Kakobe, Mtikila wapambana ubalozi wa Marekani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kakobe, Mtikila wapambana ubalozi wa Marekani

Discussion in 'Celebrities Forum' started by EMT, Jul 11, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  MCHUNGAJI Christopher Mtikila andaiwa kwamba amevuruga mpango wa kwenda nchini Marekani wa Askofu Zachary Kakobe wa Kanisa la Full Gaspel Bible Fellowship (FGBF). Mtikila anadaiwa kuuomba Ubalozi wa Marekani nchini kumnyima viza kiongozi huyo mkuu wa FGBF kwa maelezo kwamba ana kesi ya kujibu mahakamani. Kupitia taasisi ya Liberty International Foundation, Mchungaji Mtikila ameuandikia barua ubalozi wa Marekani nchini, akiutaka usimruhusu Kakobe kwenda nchini humo, kwa kuwa ana kesi ya kujibu.


  Akiwa ameorodhesha tuhuma mbalimbali anazoeleza kuwa zinamkabili Askofu Kakobe katika kesi hiyo, Mtikila amesema, mpango wake wa kwenda Marekani, umelenga kuikimbia kesi hiyo. "Tunaomba Askofu Kakobe asiruhusiwe kwenda Marekani hadi hapo kesi yake Namba 78 ya mwaka 2011 iliyofunguliwa kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania itakapomalizika," alisema Mtikila katika barua hiyo ya Julai 5 mwaka huu.

  Mtikila ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa taasisi hiyo ya haki za binadamu, amefafanua kuwa Askofu Kakobe ameshtakiwa na wachungaji watatu wa kanisa lake la FGBF ambao ni Dezedelius Patrick, Angelo Mutasingwa na Benedict Kaduma. "Anahusishwa na matumizi mabaya ya fedha za kanisa hilo zinazofikia Sh14 bilioni," alisema Mtikila katika barua hiyo na kuongeza: “Tunakuandikia kuomba mamlaka zako husika kumnyima Zacharia (Zachary) Kakobe kibali cha kuingia nchini kwako hadi hapo kesi dhidi yake iliyofunguliwa Mahakama Kuu itakapoamuliwa.”

  Katika barua hiyo, Mtikila ameueleza ubalozi wa Marekani kuwa Askofu Kakobe anataka kuimbikia kesi hiyo na kuhamia katika mji wa Boston, ambako ataishi na kuendesha taasisi yake inayojulikana kama Bishop Zachariah Kakobe International Ministry. Mwananchi lilimtafuta Askofu Kakobe juzi na jana ili kufahamu undani wa safari yake ya kwenda nchini Marekani, lakini simu yake ilikuwa ikiita muda wote bila kupata majibu. Baadaye gazeti hili lilimpata msadizi wake ambaye alisema kwamba askofu huyo asingeweza kuzungumza kutokana na kwamba alikuwa kwenye huduma.

  Kakobe, Mtikila wapambana ubalozi wa Marekani
   
 2. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Wachungaji waliomaliza bible, wameamua kuperuzi ya dunia.
   
 3. emmanuel1976

  emmanuel1976 JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kakobe hawamwezi hawa...wakamwulize Ngereja! Hivi..Kakobe ametafunaje 14b na juzi tu zaidi ya maaskofu na wachungaji 400 wamempitisha kuwa Askofu mkuu baada ya kukosa mpinzani? Majungu tui. Kwanza nasikia hawa wanaomshitaki Kakobe, walifukuzwa miaka kadhaa baada ya kuasi sasa watamnenea mema Kakobe?
   
 4. n

  njija Senior Member

  #4
  Jul 12, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Yaani nina mwonea huruma MTIKILA NA HAO WACHUNGAJI WANAO HANGAIKA Juu ya ASKOFU KAKOBE, kwani nilipokuwa katika ibada hiyo maaskofu na wachungaji walisema wameamua kumpitisha kuwa Askofu wao milele kuonyesha kuwa wana mkubali na kumheshimu, na watu wanao mpiga vita wakaanzishe makanisa yao nao wawe MAASKOFU,SIKUAMINI MASIKIO YANGU JINSI WALIVYO ONYESHA UPENDO WAO JUU YA ASKOFU KAKOBE,NA mimi naona hao wachungaji wanapoteza muda wao tu! ila kwa Mtikila yeye amesha zoea maisha ya mahakamani.
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Serikali hii ukiisakama utakipata cha moto, kakobe alikuwa msitari wa mbele kuisakama kipindicha kampeni na kufikia kutoa cd iliyokuwa inahamasisha watu kwenda kupiga kura na huku akiiponda serikali ya ccm kwa propaganda zake za kijinga...sasa naoma wameanza kumfanyia kazi...
   
 6. s

  smirna Senior Member

  #6
  Jul 14, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mtikila ana matatizo makubwa. He is a slow learner. Hajifunzi kwa makosa yake. Ikiwa kazi imetoka kwa Mungu, hakuna awezaye kuizuia (ISAYA 43:13; MATENDO 5:34-39). Kwa taarifa yenu wanaJF; mwaka 1999, Mtikila huyuhuyu alikwenda Ubalozi wa Denmark ili kumzuia Kakobe asiende Denmark, kuhubiri Injili huko. Gazeti la Alasiri, nyakati hizo liliandika habari hiyo (nakala ninayo).
  Huko Ubalozi wa Denmark, alifukuzwa kama mbwa, na kuambiwa hana haki ya kuwazuia watu wengine kusafiri. Kakobe alikwenda Denmark, na kufanya Mkutano wa Injili huko Copenhagen, uliokuwa na mafanikio makubwa; na kurudi. Mtikila aliaibika vilivyo, lakini hakomi. Safari hii, anatafuta aibu nyingine. Yeye ni nani kumzuia mtu kusafiri? Kama angepeleka Ubalozi wa Marekani, amri au zuio la Mahakama, hapo inge make sense. Lakini siyo barua yake. Eti Kakobe amehamishia mabilioni Marekani bila nchi ile kuwa na taarifa! Marekani siyo Bongo, bwana; tunaijua Marekani. This is utter nonsense. Wadanganye wajinga wako unaowatapeli!
  Mtikila, kushindana na kazi za Mungu kumekuletea laana. Hivi sasa akili yako siyo timamu, unahitaji msaada wa Psychiatrist! Ni juzi tu umeshindana na Mtumishi wa Mungu Mulilege Mkombo. Siku chache tu zilizopita patina wako Rwakatare uliyekuwa naye katika kikao dhidi ya Kakobe, naye umempeleka mahakamani unamdai bilioni 3. Shame on u!
  Kibali cha siasa ulichokuwa nacho wakati wa sera zako za ma*********, chote kimeondoka kwako. Umekuwa Ikabodi! Ulilishikia bango suala la Marehemu Wangwe, huko Tarime, ukafikiri utapata support yao, matokeo yake hukupata hata mtu mmoja wa kumhutubia. Kinyume chake ukiwa kando ya barabara, unajihutubia mwenyewe, ukashitukia jiwe linakupiga kichwani; ukarudi na maplasta kichwa chote. Kidogo tu wana Tarime wakuue!
  Mtu ambaye gari lako lilisukumwa na wana-Chuo Kikuu, enzi hizo unawika kisiasa, leo umekuwa a laughing stock! DP yako, ndiyo chama cha mwisho kabisa katika vyama vya siasa. Nobody is interested to join DP, DP is dead! Hii ni laana ya Kaini, aliyemwua Habili aliyempendeza Mungu. Umepata laana hii kwa kushindana na kazi ya Mungu. Mwache Kakobe alone, na wewe tuonyeshe kazi za Kanisa lako, tuzione!
   
 7. Esperance

  Esperance JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Laana za watumishi tu hapa zinamwagika.
   
 8. w

  werawera Senior Member

  #8
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Huyu Mtikila duh... Atalaanika sana.. anatakiwa kuomba radhi na kumrudia Mwenyezi Mungu.
   
 9. z

  zamlock JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  mimi namuunga mtikila kutakuwa na jambo siyi bure ni swala la kakobe kupitishwa na wachunguji aiwezi kuwa sababu ya kakobe kuwa msafi, cha msingi hapa nikujua kwa undani zaidi kama kwa juu ya hili smtikila anamshutumu basi atakuwa anajua hizo ppesa zimeliwa vp hao wote ni kitu kimoja wanajuanawa
   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu mtikila anafanya kazi gani inayomwingizia kipato? Maana mda mwingi anatumia kufatilia na kufungua kesi tu!!
   
 11. u

  ureni JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mtikila anatumiwa na vigogo katika kufanikisha mambo yao.
   
 12. m

  mja JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 311
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nadhani hawajamaliza, ilispokuwa wameshindwa kuielewa ndo maana wanajaribu kuperuzi ya dunia kutafuta wanachojua wapo...Mungu awasamehe sana, na ianonejana si "wachungaji" manake wanaacha kondoo wao na kualumbana , who will look after the kondoo
   
 13. J

  JayM Member

  #13
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Du mwana Jr umetoa dozi ya ukweli, laiti anapata hii massege yamkini atabadilika.
   
 14. J

  JayM Member

  #14
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Mtikila kwa Kakobe umechemsha, huyu Askofu maisha yake ameyatoa kumtumikia Mungu kweli kweli, hivi mwana Jr tujiulize katika pita pita yako mlimani city ulishawahi kukutana naye kama watu wengine wakiwa bize na maisha ya shopping like mtikila mwenyewe. sasa mtikila anadhani atafanikiwa kwa jaribio lake la zaidi ya mara mbili kumzuia Kakobe asiende malekani kuhubiri?
   
 15. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Poor Mtikila
  Pesa za mlungura zitamchoma siku moja.
   
 16. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #16
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Kuna waumini wa dini mbali mbali acha tu ya Kikristo waumini huwasikiliza Regional leaders as if wao ndio GODs... wengine wameharibu system yoote ya personal life in the pretense of the Church OR Mosque... cha ajabu vitabu vyoote viwili vinasema sali na utafute...

  I hope walo katika hilo kundi waone kua this is evidence enough kua hata Viongozi wao wa dini are only human...
   
 17. M

  Marytina JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  mtikila hana dini
   
 18. EBENEZA MT

  EBENEZA MT JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 264
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mtikila anahitaji maombi ya ukombozi.
   
 19. sekulu

  sekulu JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  kuna mungu wanaemtaja,sio mungu wa yakobo wala ibrahim.
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mtikila anataka mgao wake tu kwa Kakobe na Kakobe kamgomea. Hapo sasa.
   
Loading...