Mkuu Mzee Mwanakijiji, Rais Magufuli Sio Alfa na Omega. Rais Sio Mungu! Na Kwenye Utawala ni Katiba!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,685
119,325
Wanabodi,

Hili ni bandiko la kumjibu mwana JF mwenzetu, Mkuu Mzee Mwanakijiji, aliyesema rais Magufuli ni alfa na omega, hapa mimi natofautiana naye kuwa rais Magufuli sio alfa na omega, Alfa na Omega ni Mungu tuu pekee!. Rais wa nchi sio mungu hivyo kumuita Rais Magufuli kuwa alfa na omega, ni sawa na kumuita rais wa nchi ni mungu!. Rais wa nchi sio mungu bali ni mkuu wa nchi yetu ya Tanzania. Alfa na Omega ni kila kitu, rais wa nchi sio kila kitu, hivyo rais Magufuli hawezi kuwa alfa na omega, bali katika mambo ya utawala na uongozi wa nchi, then yes, rais ni alfa na omega, kama ilivyo kwa Mungu na mungu. Haya mambo ya watu kuwa na mahaba na kiongozi wao hadi kupitiliza na kuanza kumuita majina ya Mungu kama alfa na omega, inakuwa ni kama kutaka kumuabudia!. Japo hili linafanyika kwa nia njema, tunaweza kujikuta tunamponza mtu wetu bure bila sisi kujijua, pale Alfa na Omega mwenyewe atakaposikia kuna binadamu anaitwa alfa na omega hivyo Alfa na Omega mwenyewe akaamua kufanya yake!.

Tukiacha tumpe Mungu yaliyo ya KiMungu, na tumpe Kaisary yaliyo ya Kaisari, tukija kwa yaliyo ya Kaisari na kwenye utawala wa nchi, pia rais bado sio alfa na omega, watawala waliokuwa alfa na omega, walikuwa ni watawala wa kifalme, au watawala wa Rumi ya kale kama kina Herode au Kaizari, lakini kwenye tawala za sasa za kidemokrasia, Mkuu wa nchi sio alfa na omega, alfa na omega ya utawala wa nchi ni katiba na sio rais, ndio maana akiishachaguiwa, anaapishwa kwa katiba na kuapa kuilinda katiba, hivyo katiba ya nchi ndio kila kitu, rais yuko chini ya katiba. Kitendo chá rais Magufuli kuikanyaga katiba aliyo apa mbele ya Mungu kuilinda, na kuachwa tuu hivi hivi akiangaliwa tuu, ndiko kumepelekea baadhi yetu kumuona yeye ndio kila kitu hadi kumfananisha na Alfa na Omega.
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa ufupi ni kuwa Rais amesema tuhuma zinazomkabili Mkuu wa Mkoa wa Dar Bw. Paul Makonda hazijamfanya afikirie mara mbili uteuzi wake. Ni kweli kuwa Rais ndiye aliyemteua na ni yeye pekee anayeweza kutengua uteuzi wake.

Na niseme neno moja tu kwa Makonda. Una bahati kuwa Rais ameonesha imani yake kwako. Ni wakati wa wewe mwenyewe kujiangalia, kujisahihisha na kutengeneza ulipobomoka. Usije kukaa na kutegemea imani ya Rais tu ukaamini unaweza kufanya lolote. Magufuli amekuacha si kwa sababu unafanya vizuri; amekuacha ili kufunga vinywa vya sauti zilizokuwa zinampigia kelele; amekuacha ili kuwaambia watu "yeye ndiyo alfa na omega wa utawala nchini" kitu ambacho ni kweli.
Hata mimi jana nilimsikia Mhe. Rais Magufuli alipozungumza kuwa kwenye mambo ya uteuzi, alisema yeye ndio kila kitu, hakuna yoyote anayeweza kumpangia kitu, au kumuelekeza cha kufanya, hivyo kwa namna moja, rais yuko right kwenye uteuzi wa mwisho, yeye ndio kila kitu kwa upande mmoja, ila sio kila kitu kwa upande mwingine kwa sababu kwenye baadhi ya nafasi, lazima rais aletewe majina ya wenye sifa na lazima ateue miongoni mwa majina hayo, hivyo kitu ambacho ni kila kitu ni katiba ndio kila kitu hivyo kuna vitu hata rais anapangiwa cha kufanya na katiba na kulazimishwa avifanye kwa mujibu wa katiba itakavyo elekeza.

Hii maana yake ni kuna vitu ambavyo rais anaweza kuvifanya kwa mapenzi yake na ridhaa yake, at his own pleasure and his discretion kwa mapenzi yake na kuna vitu rais anatakiwa kuvifanya sio kwa ridhaa yake, not at his own discretion or at his pleasure kwa mapenzi yake, bali huvifanya kwa mujibu wa maelekezo ya katiba, hivyo katiba ndio kila kitu na sio rais ndio kila kitu, ila kwa sasa Tanzania hapa tulipo, tunaelekea kwenye direction ya totalitarian ambapo rais ni kila kitu!.

Miongoni mwa vitu ambavyo rais anavifanya kwa ridhaa yake na mapenzi yake ni pamoja na mamlaka yake ya teuzi mbalimbali za wasaidizi wake, hakuna wa kumpangia au kumlazimisha amteue nani, katiba imeweka kipengele cha kabla hajawateua wakuu fulani fulani, anaweza kushauriana na wasaidizi wake au vyombo fulani, mfano majaji, etc, lakini katika kufikia uamuzi wa mwisho ni nani amteue, katiba yetu imempa mamlaka yote rais kufikia uamuzi wa mwisho yeye mwenyewe kama yeye bila kufuata ushauri wa yeyote, isipokuwa uteuzi wa Waziri Mkuu tuu pekee, ndio Bunge limepewa mamlaka ya mwisho kuridhia mteule wa rais, kama rais akimteua mtu wa hovyo kuwa Wazri Mkuu, Bunge limepewa mamlaka ya kuridhia uteuzi wa Waziri Mkuu, Bunge linaweza kumkatalia, na kumlazimisha rais, ateue mtu mwingine, (ila pia hebu tusemezane ukweli, kwa Bunge letu hili, na wabunge wetu hawa, hata kama rais Magufuli akipendekeza jina la Waziri Mkuu ni yule Bi. Sundi au Janet, kuna mtu wa kumkatalia?). Lakini katika teuzi nyingine zote, rais wetu amepewa mamlaka bila kuingiliwa, kuteua yoyote at his pleasure na kutengua yoyote. Kuhusu mamlaka ya rais kumteua yoyote, nimeieleza hapa. Je, wajua Rais aweza kuteua yeyote hata darasa la saba?. Teuzi hizi hazihojiwi popote na yeyote!

Lakini inapotokea mteule wa rais anapofanya makosa ya jinai, uamuzi wa rais kutengua uteuzi wake, haupo tena kwenye ridhaa ya rais kwa mapenzi yake, yaani at his pleasure or discretion bali sasa hugeuka kwenye kutimiza wajibu kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, mteule wa rais akifanya jinai, hata rais ampende vipi, mteule wake akimess, he has to go!. Hili limewahi kutokea kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mzee Kissoky, aliyemuua mke wake mdogo kwa wivu wa mapenzi, alikuwa ni best sana wa Nyerere, but he had to go. Mkuu wa mkoa wa Tabora, Capt. Ditopile Mzuzuri (Brother Ditto) aliyekuwa best wa Jakaya, alipomuua yule dereva wa daladala kwa hasira, he had to go!. Hivyo kama ni kweli, Makonda amefoji jina, amefoji vyeti, na mna uthibitisho na ushahidi usio tia shaka, kisha akavitumia vyeti hivyo vya kufoji kujiendeleza, then hii ni jinai, jinai hii ikithibitishwa na vyombo husika, hata rais ampende vipi, Makonda anakuwa hana jinsi, he has to go!. Kama ni kweli Makonda amefoji lakini rais Magufuli, anampenda sana Makonda, then rais Magufuli yuko free amchukue akanywe nae chai Ikulu, lakini public office haiwezi kushikwa na criminals!.

Kwanza sote tunakubaliana kwa kauli moja kuwa Mhe. Rais Magufuli ndiye rais wetu, ndio mamlaka kuu kupita zote za kiutawala nchini mwetu mwenye nguvu na mamlaka zote za dola kwa mujibu wa katiba, hivyo anapaswa kuheshimiwa, lakini sio kuogopewa au kuabudiwa as if yeye ni Mungu!. Hili nimelizungumza hapa Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Hizo mamlaka alinazo rais Magufuli, sii malí yake binafsi kama John Pombe Joseph Magufuli, bali tumeuazima kama dhamana tuu baada ya sisi (we the people) kumuajiri kazi ya kututawala kama rais wetu, kupitia taasisi ya urais, sisi ndio waajiri wake, ndio tunayemlipa mshahara wake, tunaemlisha, kumvisha na kumuhudumia yeye na família yake kwa kodi zetu na hizo powers alizonazo kama rais wa JMT, sio personal powers za kwake as if ni mali yake, bali institutional powers za ile taasisi ya urais inayoshikiliwa na rais, ni mali ya Watanzania na tumemuazima tuu rais Magufuli kuzishika kama dhamana tuu ya kututawa kwa mkataba wa miaka mitano mitano kwa mujibu wa katiba na atafanya kile sisi waajiri wake tulichomtuma pale kwenye Ikulu yetu tulipompangisha kama mpangaji kwa mkataba wa miaka mitano mitano, kwa mujibu ya ile ilani yake, na sio kufanya chochote anavyotaka yeye. Mkataba wa miaka 5 ya mwanzo ukiisha tunaweza kumuongezea mkataba wa miaka 5 mingine, au tunaweza hata kuukatisha wakati wowote kukiwa na sababu za msingi kupitia katiba yetu.

Rais ana powers, ila sio absolute powers, yuko chini ya katiba, katiba ndio kila kitu, hata rais akimess, anaondoshwa kupitia kifungu Namba 46A.chá katiba yetu (1977)

Magufuli kama rais wetu ana two personalities, ya kwanza yeye ni mtu, ni binadamu anayeitwa John Pombe Joseph Magufuli ambaye ni binadamu, a human being kama sisi na sio malaika, hivyo yeye kama binaadamu mwingine yoyote, anaweza kuwa na mapungufu yake ya kibinadamu, ambayo inatubidi tuyavumile. Moja ya mapungufu makubwa ya rais Magufuli ya kibinaadamu, ni ile pride ya Kisukuma-Kihaya ya kujisikia kuwa yeye ndio kila kitu!, hili la kujisikia ni human nature ya baadhi ya makabila fulani fulani ya tabia za braaging, hivyo anaweza kumgombeza mtu yoyote popote. Magufuli wa pili ni Rais Magufuli taasisi ya urais, anayeshikilia taasisi hiyo ni rais, huyu ni top boss, kupitia urais, then rais Magufuli ana mamlaka yote ya kufanya chochote bila kuulizwa na yoyote. kwa vile yeye ndio rais wetu.

Ili kumpa mamlaka, rais akiishachaguliwa anaapishwa kwa mujibu wa katiba kuwa atailinda, kuitetea na kuitawala nchi kwa mujibu wa katiba kwa kuitekekeza katiba ya JMT. Lakini kwa bahati mbaya sana, kwa Tanzania ya sasa, japo rais Magufuli ameapa kuilinda katiba, lakini inawezekana kabisa yeye akawa haijui kuwa mamlaka yake yamewekewa mipaka, kuna vitu rais anaweza kufanya na kuna vitu rais hawezi kufanya hata kama yeye ni rais, hivyo yeye hapaswi kujua kila kitu ndio maana amewekewa wasaidizi wanaojua kila kitu lakini baadhi ya wasaidizi hawa, hawatimizi wajibu wao ipasavyo kwa kumshauri rais ipasavyo, ndio maana kuna baadhi ya maamuzi ya Rais Magufuli yanakwenda kinyume cha katiba, na kwa vile anatenda kwa nia njema, in good faith, wasaidizi wake hawamshauri, na hili hata mimi simlaumu kwa sababu yeye sio mwanasheria ila ni ajabu kwa wanasheria wanaojua rais anavunja katiba lakini wanamnyamazia, hata katika uteuzi wa wabunge wa kuteuliwa, unazingatia gender balance, rais Magufuli ameteua wabunge 6 wanaume, kinyume cha katiba, itabidi kumtengua mbunge mmoja. Gwiji wa Sheria na Katiba, Prof. Issa Shivji, Agoma Kuzungumzia Dhana ya Udikiteta/Uvunjifu Katiba!.

Hata suala la Makonda, kwa vile ni yeye ndiye aliyemteua Makonda, rais anaamini hakuna yoyote mwenye uwezo wa kumshauri kumtengua, ni bahati nzuri sana, Taifa letu halina wanasheria machachari, tungekuwa nao, na wakathibitisha kuwa ni kweli Makonda ni mhalifu, then hata rais Magufuli ampende vipi, mhalifu hapaswi kushika ofisi ya umma, hivyo sio tuu wangeweza kumlazimisha rais Magufuli kumtengua Makonda, bali hata yeye rais angeweza kutolewa kwenye urais na kumtoa hapo Ikulu kwa kutumia ibara ile ya 46 ya Katiba yetu, ikithibishwa amekiuka katiba!.

Sababu ya msingi ya kumtoa Makonda, ni iwapo tuu itathibitishwa beyond a reasonable doubt kuwa ni kweli jina halisi la Paul Cheriatian Makonda ni Daudi Albert Bashite, na ni kweli alifoji vyeti na akafanya udanganyifu kwa kutumia vyeti vya Paul Chistian kujipatia elimu, ajira hadi uteuzi, then kwa kutumia vipengele fulani vya kisheria, kwa kupeleka shauri mahakamani, then Mahakama inamlazimisha Paul Makonda kutumia majina yake halisi ya Daudi Albert Bashite, Nyegezi, Mbegani na Muccobs zita scrap down vyeti vyake na rais Magufuli atalazimishwa na sheria kutengua uteuzi wa Paul Christian Makonda na kushitakiwa kwa jinai.

Kitu ambapo rais Magufuli anaweza kukifanya kumuokoa Makonda kwa vile anampenda sana kwa uchapa kazi wake, hata kama amefoji vyeti, ameiba jina na kufanya udanganyifu, kwa vile rais anayo kinga ya kutokushitakiwa, anaweza kummegea kidogo Makonda hiyo kinga yake ya kutokushitakiwa, hivyo kumkingia Makonda na mashitaka ya jinai ya kufoji na kufanya udanganyifu, lakini jina la wizi lazima livuliwe hivyo lazima atengue uteuzi wa Paul Makonda kama RC wa Da es Salaam na papo hapo kumteua Daudi Albert Bashite kuwa mkuu mpya wa mkoa wa Da es Salaam na kuendelea kuchapa kazi.
Je, wajua suala vyeti vya Bashite, linaweza kabisa kumng'oa Rais Magufuli pale Ikulu?.

Ipo mifano ya rais kufukuza mtu kazi, mahakama ikaamuru arudi kazini.
Kuna mtu alitiwa kizuizini kwa amri ya rais, mahakama ikamtoa.
Kuna ile kesi ya Bawata etc.

NB. Katiba yetu imempa rais wetu mamlaka ya kuwa kila kitu endapo tuu atatangaza hali ya hatari, hili likifanyika, hapo ni kweli rais ndio anakuwa kila kitu maana katiba huwekwa pembeni na hili likitokea hata JF itabidi iwe likizo!.

Kuna vitu kibao rais wetu Magufuli alitangaza kuwa atafanya, wakati akitangaza, yeye alitangaza kwa mamlaka kabisa akijidhania anayo mamlaka hayo na uwezo huo, lakini kiukweli kabisa, kumbe kisheria hana mamlaka hayo wala hana uwezo huo na hapa chini ni baadhi ya mifano hiyo, ila katiba, sheria, taratibu na kanuni zinaweza kupindishwa na rais Magufuli akafanya kila kitu!.

  1. Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote
  2. Rais amefanya mambo mengi tuu kinyume cha katiba lakini kwa vile amefanya kwa nia njema, hakuna aliyelalamika.
  3. Udikiteta ni Dhana Tuu or ni Real?. "Lets Call A Spade A Spade!"Dikiteta ni Mtu Mwenye Tabia Hizi!".
  4. Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'!
  5. Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki 'Separation of Powers'?
  6. Watetezi Wa Kweli wa Haki za Binaadamu Tanzania ni Kina Nani?!, Jee JF Tumo?!.
  7. Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The Right Time, And Doing It Right, Or ?!
  8. Udikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka Ukweli!. Dawa ya Uongo ni Ukweli.
  9. Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize Binti huyu, ana hoja ya Msingi!
  10. Kutoonyesha Hisia/Huruma wala pole za sauti si Udikteta bali ni Ushujaa wa Kijeshi!
  11. Mawaziri Watakaolalamikia OC Ndogo!, Waache Kazi!. Ni Kauli ya Kujenga Nidhamu au Udikiteta Tuu?!.
  12. Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais Magufuli!, Alimaanisha Nini?!.
  13. Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?
Paskali
 
Pascal Mayalla,

Katika dunia hii tunayopita, siku za mnafiki uwaga ni fupi sana.
Leo hii unafiki wanu na huyo mzee mwanakijiji umefikia mwisho. Nyie ndio mlikuwa mnampamba huyu jamaa kwa kutuaminisha ni bahati au zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Muumba.
Sasa leo kiko wapi? Punguzeni unafiki na msiweke tonge mbele sana.
 
The big problem with that so called @Mwanakijiji is inflated ego.

Hadi anatupangia vitu vya kuongelea kama jamii... Kwamba tuongelee mambo ya maji vijini... Who gave him that right in the first place?

Dunia ya mahaba na hadaa....
Hata wewe Paschal ulishadadia sana haya mambo.
Chicken have come home to roost, keep quite.
 
Umeandika huku tunajua unataka Mh. Makonda aondolewe

Umeobyesha kuwa jana ulipigwa mshtuko mkubwa kama wenzako

Humu unajitia ujanja kuandika kijanja, ila wengine sisi tunayaona kupita maneno yako hata ukoroge vipi.

Mtanyooka tu, umevizia kutumia mada ya mtu ili mfunze watu wavunje amani nchini. Hii imeanza masaa yaliyopita, na wewe naona umo.

Mmmmmh

Mnatumwa wote wakati moja au mnapewaje tasks za kufanya mitandaoni?

JPM oyeeeeeee
Makonda oyeeeeee
 
Hii nguvu tunayoitumia kwenye hili swala la Makonda tungeiwekeza kwenye Kilimo leo hii tungekuwa na foodbasket wa Dunia, au hata tu kwenye kupigania Rasilimali zetu zinazopokwa kila uchawao na wageni!

Sisi Waafrika ni watu wavivu sana!


Sasa na wewe unayeshinda hapa asubuhi mpaka usiku kumsafisha makonda, na wewe ungeelekeza nguvu zako kwenye kilimo ungekuwa wapi??
 
Hii nguvu tunayoitumia kwenye hili swala la Makonda tungeiwekeza kwenye Kilimo leo hii tungekuwa na foodbasket wa Dunia, au hata tu kwenye kupigania Rasilimali zetu zinazopokwa kila uchawao na wageni!

Sisi Waafrika ni watu wavivu sana!
Sio kila mtu ni mkulima

Wanaotakiwa kuongoza kupigania rasilimali wanakataa kuambiwa
 
Wanabodi,
Hili ni bandiko la kumjibu mwana JF mwenzetu, Mkuu Mzee Mwanakijiji, aliyesema rais Magufuli ni Alfa na Omega, hapa mimi natofautiana naye kuwa rais Magufuli sio Alfa na Omega, Alfa na Omega ni Mungu tuu pekee, rais Magufuli sio Mungu, ni mkuu wa nchi yetu, lakini yeye sio kila kitu, hivyo hawezi kuwa Alfa na Omega.

Tukiacha yaliyo ya Kimungu, tukija kwa yaliyo ya Kaisari na kwenye utawala wa nchi, pia rais sio Alfa na Omega, bali katiba ya nchi ndio kila kitu, rais yuko chini ya katiba. Kitendo chá rais Magufuli kuikanyaga katiba na kuachwa tuu hivi hivi akiangaliwa, ndiko kumepelekea baadhi yetu kumuona yeye ndio kila kitu hadi kumfananisha na Alfa na Omega.
Hata mimi jana nilimsikia rais Magufuli alipozungumza kuwa kwenye mambo ya uteuzi, yeye ndio kila kitu, hakuna yoyote anayeweza kumpangia kitu, hii sii kweli, kiukweli rais sio kila kitu, bali katiba ndio kila kitu hivyo kuna vitu hata rais anapangiwa na kulazimishwa avifanye atake asitake, apende asipende.

Hii maana yake kuna vitu ambavyo rais anavifanya at his discretion kwa mapenzi yake na kuna vitu anatakiwa kuvifanya not at his discretion bali kwa lazima kwa mujibu wa katiba.

Kwanza sote tunakubaliana kuwa Magufuli ndiye rais wetu, ndio mamlaka kuu kupita zote za kiutawala nchini mwetu mwenye nguvu kubwa hivyo anapaswa kuheshimiwa, lakini sio kuogopewa au kuabudiwa as if yeye ni Mungu!. Hili nimelizungumza hapa Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Rais ana powers, ila sio absolute powers, yuko chini ya katiba, katiba ndio kila kitu, hata rais akimess, anaondoshwa!. Kuhusu mamlaka ya rais kumteua yoyote, nimeieleza hapa. Je, wajua Rais aweza kuteua yeyote hata darasa la saba?. Teuzi hizi hazihojiwi popote na yeyote!

Magufuli japo ni rais wetu na yeye ni binadamu kama sisi na sio malaika, hivyo ana mapungufu yake, na moja ya mapungufu yake makubwa ni hili kwa vile yeye ndio rais wetu, hivyo anajidhania yeye ndio kila kitu. Lakini kwa bahati mbaya sana, japo ameapa kuilinda katiba, lakini imetokea kuwa kumbe Magufuli haijui hata hiyo katiba yenyewe aliyoapa kulinda ndio maana baadhi ya maamuzi yake yanakwenda kinyume cha katiba, kwake it's OK kwa vile hajui atendalo ni kinyume cha katiba, na anatenda kwa nia njema, na hili hata mimi simlaumu kwa sababu yeye sio mwanasheria ila ni ajabu kwa wanasheria wanaojua rais anavunja katiba lakini wanamnyamazia Gwiji wa Sheria na Katiba, Prof. Issa Shivji, Agoma Kuzungumzia Dhana ya Udikiteta/Uvunjifu Katiba!

Kwa vile ni yeye ndiye aliyemteua Makonda, anaamini hakuna yoyote mwenye uwezo wa kumtoa huyo Makonda, kiukweli sio tuu Watanzania wakiamua wanaweza kumtoa huyo Makonda, bali hata yeye ampende vipi Makonda, bali Watanzania tukiamua kwa kauli moja kuwa hatumtaki Makonda kwa sababu za msingi ambazo ni justifiable, sio tuu tunamtoa huyo Makonda wake, bali tunauwezo wa kumtoa hata yeye Magufuli na Makonda wake kwa mujibu wa katiba mradi tuu ziwepo sababu za msingi.

Sababu ya msingi ya kumtoa Makonda, ni iwapo ikithibitika kuwa ni kweli jina halisi la Makonda ni Daudi Bashite, ni kweli alifoji vyeti na akafanya udanganyifu kwa kutumia vyeti vya Paul Chistian kujipatia elimu, ajira hadi uteuzi, then kwa kutumia vipengele fulani vya kisheria, kwa kupeleka shauri mahakamani, then Mahakama inamlazimisha rais Magufuli kutengua uteuzi wa Makonda kwa lazima kwa kutumia nguvu za kisheia, hata Magufuli ampende vipi Makonda ni lazima amtengue!.

Kitu ambapo Magufuli anaweza kukifanya kumuokoa Makonda wake, kwa vile anampenda sana kwa uchapa kazi wake, na rais anayo kinga ya kutokushitakiwa, anaweza kummegea kidogo Makonda hiyo kinga yake ya kutokushitakiwa, hivyo kumkingia kushitakiwa kwa jinai ya kufoji na kufanya udanganyifu, lakini jina la wizi lazima livuliwe hivyo lazima atengue uteuzi wa Paul Makonda kama RC wa Da es Salaam na papo hapo kumteua Daudi Albet Bashite kuwa mkuu mpya wa mkoa wa Da es Salaam na kuendelea kuchapa kazi.

Nawaomba mnipe muda niwatafutie vifungu vya katiba na sheria vinavyoonyesha kuwa rais sio kila kitu bali katiba ndio kila kitu, na rais anaweza kufanya maamuzi fulani na mahakama ikayatengua maamuzi hayo kwa kutumia vipengele vinavyoitwa writs or prerogative ordes kama prohibition, certiorari, mandamus, harbea copus na quo warranto ambapo rais analazimishwa kufanya kitu fulani kwa lazima, apende au asipende na akigoma, Bunge linaitishwa na kumfukuza kazi!. Hili lipo, sheria hizi zipo, ila sisi hapa Tanzania hatujawahi kuitumia, lakini anamuondoa madarakani mteule yoyote wa rais hata rais ampende vipi. Kwa vile sheria zetu tumezirithi kutoka India Para materiale, kuna sheria nyingi tunazo lakini hatujazitumia, kwa vile mimi sio practicing lawyer, kuna sheria zipo tuu kama just persuasive tuu, with time tutawathibitishia kuwa rais Magufuli sio kila kitu, bali katiba ndio kila kitu!.
Kuna mtu alifukuzwa kazi na rais, mahakama ikaamuru arudi kazini.
Kuna mtu alitiwa kizuizini kwa amri ya rais, mahakama ikamtoa.
Kuna ile kesi ya Bawata etc.

NB. Katiba yetu imempa rais wetu mamlaka ya kuwa kila kitu endapo tuu atatangaza hali ya hatari, hili likifanyika, hapo ni kweli rais ndio anakuwa kila kitu maana katiba huwekwa pembeni!.

Kuna vitu kibao rais wetu Magufuli alitangaza kuwa atafanya, wakati akitangaza, yeye alitangaza kwa mamlaka kabisa akijidhania anao uwezo huo, au mamlaka hayo lakini kiukweli kabisa, kuna vitu rais anatangaza kuwa anao uwezo lakini hana uwezo huo na mifano
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote

Rais amefanya mambo mengi tuu kinyume cha katiba lakini kwa vile amefanya kwa nia njema, hakuna aliyelalamika.

Udikiteta ni Dhana Tuu or ni Real?. "Lets Call A Spade A Spade!"Dikiteta ni Mtu Mwenye Tabia Hizi!".

Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'!
Paskali

Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki 'Separation of Powers'?

Watetezi Wa Kweli wa Haki za Binaadamu Tanzania ni Kina Nani?!, Jee JF Tumo?!.

Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The Right Time, And Doing It Right, Or ?!

Udikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka Ukweli!. Dawa ya Uongo ni Ukweli.

Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize Binti huyu, ana hoja ya Msingi!

Kutoonyesha Hisia/Huruma wala pole za sauti si Udikteta bali ni Ushujaa wa Kijeshi!

Mawaziri Watakaolalamikia OC Ndogo!, Waache Kazi!. Ni Kauli ya Kujenga Nidhamu au Udikiteta Tuu?!.

Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais Magufuli!, Alimaanisha Nini?!.

Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Paskali

Shemeji ulienda kupiga KURA TLS??Maana wakati mwingine naona kama unafanya kama Boss wenu wa TLS anavyotaka
 
Hii nguvu tunayoitumia kwenye hili swala la Makonda tungeiwekeza kwenye Kilimo leo hii tungekuwa na foodbasket wa Dunia, au hata tu kwenye kupigania Rasilimali zetu zinazopokwa kila uchawao na wageni!

Sisi Waafrika ni watu wavivu sana!

Ukija kuamka wenzio tumesharudi safari
 
Kwenye zile nyuzi zako za siku za nyuma niliwahi kusema hivi, "miongoni mwa waandishi ninao waheshimu sana hapa nchini, PAscal wewe ni mmoja wao" na hata kwenye uzi wako mwingine nikaongeza kwamba still nakuheshimu kama mwandishi makini ingawa kwenye hizo nyuzi zako zote sikua nakuunga mkono kwenye ule msimamo wako, now brother you are coming back from where you were; kwa mwenendo hu anaokwenda nao mdogo wako mhe rais wa mkoa wa Dar, je bado unaamini Gwajima alimsingizia kama anacho cheti au hana!?
 
Back
Top Bottom