john achila mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 131
- 268
Kaini alipata wapi mwanamke wa kuoa?
Kaini, baada ya kumuua ndugu yake Abeli, alikimbilia katika nchi ya Nodi (Mwanzo 4:16).
Nodi (Kiebrania) maana yake ni kutanga-tanga. Hivyo, Kaini alikwenda nchi isiyojulikana.
Je, huko alipatia wapi mke na kuzaa naye watoto?
Ukisoma kitabu cha Mwanzo 5:1-5, utaona:
“1Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;
2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
4 Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, AKAZAA WANA, WAUME NA WAKE
5 Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.”
Kwenye mstari huo wa 4, utaona kuwa kumbe mbali ya Kaini na Abeli kuzaliwa na Adamu, kulikuwa na wana wengine wa kike na wa kiume waliokuja kuzaliwa kwenye familia yao. Ndiyo huko huko, Kaini alipojitwalia mke, yaani kutoka ndani ya familia hiyo hiyo ya Adamu.
Swali linakuja kuwa, kama KAINI alitwaa mke ambaye alizaliwa na Adamu na Hawa, ambao ni wazazi wake, hiyo ina maana kuwa alimuoa dada yake. Je, ni halali kumuoa mwanamke ambaye ni dada yangu wa damu?
Kumbuka kuwa hata Adamu mwenyewe hakwenda kumtwaa mke kutoka kwenye familia nyingine, bali kutoka katika ubavu wake mwenyewe. Hivyo, kama ni undugu, basi Adamu na Hawa wana undugu mkubwa zaidi ya dada na kaka.
Kumbuka pia kuwa hata Ibrahim alioa dada yake wa baba mmoja, yaani mtoto wa mama mwingine kwa baba yake (Mwanzo 20:12). Kwa wakati huo, Mungu aliruhusu iwe hivyo mwanzoni, kwa ajili ya uzazi, ili watu waongezeke.
Lakini baadaye Mungu alitoa maagizo kuwa ni makosa mtu kutwaa ndugu wake wa karibu na kumfanya kuwa mke wake.
Hebu thibitisha hilo kupitia kitabu cha Mambo ya Walawi 18:
6 “Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi Bwana”.
Na pia mstari wa 9 unasema:
9″ Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue”.
Kwa hiyo, mbali na Kaini na Abeli kuzaliwa na Adamu, kulikuwa na wana wengine wa kike na wa kiume waliokuja kuzaliwa kwenye familia yao. Ndiyo huko huko Kaini alipojitwalia mke, yaani kutoka ndani ya familia hiyo hiyo ya Adamu. Kwa wakati huo, Mungu aliruhusu hiyo hali, ili watu waongezeke.
Baadaye, Mungu alitoa maagizo kuwa ni makosa mtu kutwaa ndugu wake wa karibu na kumfanya kuwa mke wake.
Hivyo, kwa sasa, ni machukizo kuoa ndugu yako ye yote yule wa karibu.