Kahama VS Njombe/Mafinga

Binafsi yangu kati ya hiyo miji ningechagua Njombe. Watu wanadhani njombe ni mbao ambazo kimsingi wana supply East Africa yote mpaka Sudan kusini. Njombe INA supply viazi mviringo, inatoa parachichi nyingi nje ya nchi kuliko, thamani ya ardhi njombe ni kubwa kuliko kahama. Watu wa njombe ni wachapakazi sana pia naona hata kariakoo hapa wanunuzi wakubwa wa majengo ni wananjombe. Kahama ni pazuri lakini hali ya hewa na fursa za madini hazitabiriki,
 
Hapo ndipo mnapigwa bao na kukariri,huenda ni Khm ni kubwa kwa sasa lakini kasi ya Njombe ni zaidi ya sana,miti,kilimo cha mazao ya kila aina kuanzia matunda hadi nafaka,madini(chuma,makaa,asbestos),utalii(kitulo),biashara na kujaliwa wachapakazi ni tunu za no return kwa Njombe na potential yake ni kubwa kuliko Kahama ambayo soon mgodi ukizingua itapukutika
Mambo ya barabara kuu hata huku zipo tena na nyingine zinazidi kujengwa so usichukulie poa kumbuka huu ni mkoa bila shaka huduma za msingi ziko vizuri kuliko huko kwa manamba
Kusini nilifika kitambo ila kwa info zako itabidi nirudi tena maana njombe nilikuwa napita tu na sikuona kama ulikuwa ni mji promising (naongelea kama miaka tisa nyuma). Ulipoulinganisha na potential ya Iringa ndipo nikashtuka, kwani kuna kitu gani kipya maana mbao, mazao na manpower ya ukweli vimekuwepo muda mrefu tu
 
KAHAMA: kahama pana fursa ya maduka ya jumla jumla makubwa ambapo watu wa vijijini hufunga mizigo pale ongeza na watu wa Mpanda, Tabora na Kakonko hadi Kibondo wanafunga mizigo yao ya duka pale
Hao wote wanakuja ni vile miundombinu ya barabara haijaimalika kwao lakini inavyozidi kuimarika nani afuate mzigo Kahama wakati atatoa Dar moja kwa moja hadi walipo
Future ya Kahama ni ndogo kuliko hata mpanda na Geita
 
Ukitoa mbao ambazo nazo hazina soko, njombe inabakia na viazi ngoja nikupe kidogo kuhusu kahama
Mbao ni moja tu ya by products za miti lakini kuna karatasi na lami,nguzo za umeme
Kwenye kilimo ndo kwanza hakuna wa kuigusa kuanzia nafaka hadi matunda
Kwenye huduma za kiserikali pale ni makao makuu ya mkoa nadhani utaelewa taasisi zinazohusiana lakini kikubwa zaidi Njombe ita host mabwawa makubwa ya kuzalisha umeme 4 ksehemu zingine za nchi nadhani unaelewa pesa itakayokuwa inazunguka
 
Hao wote wanakuja ni vile miundombinu ya barabara haijaimalika kwao lakini inavyozidi kuimarika nani afuate mzigo Kahama wakati atatoa Dar moja kwa moja hadi walipo
Future ya Kahama ni ndogo kuliko hata mpanda na Geita


Yaan ww kisa umekaa njombe bas unajitoa ufaham mwenyew?😅😅 njombe viazi gunia haizid 40/= hebu uwe serious bas na ww..soko la mbao l8meshuka sana sana
 
Halafu parachichi unayozungumzia njombe ambayo ilianzia tukuyu hadi ushirika na viwanda vikajengwa Rungwe, maana pale njombe ile ni raw material mnazalisha na impact yake ni ndogo na ndio maana bei za miaka ile ilikua juu kuliko wakati huu
 
Parachichi hiyo inayochukuliwa sometimes na Wakenya na kwenda kua packed kwao kwa kupelekwa Ulaya imesambaa kwa sasa Ruvuma na Moshi plus Lushoto yote wameanza kilimo hicho na unafahamu formular ya Demand and suplly itavokua
 
Back
Top Bottom