Kahama VS Njombe/Mafinga

Kahama VS Njombe/Mafinga

IMG-20231022-WA0027.jpg
 
DP WORLD YAFUATA FURSA ZA UWEKEZAJI MKOANI NJOMBE

Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya DP World ya Dubai Sultan Ahmed bin Sulayem mara baada ya kusaini Mkataba wa Uendeshaji wa Gati namba 4 mpaka 7 za Bandari ya Dar es Salaam Jana Oktoba 22,2023 alianza safari kwenda Mkoa wa Njombe kwa lengo la kutazama fursa mbalimbali za uwekezaji.

Leo Oktoba 23, 2023 amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Kissa Gwakisa na viongozi wengine wamekutana na kufanya mazungumzo katika Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Njombe.

Pamoja na Mambo mengine wamejadili kuja kufanya uwekezaji kwenye eneo la Utalii,Ujenzi wa Hotel kubwa yenye hadhi ya nyota 5, Kilimo cha chai na mazao ya Miti pamoja na Uwekezaji mkubwa kwenye eneo la Madini ya Chuma na Makaa ya Mawe.

"Ninamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kufungua fursa za kiuwekezaji nchini kwetu Tanzania, Leo hii muwekezaji mkubwa katika bandari yetu ya Tanzania amefika Mkoani Njombe akiongozana na mfanyabiashara mkubwa kwenye Mkoa wetu akitokea nchini kenya Bw. na ameahidi kuwa atafanya uwekezaji kwenye eneo la Ujenzi wa Hotel kubwa za Kitali, lakini pia tumetumia nafasi hii kama Mkoa kumkaribisha kwenye uwekezaji kwenye eneo la Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Njombe". Alisema Mhe. Mtaka
 
IDOGLAVU hizi ni glavu ambazo zimeanza kuzalishwa makambako mtaa msd INDUSTRY park idofi pia wanaanza kuzalisha na condom viwanda Vingine kazi bado inaendelea
1698198990529.jpg
1698198974920.jpg
1698198959796.jpg
1698198969710.jpg
1698198378117.jpg
1698198949103.jpg
1696737622411.jpg
 
JAPAN KUWEKEZA KATIKA MRADI WA HEWA UKAA NJOMBE

Serikali ya Japan inatarajia kuwekezaji katika mradi wa uvunaji hewa ukaa mkoani #
#Njombe nchini Tanzania.

Hayo yamezungumzwa na Yasushi Misawa Balozi wa Japan nchini Tanzania katika ziara yake ya siku moja mkoani Njombe Oktoba 25,2023 ambapo ameeleza kuvutiwa na hali ya hewa ya Njombe na kuahidi kuweka nguvu zaidi katika miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo mradi wa hewa ukaa.

Miradi mingine ambayo Japan itawekeza mkoani humo ni katika sekta ya afya, elimu na mazingira.

#kingsfmradio #jisikiemfalme #kingsfmupdates #nipotayari
 
Back
Top Bottom