Kahama VS Njombe/Mafinga

Kahama VS Njombe/Mafinga

🇹🇿🇹🇿OFISI YA MBUNGE JIMBO LA NJOMBE MJINI🇹🇿🇹🇿

BARAZA MAALUMU LA MADIWANI WAAZIMIA KUBADILI JINA LA JIMBO LA UCHAGUZI LA NJOMBE MJINI

Machi 19, 2025 Baraza maalumu la waheshimiwa Madiwani limeketi na kujadili ombi la kubadili jina la Jimbo la uchaguzi la Njombe Mjini kufuatia tangazo lililotolewa na Tume huru ya Taifa ya uchaguzi ikitaka kuwasirisha maombi ya kugawa maeneo ya uchaguzi panapokidhi vigezo au kuomba kubadilisha Majina kutoka na uhitaji na umuhimu wa eneo husika.

Hivyo, Baraza Maalumu kwa pamoja wameazimia jina la "JIMBO LA NJOMBE MJINI" na kuitwa "JIMBO LA NJOMBE KUSINI". Miongoni mwa sababu zilizofanya jina hilo kubadilishwa ni kama zifuatazo:-
1. Jimbo la Njombe Mjini lina Tarafa mbili zenye jumla ya kata 13 ambapo Tarafa ya Njombe Mjini ina kata 3 na Tarafa ya Igominyi (Vijijini) ina kata 10, hivo kuitwa Jimbo la Mjini haileti uhalisia
2. Jimbo limekuwa likikosa mgawanyo sawia wa raslimali kama watumishi wa sekta ya Afya na Elimu, mgawanyo wa fedha za barabara nk kwa kigezo ni Mjini wakati uhalisia kata 10 ziko vijijini.
3. Kuwa na Jina ambalo linaakisi uhalisia kutokana na kata nyingi kuwa vijijini

Mhe. Deo Mwanyika (MB) amelipongeza Baraza la Madiwani kwa maamuzi hayo dhabiti ya jimbo kuitwa "Jimbo la uchaguzi la NJOMBE KUSINI". Jambo ambalo litasaidia sana katika uwasilishaji wa hoja na mahitaji ya wananchi hususani wa vijijini ambao wamekuwa wakikosa mgawo sawia wa keki ya Taifa kwa kigezo kuwa wako Mjini. Ni imani yake Mhe. Mbunge kuwa Tume watazingatia ombi hilo kwa maslahi mapana ya wananchi wa Njombe.

Na Mhe. Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Njombe amelipongeza baraza hilo kwa kuona umuhimu wa kubadili jina la jimbo la uchaguzi kwa maslahi mapana ya wananchi, nao kama chama wanabariki maamuzi hayo.

#Njombe Mpya
# Dira Mpya, kazi iendelee
 
Back
Top Bottom