na Robinson humo kuna kijana anaitwa Richard, yule fala alikuwa na sura nzuri sana, nina uhakika hata demu wako angemuona angemtaka kimapenzi tu,” alisema Chilo na kuanza kucheka.
“Bro we’ mjinga sana...Hahaha!” alisema Juma na kuanza kucheka.
“Achana na huyo, humu kuna mtu mwingine, huyu ndiye amefanya nikuite mahali hapa,” alisema Chilo.
“Bila shaka ni mzee wa mipango, yule Mchaga Robert!” alisema.
“Exactly,” (Hakika) alisema Chilo.
“Aya niambie kuhusu huyo jamaa!”
“Hivi unajua kwamba uwezo wa Robert unaosifiwa na wasomaji ulitoka kwenye hili bichwa langu?” aliuliza Chilo huku akimwangalia Juma.
“Hahaha! Ndiyo!”
“Sasa kama uwezo huo ulitoka kwenye hiki kichwa, kwa nini na mimi nisifanye mitikasi kama huyo jamaa?” aliuliza Chilo huku akimwangalia Juma aliyeonekana kushangaa kidogo.
“Sijakusoma mbaba!”
“Nataka kusuka mpango! Kuna mtu nilionana naye juzikati, huyu mtu tutamuingiza kwenye mipango! Utakuwa tayari?” alisema Chilo na kuuliza.
“Mtu gani?”
“Nikikwambia sasa hivi mpango wetu hautoweza kufanikiwa, ila nitataka tufanye kwanza halafu baadaye utajua ni mtu gani!” alisema Chilo.
“Mh!” Juma akaguna.
“Ninataka kukupa akili moja kubwa sana,” alisema Chilo.
“Akili gani?”
“Kubwa sana!”
“Ipo vipi?”
“Unaamini kama CIA wanaweza wakamtafuta bwege mmoja kama wewe ambaye kila siku unajiona si lolote?” aliuliza Chilo huku akimwangalia Juma.
“Yaani wanitafute mimi? Kwa lengo gani?”
“Kuwaonyesha mahali ulipopata hizo akili kubwa!”
“Akili gani”
“Hizi ninazotaka kuzipandikiza kichwani mwako!”
“Zipoje?”
“Ni kubwa!”
“Ukubwa kama wa kontena?”
“Hapana! Ni ukubwa zaidi ya uwanja wa taifa, ni kubwa zaidi ya mbuga ya Serengeti!” alisema Chilo, wote wakaanza kucheka, halafu Chilo akarudi katika sura yake ile ya usiriazi.
“Nataka tupige pesa kupitia kitabu!”
“Kitabu gani? Tuuze kopi ngapi? Elfu tano ama?”
“Hapana! Kopi hata milioni moja na zaidi!” alijibu.
“Damn! Mzee baba unajua kopi milioni moja tuna kiasi gani hapo?”
“Ni pesa nyingi, ila ni lazima tuwe makini kwenye upigaji huo wa pesa!”
“Kivipi? Tutaiba ama?”
“Hapana! Tutacheza mchezo wa namba!”
“Mchezo wa namba, unamaanisha nini?”
Chilo hakujibu swali hilo, akachukua kidaftari chake kidogo anachopenda kuandikia mambo yake kilichokuwa pembeni ya kitanda chake na kumpa Juma, kikaratasi kile kiliandikwa namba tatu tu, yaani 185. Juma akaziangalia lakini akashindwa kujua zilikuwa na maana gani.
“Zinamaanisha nini hizi?”
“Ni matokeo ya jina la Kitabu!”
“Kitabu kipi?”
“Kitakachokwenda kuwafanya CIA wakutafute?”
“Mh! Ndiyo kipi? Nitakiandika mimi?”
“Hapana! Nimekiandika mimi! Kimekamilika. Nitataka uonekane wewe ndiye umekiandika, yaani ujulikane wewe ndiye mwandishi!” alisema Chilo.
“Kwa nini mimi na si wewe?”
“Kwa sababu ukikamatwa, nikiwa uraiani nitaendelea kucheza michezo hatari na kuhakikisha unatoka hata kama wamekufunga kwenye gereza gumu kama Guantanamo!” alijibu Chilo.
“Yaani sijakuelewa mbaba, unaongea sana kwa mafumbo!” alisema Juma.
“Usijali! Utaelewa kila kitu! Nitakwenda hatua kwa hatua, mwisho wa siku utajua namaanisha nini!” alisema Chilo.
“Umesema kuhusu namba 185 ni matokeo ya jina la kitabu, kitabu gani?”
“Hicho nilichokiandika!”
“Ambacho kinaitwa?”
“There Is No God At All,” (Hakuna Mungu Kabisa)
“Wewe mtu utalaaniwa!” alisema Juma na kutoa kicheko cha chini.
“Wakati mwingine unapotafuta pesa, mchokoze kidogo Mungu, mfurahishe kidogo shetani akuone wewe ni swahiba wake, halafu baadaye unamgeuka, unakuwa rafiki wa Mungu na adui wa shetani!” alisema Chilo.
“Sijakuelewa!”
“Unaamini kwamba kuna watu wana pesa za kishetani?”
“Naamini!”
“Na unaamini watu hao hao wanatoa sadaka na kusaidia masikini?” aliuliza.
“Ndiyo ninaamini!”
“Hiyo ndiyo maana yangu!” alisema Chilo na kuanza kucheka kama kawaida yake, ila kicheko chake kilikuwa cha chini.
“Turudi kwenye namba!”
“Hii hutoweza kujua ninamaanisha nini, na si wewe, hata CIA nao hawatojua maana ya hii namba! Ila nitakwenda kusuka mpango kuhakikisha hii namba inagundulika, na siku ambayo itagundulika inamaanisha nini, tutakuwa mabilionea zaidi!” alisema Chilo.
“Unamaanisha kabla ya namba kugundulika tutakuwa mabilionea? Ila ikigundulika tutakuwa mabilionea zaidi?” aliuliza Juma.
“Ndiyo! Hiki kitabu tutakiingiza sokoni, kwenye mtandao wa Amazon, mwandishi utakuwa wewe, nina uhakika kwa kupitia jina hili la kitabu, kitanunuliwa sana,” alisema Chilo.
“Sasa Wazungu watanunua wakiona kimeandikwa na mtu mwenye jina la Juma Hiza?” aliuliza Juma.
“Usijali! Utaitwa Williams McCannon!”
“Hilo jina umelitoa wapi?”
“Nalo pia ni mchezo wa namba, yaani kama ile 185,” alijibu Chilo.
“Bado unanichanganya sana na manamba yako!”
“Wala usijali! Sasa ikitokea wewe ukakamatwa, huyo mtu ambaye kwa sasa sitaki kukwambia ni nani ataingilia mchezo kwa lengo la kuwavuruga watu watakaokukamata!” alijibu.
“Akina nani?”
“CIA na Al Qaida!”
“Hebu subiri kwanza...nimesikia Al Qaida...hawa ninaowajua mimi ama mtaa ule wa kule Kijitonyama unaoitwa Al Qaida?” aliuliza Juma.
“Haohao unaowajua wewe!”
“Inawezekanaje?”
“Ndiyo maana nakwambia kama hili bichwa lishawahi kumtengeneza mtu kama Robert na mipango yake kabambe, kwa nini bichwa hilihili lisitumike kutengeneza matukio kama haya, tukapiga pesa na kutimka zetu?” alisema Chilo.
“Dooh! Wewe jamaa wewe...hakika sijuti kukufahamu!” alisema Juma.
“Hahaha! Nenda nyumbani! Nataka ujifikirie kwa wiki nzima! Utakuwa tayari kumiliki kiasi cha shilingi trilioni mbili ama hutokuwa tayari? Kama utakuwa tayari, naomba uniambie! Msalimie sana mtoto wako, Ilham,” alisema Chilo.
“Zimefika!” aliitikia Juma na kuondoka mahali hapo. Sasa kazi ikawa ni kusubiri kuona mwanaume huyo angefanya jambo gani kuhakikisha zile pesa alizomwambia zinaingia kwenye akaunti yake, ila kilichokuwa kikimtisha ni uwepo wa maofisa wa CIA kutoka nchini Marekani na magaidi wa kundi la AL Qaida la huko nchini Afghanistan katika mpango huo.

Je, nini kilitokea?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom