Kahama VS Njombe/Mafinga

Kahama VS Njombe/Mafinga

KITWE, ZAMBIA: Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) imetangaza uwekezaji mkubwa wa Dola bilioni 1.4 kwa ajili ya kuboresha miundombinu yake na shughuli zake, ikiwa ni hatua mpya kwa mfumo wa reli wa zamani.

Mkataba huo utakaotekelezwa na Kampuni ya Ujenzi ya Uhandisi ya China (CCECC), ulitangazwa Alhamisi na Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA, Mhandisi Bruno Ching'andu, kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Madini na Nishati wa Zambia (ZIMEC) uliofanyika Kitwe.

Akizungumza mbele ya umati wa wawekezaji na wataalamu wa sekta, Ching'andu alielezea vipengele vikuu vya uwekezaji huo, ambao unalenga kurejesha ufanisi na uwezo wa TAZARA.

Amesema, "ingawa mazungumzo bado yanaendelea, mkataba huu utatekelezwa chini ya makubaliano ya miaka 30."

Kifurushi cha uwekezaji kimejumuisha Dola bilioni 1.0 kwa ajili ya ukarabati wa reli za TAZARA, pamoja na Dola milioni 400 kwa ajili ya kununua vichwa vipya 32 na mabehewa 762.

Imeandaliwa na Mwandishi Wetu

#HabariLeoUpdates
 

View: https://www.instagram.com/p/DHc_bJ8M4oQ/?img_index=9&igsh=MWNyOWU3bmllZWJlaw==
tzcuom_1742544790394.jpg
tzcuom_1742544798228.jpg
tzcuom_1742544794502.jpg
tzcuom_1742544793424.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, amesema kuwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ni kitovu cha misitu nchini, kwani misitu sio tu biashara, bali ni sehemu ya maisha yao. Amesema hayo leo Machi 21, 2025, katika kuadhimisha Siku ya Misitu Duniani na Upandaji Miti Kitaifa mkoani Njombe. Chongolo ameongeza kuwa uvumilivu na uchapakazi mkubwa wa wakazi wa mikoa hiyo ndio unawawezesha kupanda miti inayochukua muda mrefu kuvunwa.

Amemwomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kusaidia kujenga bandari kavu Makambako, kutokana na ukweli kwamba eneo hilo na mkoa wa Njombe unapitiwa na reli ya TAZARA na hiyo itasaidia kusukuma ajenda ya miradi mikubwa katika mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama parachichi alipotembelea Kiwanda cha Kuchakata zao la Parachichi AvoAfrica Tanzania Limited kiichopo Makambako Mkoani Njombe, Machi 23, 2025. Kulia kwake ni Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Nagib Kamal.
FB_IMG_17427831580001902.jpg
FB_IMG_17427831511229828.jpg
FB_IMG_17427831757582868.jpg
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania @kassim_m_majaliwa amewaasa wananchi wa Makambako waendelee kufanya kazi kwa bidii kwani ni Mji unaokua kwa kasi kubwa.

Ameyasema hayo leo Machi 23,2025 akiwa mjini makambako, wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kumsikiliza eneo la tenki la maji ambapo pia amesema serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ili kusogeza huduma za kijamii karibu na wananchi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Makambako Deo Sanga, ameshukuru serikali kwa kutatua baadhi ya kero zinazowakabili wananchi huku akisisitiza kulipwa fidia kwa wananchi waliopisha mradi wa umeme wa upepo.

@makambakotc
FB_IMG_17427843913178651.jpg
FB_IMG_17427312036836006.jpg
FB_IMG_17427844064216376.jpg
FB_IMG_17427311954345578.jpg
 
WAZIRI MKUMBO AZINDUA OFISI ZA TIC KANDA YA NYASA – NJOMBE

NJOMBE, 24 Machi 2025 – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb), amewasili mkoani Njombe na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka, ambapo amesaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Prof. Mkumbo ni mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Nyasa, Njombe, hatua inayolenga kurahisisha huduma kwa wawekezaji katika Nyanda za Juu Kusini.

Kwa sasa, Waziri Mkumbo anaendelea kuhutubia viongozi wa serikali, wafanyabiashara na wawekezaji wa mkoa wa Njombe. Baada ya uzinduzi, atafanya ziara kutembelea Mradi wa Murikado Food Supply Co. Ltd wilayani Wanging'ombe.
 
Katika jitihada za kuimarisha mazingira ya uwekezaji kwa Watanzania, Serikali ya Mhe. Rais imesogeza fursa za uwekezaji wa ndani (watanzania) kwa kutoa huduma bora na kufanya uwekezaji wao katika mazingira bora. Leo 24 Machi, 2025 Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), tunafungua rasmi ofisi mpya ya Kanda ya Nyasa katika Mkoa wa Njombe. Ofisi hii itatoa huduma kwa mikoa ya Njombe, Ruvuma, Iringa, na Mtwara. Tunalenga kutoa huduma bora kwa wawekezaji wa ndani na kuwasogezea fursa kwa karibu.Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, atakuwa mgeni rasmi katika hafla hii ya ufunguzi hapa Njombe na pia atatembelea miradi ya uwekezaji na kuwasikiliza wawekezaji ili kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa wawekezaji wa kanda hii.Tunatarajia kuwa ofisi hii itaimarisha zaidi uwekezaji wa ndani na kuleta maendeleo ya kiuchumi katika kanda hii na taifa kwa ujumla.
 

WAZIRI MKUMBO ATEMBELEA KIWANDA CHA KUSINDIKA PARACHICHI NJOMBE

NJOMBE – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, tarehe 24 Machi,2025 alifanya ziara mkoani Njombe ambapo, aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, alitembelea Kiwanda cha Muricado Fruit Supplies kujionea uwekezaji mkubwa unaofanyika katika kuongeza thamani ya zao la parachichi.

Akizungumza baada ya kutembelea kiwanda hicho, Mhe. Prof. Mkumbo alimpongeza muwekezaji kwa juhudi zake katika kukuza sekta ya viwanda na kilimo. "Huu ni uwekezaji wenye tija kwa wakulima wa parachichi na uchumi wa taifa kwa ujumla. Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani ili kuhakikisha viwanda vya aina hii vinakua na kuchangia maendeleo ya nchi," alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Josiah Mrimi, alisema kuwa uwekezaji huo unalenga kuongeza thamani ya zao la parachichi kwa kusindika na kuuza bidhaa zake katika soko la ndani na kimataifa.

Kiwanda cha Muricado Fruit Supplies kinatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa wakulima wa parachichi kwa kuwapatia soko la uhakika, sambamba na kusaidia jitihada za serikali za kuendeleza sekta ya viwanda na kilimo nchini.
FB_IMG_17429535819486251.jpg
FB_IMG_17429535918695750.jpg
FB_IMG_17429536058256170.jpg
 
WAZIRI MKUMBO ATEMBELEA KIWAANDA CHA KELIN WOOD EAST AFRICAN, AONYESHA KURIDHIKA NA UWEKEZAJI MKOANI NJOMBE

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo,alipata fursa ya kutembelea kiwanda cha KELIN WOOD EAST AFRICAN kilichopo mkoani Njombe halmashauri ya Wilaya ya Njombe na kujionea mwenyewe uwekezaji mkubwa unaofanywa katika kuongeza thamani ya mazao ya misitu. Ziara hiyo ilifanyika tarehe 24 Machi, 2025, akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka.

Akizungumza baada ya kutembelea kiwanda hicho, Mhe. Prof. Mkumbo alielezea kuridhika kwake na juhudi za kiwanda hicho katika kuongeza thamani ya mazao ya miti, ikiwemo uzalishaji wa bidhaa kama Ringboard na Siljng board. Waziri alisisitiza kuwa uwekezaji huu unachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi wa mkoa na kutoa ajira kwa vijana, hasa katika maeneo ya vijijini.

"Tunashuhudia Njombe ya viwanda sasa, na hii ni alama kubwa sana ya maendeleo. Uwekezaji huu umefungua milango ya ajira kwa vijana wetu na kuinua uchumi wa wakulima. Ni mfano mzuri wa namna ambavyo mazingira rafiki ya uwekezaji yanavyoweza kuleta maendeleo ya haraka," alisema Prof. Mkumbo.

Mhe. Prof. Mkumbo pia aliongeza kuwa serikali itaendelea kuwekeza katika miundombinu na sera zinazohamasisha uwekezaji katika viwanda vya ndani, akielezea furaha yake kwa kuona kiwanda cha KELIN WOOD EAST AFRICAN kikiendeleza uzalishaji wa bidhaa zenye manufaa kwa uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.
FB_IMG_17429779668858065.jpg
FB_IMG_17429779367650251.jpg
 
Back
Top Bottom