Kaka unafanya “Sikirabu''?!

Nazichukia sana hizi salon za sasa hivi, tulishazoe ukinyoa unapakwa after shave yako unatambaa. Mdau wewe km mie huwa sifanyi hayo madudu yao sijui scrub, kuna siku nilifanyiwa like 4 yrs ago ngozi ya usoni after 4 days ikaanza banduka km ya nyoka. Ukiwakatalia utaona wananuna km wamekutafutia hiyo pesa yako, ikifika wakati Wa kunyoa huwa mpaka nakosa raha nikiwakumbuka hao Wa Dada saluni. Halafu Mara nyingi hunyoa jioni nnapotoka kazini nikijua baada ya halo naenda kuoga lkn hawa ma Dada Wa saluni no kero kubea saaana
 
Anachosema mlata mada ni kweli kabisa, ukikataa hizo huduma zao zingine wanakununia kweli mimi binafsi huwa sipendi kushikwa na hao wadada
 
Tutawaanzishia movement for change(M4C) wakizidi hahahaha
 
Hawa wadada wa barber shops wanazingua sana!

Akikuuliza unafanya scrub ukamwambia hufanyi… Na hizo huduma zao nyingine (mimi sio muumini wa hizo huduma) ukazipangua zote , Sana sana ukataka uoshwe tuu. Utaoshwa kwa hasira na minuno juu!

Kwani lazima!! Wengine waume za watu hawapendi kushikwashikwa na watu tofauti na wake zao! Dawa yao naichemsha maana naona haka katabia kamezidi sasa!

Yaani imenitokea Zaidi ya mara moja mtu unaoshwa kwa hasira as if umenyoa bure!!!
Hahahaha ni kweli kabisa mi mwenyewe huzipangua kabisa lazima wanune kabisa na wanakuona mshamba.. .
 
Utawauwa njaa wenzako... Hata mimi huwa nachukia vile wanavyolazimisha ununue huduma flani mathalani hiyo scrub...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom