Kahama VS Njombe/Mafinga

Kahama VS Njombe/Mafinga

Walituchelewesha sana atimaye mradi utaanza utekelezaji lakini sijaona miradi ya masoko, kingo za mito na stendi, je miradi itaanza lini?
Ipo itaanza baadae mwaka ujao au mwisho mwa mwaka huu huu maana mwezi ujao wa 10 wanatangaza zabuni za kuitisha wakandarasi wa Ujenzi.Soko lenu hili hapa 👇
20230923_162028.jpg

Pili naona wamepunguza wingi/urefu wa Barabara
Screenshot_20230923-172020_1.jpg
 
Duh huu mradi naona ni Barabara tu walizo sain stend na masoko hamna
1695486031108.jpg
 
Duh huu mradi naona ni Barabara tu walizo sain stend na masoko hamna
View attachment 2759701
Ndio ni Barabara tuu Kwa package one,masoko na Stand wanatangaza tender mwezi wa 10.

Naona Mwanza CC& Ilemela imependelewa kweli kweli, Barabara tuu ni km 26.8 Bado masoko yanakuja,mitaro inakuja kwenye package ya II
 
TRILIONI 1 KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MIJI NA MAJIJI MCHINI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa, akiongozana na Naibu Waziri Mh. Deogratius J. Ndejembi, pamoja na Mh.Denis Londo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Wabunge, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakandarasi na Wanasheria wa Halmashauri, leo wameshuhudia utiaji saini wa Mradi wa Uboreshaji Miundombinu Ya Miji na Majiji.

Mradi umepanga kuboresha Barabara, Masoko, Vituo vya Mabasi na Daladala, Bustani za Mapumziko na Burudani, Mitaro ya Maji ya Mvua na Vivuko maji katika Miji 45 na Manispaa 16, utakaotekelezwa kwa muda wa miaka (6), wenye thamani ya Dola za Kimarekani Millioni 410 sawa na Tsh. Trilioni 1 za Kitanzania.

Mhe. Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa (TAMISEMI) amesisitiza wakuregenzi wa Halmashauri, Wakandarasi pamoja na watendaji wa serikali kuzingaria weledi, uadilifu na uzalendo katika kuhakikisha fedha zilizotengwa kutekeleza miradi hii zinatumika ipasavyo kama ilivyokusudiwa.
 
MCHENGERWA AWATANGAZIA KIAMA WAKURUGENZI WATAKAOSHINDWA KUTEKELEZA MRADI WA TACTIC

OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Mkurugenzi wa Halmashauri atakayeshindwa kusimamia Mradi wa Uboreshaji wa miundombinu ya Miji ya Tanzania(TACTIC) atachukuliwa hatua za kinidhamu.

Mhe.Mchengerwa ameyasema hayo leo Septemba 23, 2023 kwenye hafla ya kushuhudia utiaji saini Mkataba wa Mradi huo iliyofanyika jijini Dar es salaam.

"Wakurugenzi mna tabia za kukaa na fedha kwenye akaunti bila kutekeleza miradi wengine walikaa nazo mpaka nilivyokuja huku nikasema nitawachukulia hatua ndio wakaanza kukimbizana kutekeleza miradi sasa kwa yeyote atakayekaa na fedha za mradi huu na kuchelewa kuanza utekelezaji wa mradi wa TACTIC nitamchukulia hatua za kinidhamu,"ameonya.

Amesema Mradi huo ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa na serikali ya kuboresha miundombinu ya Barabara, mifereji ya maji ya mvua, stendi za mabasi, masoko, pamoja utunzaji wa Mazingira katika maeneo ya mijini.

"Lengo kuu la mradi wa TACTIC ni kuboresha usimamizi wa ukuaji wa Miji pamoja na kuziwezesha Halmashauri za Miji na Majiji kutoa huduma bora kwa wananchi, mikataba inayosainiwa leo ni sehemu ya miradi itakayotekelezwa kwa Mkopo wa Benki ya Dunia utakaogharimu kiasi cha Dola za Marekani Milioni 410 sawa na Sh.Trilioni moja na inatekelezwa katika Miji 45 nchini,"amesema.

Amebainisha kuwa utekelezaji wa miradi hiyo ni kwa awamu tatu na katika Kundi la kwanza linahusisha Miji 12 ambayo ni Mwanza CC, Mbeya CC, Arusha CC, Dodoma CC, Ilemela MC, Morogoro MC, Kahama MC, Kigoma Ujiji MC, Songea MC, Sumbawanga MC, Tabora MC na Geita TC ambapo utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa Fedha 2023/24.

Katika kundi la Pili, itahusisha Miji 15 ya Tanga CC, Moshi MC, Kibaha TC, Iringa MC, Bukoba MC, Singida MC, Bariadi TC, Shinyanga MC, Musoma MC, Lindi MC, Mpanda MC, Njombe TC, Mtwara Mikindani MC, Babati TC and Njombe TC na utekelezaji wake utaanza mwaka ujao wa Fedha 2024/25.

"Katika kundi la tatu Miji 18 itahusika ambayo ni Kasulu TC, Tunduma TC, Vwawa TC, Ifakara TC, Makambako TC, Masasi TC, Nanyamba TC, Handeni TC, Bagamoyo DC, Mafinga TC, Tarime TC, Chato DC, Bunda TC, Mbinga TC, Mbulu TC, Nzega TC, Kondoa TC and Newala TC ambayo utekelezaji wake utaanza mwaka ujao wa Fedha 2024/25.

Naye, Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Adolf Nduguru amesema mikataba ya ujenzi wa barabara na mitaro inayosainiwa leo katika kundi hilo la kwanza itagharimu Sh. Bilioni 276.18 kwa Miji yote 12 na gharama za usimamizi zitakuwa sh. Bilioni 17.05.

Awali, Mratibu wa mradi huo, Mhandisi Hamprey Kanyenye amesema katika mikataba inayosainiwa leo zitajengwa barabara zenye urefu wa kilometa 147.54 kwa kiwango cha lami nzito, madaraja, vivuko maji, uwekaji wa taa za barabarani zenye kutumia mfumo wa umeme jua, njia za watembea kwa miguu, mitaro ya maji ya mvua kwa pande zote za barabara na mitaro mikubwa ya maji ya mvua yenye urefu wa kilometa 24.66 itajengwa.

&&&&&&
 
Fahamu zaidi kuhusu Mradi wa TACTIC

1. Miundombinu itakayojengwa - Barabara za Lami, Masoko, Vituo vya mabasi na daladala, Bustani za mapumziko na burudani, Mitato ya maji ya mvua na Vivuko vya Maji
2. Jumla ya Halmashauri zitakazofikiwa na Mradi huu ni 46.
3. Halmashauri zitakazonufaika katika Awamu ya Kwanza - Arusha Jiji, Dodoma Jiji, Mbeya Jiji, Mwanza Jiji, Geita Mji, Ilemela Manispaa, Kahama Manispaa, Kigoma Manispaa, Morogoro Manispaa, Songea Manispaa, Sumbawanga Manispaa na Tabora Manispaa
4. Vigezo vya Kupata Wanufaika - Taarifa za idadi ya watu na kiwango cha Ongezeko la watu kwa kila wilaya kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu hivyo makundi ya awamu za utekelezaji yamezingatia Miji yenye idadi kubwa ya watu.
5. Gharama za Mradi - Dola milioni 410 kutoka mkopo wa Benki ya Dunia
 
Ukiangalia nyanda za juu kusini mkoa wa njombe unaenda kuwa na soko la mazao la Kanda ya nyanda za juu kusini ,tpdc wanaweka eneo la kuhifadhi mafuta na kusupply ,na bandari kavu hii ni kutokana na kuzungukwa na maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao mfano mbarali ambayo ukitoka makambako hadi makao makuu ni km 53 wakati ukitoka mbarali hadi mbeya ni zaidi ya km 110 ko mahitaji mengi wanategemea mkoa wa njombe hivo hivo ruvuma ndo maana wameamukutekeleza hata👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Tamko hilo limetolewa leo na Waziri wa Uwekezaji,Biashara na Viwanda, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji katika mkutano wa saba wa baraza la biashara, Mkoa wa Njombe lililofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe , na kuwakutanisha wafanyabiashara wote wa Mkoa wa Njombe ili kusikiliza na kujadili changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
Mhe. Kijaji amesema kuwa Wananchi hao ambao hawakufanyiwa uthamini wa maeneo yao wakati wa uthaminishaji wa awali na kushindwa kulipwa fidia ya maeneo yao , Wizara imeanza kufanyia kazi suala hilo ili kumalizana na wananchi hao , ili pindi wadau wa kujenga soko hilo watakapo patikana ujenzi uanze mara moja bila kikwazo chochote.
Amesema kuwa endapo ujenzi wa soko hilo la Kimataifa na bandari kavu katika Halmashauri ya Mji Makambako ukikamilika,utasaidia kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa katika Mkoa wa Njombe na wananchi wataweza kunufaika na kujipatia maendeleo.
Ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya nchini kusimamia Sekta binafsi katika maeneo yao na kuzilea ili zikue na kutokuwa kikwazo katika ukuaji wa Sekta hizo ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Samia Suluhu Hassan kwani Sekta binafsi ndizo zimebeba uchumi wa taifa.



 
MAKAMBAKO KUWA BUSNESS AND LOGISTIC CENTRE KAZI ZINAENDELEA 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇🚊🚊🚊Kamati ya Siasa Wilaya ya Njombe, yapongeza utekelezaji wa mradi wa maghala 112 Makambako.

Na. Lina Sanga

Kamati ya siasa Wilaya ya Njombe imepongeza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa maghala 112 ya kuhifadhia nafaka unaogharimu takribani bil. 2.24,katika Mtaa wa Makatani,Kata ya Lyamkena, Halmashauri ya Mji Makambako.

Pongezi hizo zilitolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Njombe pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo,katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Mji Makambako katika mwaka wa fedha 2023/2024.

Mhe. Justin Nusupila Sanga,Mwenyekiti Kamati ya siasa Wilaya ya Njombe amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo una tija kubwa kwa wananchi na Serikali,kwani ni mradi mzuri wa uwekezaji unaowaweka wafanyabiashara pamoja kwenye mazingira rasmi na kupata soko la uhakika.

"Nipongeze utekelezaji wa mradi huu kwani una tija kwa wananchi na Serikali,na ni uwekezaji mzuri unaoenda sambamba na jitihada za Serikali kutenga maeneo rasmi ya biashara mbalimbali",alisema Mhe. Sanga.

Ametoa rai kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako,kuendelea kufanya maboresho na kukamilisha mahitaji mbalimbali ambayo yanatakiwa kufanywa na Halmashauri ikiwa ni pamoja na kusogeza huduma muhimu zinazojitajika eneo la mradi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha huduma ya Umeme inapatikana pamoja na huduma ya Maji.

Aidha,ametoa rai kwa Ofisi ya Meneja wa TARURA Wilaya ya Njombe, kutenga bajeti ya matengenezo ya barabara kwenye eneo la mradi ambayo ina uwezo wa kuhimili magari mazito ya mizigo.

Leo Sanga,mbeba mizigo katika maghala hayo,ameishukuru Serikali kwa kubuni mradi huo kwani umeongeza uhakika wa watu mbalimbali kufanya kazi na kupata fedha kwa ajili ya kuendesha maisha yao.
1695526190346.jpg
 
Back
Top Bottom