Kahama VS Njombe/Mafinga

Kuifananisha Njombe na Kahama ni utovu wa nidhamu, Kahama mji mkubwa sana hapa Tanzania na una mchanganyiko wa watu wengi, una biashara nyingi tofauti na madini, ni Mji ambao ni kiungo cha nchi zinazopakana na Tanzania upande wa Magharibi.

Njombe ni mji mdogo ambao unategemea zaidi Wakinga na Wabena wapande Miti ili kupata mbao ambapo hapo unaongelea miaka 7-10 ukianza hicho kilimo tarehe ya leo. Na mjue miti ina risky za kuchomwa moto nk.
 
Na road ya Ifakara ikikamilika,na Mbeya makete Njombe ikimalizika movements za biashara zitakuwa kubwa sana kati ya Mbeya Njombe Ifakara lazima vumbi liwatimkie watu wa Songea na Iringa maana hata mabus ya Dar yata skip kupitia Iringa sasa yatapitia Njombe na Ifakara to mikumi
Njombe -ifakara -Mikumi mbona njia hii ngumu kuiconnect au ni ile inapitia Bwawa la Kihansi?
 
Kuifananisha Njombe na Kahama ni utovu wa nidhamu, Kahama mji mkubwa sana hapa Tz na unamchanganyiko wa watu wengi, unabiashara nyingi tofauti na madini, ni Mji ambao ni kiungo cha nchi zinazopakana na Tz upande wa Magharibi.

Njombe ni mji mdogo ambao unategemea zaidi Wakinga na Wabena wapande Miti ili kupata mbao ambapo hapo unaongelea miaka 7-10 ukianza hicho kilimo tarehe ya leo. Na mjue miti ina risky za kuchomwa moto nk.
Mawazo kama haya mara nyingine ni kama mawazo ya baadhi ya viongozi.
 
Kahama mzee unaisikia tu, kule hakukauki pesa na haijawahi kauka madini yapo ya kutosha.
.
Njombe kwenye mambao kitendo cha kusema ni sehemu ya mambao hii ina maana ni porini huko ulinganishe na sehemu yenye madini kama kahama?
.
Una bahati mbaya nakujua njombe kahama iko juu
Lakini kahama ni mji wa watu masikini licha ya kuwa na migodi
 
Unajua kwanini Njombe imekua ya 3, Katika Mikoa tajiri Tanzania ?, Wakati imekua Mkoa miaka 5 tu iliopita, Sababu ni wajanja katika biashara. Kuanzia Upangwa(Ludewa), Ukinga (Makete) hadi maeneo mengine wanachakarika sana hata kama eneo ni dogo.

Wanalima kilimo biashara hata iwe Mahindi kuliko maeneo mengine(ambao wao wanafanya Kilimo kula). Ingawa kwa sasa uchumi ni mgumu kokote pale lakini huwezi linganisha maeneo ya madini na yasio ya madini. Njombe wametumia akili kwa kupanda miti, Kahama wamepewa madini bure na Mungu.
 
Njombe -ifakara -mikumi mbona njia hii ngumu kuiconnect au ni ile inapitia Bwawa la Kihansi?
Ndio hiyo hiyo, Mikumi-Kihansi-Ifakara-Mlimba-Taveta-Lupembe-Njombe. Ujenzi unaendelea kwa Njombe Lupembe na Kihansi Ifakara mkuu na wala sio ngumu inapitika sehemu kubwa
 
Hahaha! Eti nimeishi miaka mitatu alafu unabwabwaja sisi wazawa tusemeje?
.
Mwanza-Shinyanga ni KM 141 na si chache ni nyingi mnooo ni masaa mawili hadi matatu kwa gari.
Njombe ni porini kumejificha watu ni washamba, Kahama wajanja wengi alafu sio wasukuma tu wametoka maeneo mbalimbali ya nchi na jirani
Sasa Kahama utaitenganishaje na usukuma ushamba na umasikini
 
Naifahamu njombe sana sana..kuna miaka biashara ya mbao ilikua juu vby sana sana..naijua hii biashara ...lakini huwez ifananisha Njombe na Kahama..mayb weka battle la Njombe na Mafinga..na mafinga itaibuka kidedea...! njombe imekuwa uswekeni..zaman kina mama walikua wanajiita mama mbao sasa hv watu wanaenda na aluminium and the like...uliza wauza mbao wa pale mwnge kama wanauza kma 7yrs ago!

Hii battle nimemshangaa labda hajatembea huyu muanzisha maada, Kahama huwezi ifananisha na hata Iringa, Tabora, Songea, Kigoma, Shinyanga na the like
 
Kuifananisha Njombe na Kahama ni utovu wa nidhamu, Kahama mji mkubwa sana hapa Tz na unamchanganyiko wa watu wengi, unabiashara nyingi tofauti na madini, ni Mji ambao ni kiungo cha nchi zinazopakana na Tz upande wa Magharibi.

Njombe ni mji mdogo ambao unategemea zaidi Wakinga na Wabena wapande Miti ili kupata mbao ambapo hapo unaongelea miaka 7-10 ukianza hicho kilimo tarehe ya leo. Na mjue miti ina risky za kuchomwa moto nk.
Hapo ndipo mnapigwa bao na kukariri, huenda ni Kahama ni kubwa kwa sasa lakini kasi ya Njombe ni zaidi ya sana, miti, kilimo cha mazao ya kila aina kuanzia matunda hadi nafaka, madini(chuma, makaa, asbestos), utalii(kitulo), biashara na kujaliwa wachapakazi ni tunu za no return kwa Njombe na potential yake ni kubwa kuliko Kahama ambayo soon mgodi ukizingua itapukutika.

Mambo ya barabara kuu hata huku zipo tena na nyingine zinazidi kujengwa so usichukulie poa kumbuka huu ni mkoa bila shaka huduma za msingi ziko vizuri kuliko huko kwa manamba
 
Hii battle nimemshangaa labda hajatembea huyu muanzisha maada, kahama huwezi ifananisha na hata Iringa, tabora, songea, kigoma, shinyanga, na the like
Mnhh

Ambao hatujafika Kahama wacha tu mute tu.
 
Hii battle nimemshangaa labda hajatembea huyu muanzisha maada, kahama huwezi ifananisha na hata Iringa, tabora, songea, kigoma, shinyanga, na the like
Hayo ni matusi kwa miji tajwa hapo juu. Nini kikubwa kiko Kahama afu miji uliyoitaja haina au imepitwa? Labda Kigoma, Sumbawanga ila Iringa unaidhalilisha kuiweka ligi moja na Kahama
 
33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom