Kakobe "Tanganyika huru lazima ipatikane, Nyerere sio Mungu naye alikuwa na mapungufu yake"

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Amesema Tanganyika huru lazima ipatikane ni suala la muda tu Nchi yetu imekuwa katika laana kwa muda mrefu kwa sababu tumeshindwa kuilinda mipaka yetu Moto wa kudai Tanganyika umewaka na hamna mtu awezaye kuuzima.

Awaonya watawala kusoma alama za nyakati na amewataka kuiepusha nchi kuingia katika machafuko kwa kuridhia Serikali ya Tanganyika. Pia amesema Nyerere sio Mungu naye ana mapungufu yake wanaomuabudu wanakosea.

Kosa alilolifanya Nyerere ni kuruhusu kuunda serikali hewa ya Tanzania bara ambayo kimsingi haipo ukiliganisha na Zanzibar.

Amewaonya viongozi wanaopinga kurejeshwa kwa Tanganyika kuwa wataitumbukiza nchi katika machafuko.

Hizo zilikuwa salamu za Pasaka alizozitoa leo katika kanisa la FGBF Dar es salaa.
 
Maaskofu 32 Tanzania mzima wanatetea rasimu ya Mhs Jdg Warioba!!
Maalimu Prof Lipumba anatetea rasimu ya Jdg Warioba!!
Hawa MaCCM kina Lukuvi kuifumua hiyo rasimu wanawakilisha maoni ya nani???
Maoni ya Jdg Warioba Tanganyika ikae meza moja na Zenji wajadili ni muungano upi wanautaka!!
 
Neno askofu linatumika vibaya. Kila anayeibuka anajiita askofu. Hao 32 ni wepi? Ili uwe askofu si mchezo. Askofu ni phd holder.
 
Hao maaskofu ni wa madhehebu gani? Baba yetu Pengo ameshatoa msimamo wake. Wengine ni wapiga mayowe tu
 
Hao maaskofu ni wa madhehebu gani? Baba yetu Pengo ameshatoa msimamo wake. Wengine ni wapiga mayowe tu

Juzi nilitoa comment hapa Jf kuwa Cardinali Pengo sio msemaji wa ka isa katoliki, alichosema yy ni kauli yake na mtazamo wake.
TEC ndy chombo rasmi la kanisa katoliki lenye kutoa tamko kwa niaba ya kanisa.
 
Hao maaskofu ni wa madhehebu gani? Baba yetu Pengo ameshatoa msimamo wake. Wengine ni wapiga mayowe tu

Baba ako si baba yetu sisi, unataka na sisi tuunge mkono akilifupi za baba yako? Yale alotoa ni mawazo yake si kwamba alikaa akakubaliana na ninyi watoto wake
 
Askofu Kakobe ni mwiba kwa ccm tayari naona wamesha anza kutoa povu."..........nimekuwa adui yenu kwa sababu naseme yaliyo ya kweli"
 
Juzi nilitoa comment hapa Jf kuwa Cardinali Pengo sio msemaji wa ka isa katoliki, alichosema yy ni kauli yake na mtazamo wake.
TEC ndy chombo rasmi la kanisa katoliki lenye kutoa tamko kwa niaba ya kanisa.
Hao TEC ni mawakala na vibaraka wa UKAWA.
 
Baba ako si baba yetu sisi, unataka na sisi tuunge mkono akilifupi za baba yako? Yale alotoa ni mawazo yake si kwamba alikaa akakubaliana na ninyi watoto wake
Kwani hao maaskofu waliotoa Kauli za kipuuzi akiwemo Kakobe wametumwa na waumini wao? Acheni kuwashabikia hawa wachumia tumbo
 
Neno askofu linatumika vibaya. Kila anayeibuka anajiita askofu. Hao 32 ni wepi? Ili uwe askofu si mchezo. Askofu ni phd holder.
Kweli PhD inaitajika lakini siyo lazima kwani Bill Gate hakuitaji PhD kwanza kuasisi hiyo program unatumia kupost ujumbe wako
 
Huyu Kakobe anashindwa kabisa kuficha mahaba yake dhidi ya chama flani cha siasa, anawagawa wafuasi wake.
 
Back
Top Bottom