Kaka/Dada soma kwa makini post hii

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Wasichana wanne waliingia katika mkutano wakiwa wamevaa nguo mapaja yakiwa nje. Kabla ya mkutano kuanza mzee mmoja alikuwa ndiye mwenyekiti wa mkutano huo.

Mzee huyo aliwaangalia kwa makini wasichana hao kicha akawakaribisha kwenye mkutano huo.

Baada ya hapo mzee huyo aliwaambia binti zangu kila kitu cha thamani Mwenyezi Mungu amekiumba lkn huwa kimefichwa kiasi kwamba ni vigumu sana kukiona.

Mzee huyo aliwaambia Almasi huwa iko chini ya ardhi imefichwa na kulindwa vzr na miamba. Pia samaki huwa zipo chini ya maji sio rahisi kuziona juu ya maji.

Mzee huyo aliwaangalia tena alionekana kuchukizwa sana jinsi wasichana hao walivyo vaa. Mzee huyo aliwaambia wasichana hao miili yenu ni ya kipekee na ya thamani sana.

Nyie ni thamani mno kuliko Almasi au dhahabu, mnatakiwa muwe na Coverd. Mzee huyo alisema kama mtaficha miili yenu kama madini yaliyofichwa chini ya ardhi yakilindwa na miamba.

Basi kampuni kubwa ya uchimbaji madini yenye vifaa vya kisasa vya uchimbaji madini watakuja kwako na kufanyiwa utafiti...

Ni ( MUME BORA ) itawasiliana na serikali yako yaani ( FAMILIA YAKO) itatia saini mkataba wa kitaalam yaani (NDOA ) na kuchimba madini yako kitalaam yaani (NDOA HALALI )

Lkn kama mtaacha madini yenu nje bila kulindwa au kufichwa mtawavutia wachimbaji madini wasio waaminifu yaani ( WANAUME WAONGO )

Kuja kuchimba hivyo kila mtu atakuja kuchimba na kupata alichokuwa akikitaka na kuondoka baada ya muda mfupi. Madini hayatakuwepo yatabaki mashimo.

Mzee huyo alisema "Ificheni miili yenu ili muwavutie wachimbaji madini walio waaminifu na sio wapita njia.

SITARA YA MWANAMKE NI HIJABU NA NDOA.

Jihifadhi Uhifadhike👚

"Jifunze Dini Yako upate kumtambua Mola wako".
 
Unacompare binadamu mwenye self interests na mahitaji na matamanio na hisia dhidi ya jiwe?
 
Hakuna lolote ktk hayo. Vinginevyo wangezaliwa na nguo ndefu. Adamu na Hawa waliishi kama walivyozaliwa, miaka ikaenda wakaanza kuvaa magome ya miti, lakini sehemu kubwa ya mwili ikiwa wazi.
 
Hakuna lolote ktk hayo. Vinginevyo wangezaliwa na nguo ndefu. Adamu na Hawa waliishi kama walivyozaliwa,miaka ikaenda wakaanza kuvaa magome ya miti,lakini sehemu kubwa ya mwili ikiwa wazi.
Adamu na eva.
Hivi ni kweli et
 
Kwahiyo huyo Mzee hakuwa na agenda za huo uliouita mkutano akaamua kuokoteza!

Basi mkumbushe haki za wachimbaji wadogo wadogo.🌚
 
Embu muulize huyo mzee, Kwahiyo yakibaki mashimo ndo zile nyimbo za vibamia zinaanza au huwa zinaanzaga mapema?
 
Back
Top Bottom