Kahama VS Njombe/Mafinga

The Rovos Rail journey from Cape Town to Dar Es Salaam covers approximately 5,530 kilometers.

This journey takes 15 days and travels through SouthAfrica๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡ฆ, Botswana๐Ÿ‡ง๐Ÿ‡ผ, Zimbabwe๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡ผ, Zambia๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡ฒ, and Tanzania๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

The Pride of Africa train, used for this route, is known for its luxury and scenic views.
 
Msongamano wa maroli makambako baada ya songea road nayo kuwa na maroli mengi
 
MKOA WA NJOMBE NI MOTO AGENDA YAO YA KUWA NA MJI MKUBWA WA VIWANDA NA BIASHARA INAZIDI KUELEWEKA WAGENI WANAINGIA KILA SIKU ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡I๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡MwakilishiMaendeleo Umoja wa Mataifa (UNDP) Shigeki Komatsubara amesema amefurahi kutembelea ardhi ya Njombe na kushuhudia viwanda vya parachichi jinsi vinachakata tunda hilo.

Ameeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya parachichi Avoafrika kilichopo Mtewela , na kiwanda cha kufungasha parachichi AvoAfrica kilichopo majengo Halmashauri ya mji makambako wilaya ya Njombe.

@makambakotc
 
Mapatachichi as usual ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿค— ๐Ÿ˜‚
 
Mapatachichi as usual ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿค— ๐Ÿ˜‚
Soma hapo alitembelea VIWANDA vingapi usikalili ukajua Kuna VIWANDA vya parachichi tu ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡ MWAKILISHI MKAZI WA UNDP ATEMBELEA MIRADI YA UWEKEZAJI MKOANI NJOMBE

Njombe, 12 Juni 2025 โ€” Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bw. Shigeki Komatsubara, amefanya ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Njombe yenye lengo la kutembelea na kujionea fursa za uwekezaji zilizopo Mkoanj Njombe, hasa zile zilizojikita zaidi kwenye mazao ya kilimo na kuongeza thamani.

Mara baada ya kuwasili, Bw. Komatsubara alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, ambaye alitumia nafasi hiyo kumkaribisha mkoani Njombe na kumweleza fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta mbalimbali.

โ€œMkoa wa Njombe una ardhi nzuri na yenye rutuba, mazingira rafiki kwa uwekezaji, na wananchi wachapakazi. UNDP mnayo nafasi ya kipekee ya kushirikiana nasi katika kuinua kilimo, viwanda na ajira kwa vijana wetu,โ€ alisema Mhe. Mtaka.

Katika ziara hiyo, Bw. Komatsubara alitembelea viwanda mbalimbali vikiwemo cha kuchakata mafuta ya parachichi cha AVO Afrika, kiwanda cha kufungasha parachichi Makambako, kiwanda cha mbao cha EAST KELIN WOOD, pamoja na viwanda vya chai vya Kibena na TANWAT.

Akiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, alipewa taarifa ya fursa za uwekezaji zilizopo mkoani humo, hasa katika sekta ya kilimo, viwanda vidogo na huduma za kijamii.

Akizungumza mwishoni mwa ziara yake, Bw. Shigeki Komatsubara jana tarehe 11, 2025 alisema:

โ€œNimefurahishwa sana na mapokezi niliyoyapata Njombe. Ardhi yenye rutuba, mazingira mazuri na watu wa kujituma vinaufanya mkoa huu kuwa na fursa kubwa sana za maendeleo. Bila shaka, nitarejea tena Njombe kuona namna bora ya kushirikiana katika utekelezaji wa miradi ya pamoja.โ€

Ziara hii inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya UNDP na Serikali ya Mkoa wa Njombe katika kuchochea maendeleo endelevu kupitia uwekezaji, ubunifu, na matumizi bora ya rasilimali zilizopo.
 

Viwanda vinazidi KUONGEZEKA mkoa wa njombe ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡LUDEWA CEMENT YATARAJIWA KUANZISHWA LUDEWA WAWEKEZAJI WA KAMPUNI YA KICHINA HWTZ KWA WANANCHI WA LUPANGA NA MASIMBWE​



Katika juhudi za kukuza uchumi wa Wilaya ya Ludewa kupitia rasilimali zake kama chuma na makaa ya mawe, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mhe. Olivanus Thomas, amefanya mikutano ya hadhara katika vijiji vya Lupanga na Masimbwe kwa lengo la kuwatambulisha wawekezaji kutoka kampuni ya HWHG ya China. Kampuni hiyo imeanzisha kampuni tanzu nchini Tanzania kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) inayoitwa HWTZ, ambayo inapanga kuwekeza katika ujenzi wa viwanda mbalimbali wilayani humo.

Miongoni mwa viwanda vinavyotarajiwa kujengwa ni kiwanda cha saruji, ambacho kitazalisha bidhaa itakayojulikana kama "Ludewa Cement." Mhe. Thomas aliwahakikishia wananchi kuwa maeneo yao yatakayotumika kwa uwekezaji huo yatazingatia haki na fidia stahiki, na kwamba serikali itasimamia mchakato huo kwa uwazi na ushirikishwaji wa jamii.

Uwekezaji huu wa viwanda utahusisha baadhi ya vijiji katika wilaya hiyo, ambapo Mhe. Thomas alieleza kuwa mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na ajira, maendeleo ya miundombinu, na fursa za biashara.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Ndg. Sunday Deogratius, aliwataka wananchi kutumia fursa za kibiashara zitakazojitokeza kutokana na uwekezaji huo, kama vile usambazaji wa bidhaa na huduma mbalimbali kwa viwanda hivyo.

Wananchi waliohudhuria mikutano hiyo walieleza furaha yao kwa kuwapokea wawekezaji hao, wakielezea matumaini yao kuwa uwekezaji huo utaleta maendeleo na kuboresha maisha yao kwa ujumla.

Uwekezaji huu unatarajiwa kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi katika Wilaya ya Ludewa, na kuchangia katika juhudi za serikali za kukuza sekta ya viwanda nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ