"JIJI LINA VUMBI, SUTI HAZIVALIKI" DKT. TULIA ALIVYOOMBA KIAINA UJENZI WA MIUNDOMBINU KWA MAKAMU WA RAIS.
Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson amemuomba kiaina Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango ujenzi wa miundombinu ya barabara za Jiji la Mbeya na soko la machinga eneo kilipojengwa kiwanda cha kusindika mbogamboga na matunda.
Akitoa ombi hilo mbele ya Makamu wa Rais, Dkt Tulia amesema Jiji la Mbeya Lina kilomita zaidi ya 400 ambazo kwa Sasa zina vumbi, na kua kikwazo kwa wananchi wa Jiji hilo, hivyo ujenzi wa miundombinu utasaidia wafanyabiashara na wasindikaji kufanya shughuli zao nyakati zote.
Cc @enocksaimon
#WasafiDigital