Kagoda Haina Kesi, hawafikishwi Mahakamani Ng'o! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kagoda Haina Kesi, hawafikishwi Mahakamani Ng'o!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Nov 3, 2009.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,595
  Likes Received: 18,589
  Trophy Points: 280
  Wana bodi, hii ni kubwa kuliko na kali ya aina yake sio tetesi, ni uhakika wa 100% Kagoda inajulikana na wote, ni Safi, na kamwe haitafikishwa mahakamani.
  Nikiwa mjini Dodoma kwenye kona kona za hapa na pale, nilibahatika kukutana mmoja wa waheshimiwa wenye nguvu sana nchi hii. Katika mazungumzo yetu, mimi nilimbeza kuwa Mkuu wa kaya ni dhaifu, hana uwezo, na too weak to fight mafisadi kweli.

  Basis ya udhaifu wa mkuu wa kaya niliuelekeza kwa kile kitendo cha kuushindwa mpasuko wa Zanzibar nikampa na angalizo kuwa kitendo cha kumuonea aibu Kagoda na kuendelea kuwakumbatia mafisadi ndani ya chama, kitamcost, kasababu atafikia mahali akashindwa kuwabeba, uzito utamwelemea, mwisho au watamuangusha, au wataanguka nae.

  Akamtetea mkuu wa kaya kuwa sio kweli ni dhaifu, issue ya Zanzibar hata yeye haimfurahishi, ila wengi wape.

  Ndipo akanipa siri ya Kagoda, kumbe Kagoda, alirudisha fedha zote, hivyo hadaiwi hata senti moja, hivyo unamfikisha mahakamani kumdai nini?.
  Eti kumbe Kagonda ni mtu safi, clean, tatizo liko wapi?.
  Kwa hiyo wanabodi, suala la Kagoda ni kelele tuu za mlango, hazimkoseshi mwenye nyumba usingizi.

  NB. Pamoja na JF 'where we dare talk open', nawaombeni nimhifadhi source wangu kwa kutumia 'confidentiality of the source', ukiaminiwa, jiaminishe.

  Naomba kuwasilisha
   
 2. G

  Gashle Senior Member

  #2
  Nov 3, 2009
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pasco, makubwa hayo, though mimi kwa ufahamu wangu nilifikiri kuwa kupelekwa mahakamani sio tu ili ulipe ama kurudisha. nafikiri issue hapa ni wizi. ingredients za wizi ziko wazi, km mens rea na actus reus zimethibitishwa, kwa nini asipelekwe mahakamani? sidhani km mwizi kurudisha alichoiba kunamuondolea ule uizi aliokuwa nao
   
 3. K

  Keil JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tangu lini mwizi akirudisha alichoiba anakuwa ni msafi?

  Mbona waliorudisha ni wengi tu na wengine kati yao wamefikishwa mahakamani. Wanatumia basis gani kuona kwamba KAGODA is clean while wengine walio chota kwenye EPA hawako clean?

  Wao waseme wazi kwamba KAGODA ni clean kwa sababu alipeleka fedha kiasi fulani zikaenda kufadhili uchaguzi wa CCM. Serikali ya JK haiwezi ku-deal na KAGODA kwa kuwa ni sawa na serikali kukata tawi la mti ambalo wamekalia, likidondoka na serikali nayo inakwenda na maji.

  Mfumo wa law enforcement ndio ambao unawafanya "wao" waseme kwamba KAGODA hana kosa. Kwa kuwa PCCB, DPP, IGP, na AG, wote wanafanya kazi kwa kufuata maelekezo ya Ikulu na hawawezi kwenda kinyume unless wawe hawataki hiyo kazi.
   
 4. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,106
  Trophy Points: 280
  Oops my ass, Kagoda karudisha bil 40? ziko wapi? Dhambi hii ndiyo itakayowaondoa CCM madarakani.
   
 5. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2009
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kama suala lingekuwa ni kurudisha ulichoiba basi wafungwa wangepungua magerezani kwani wapo wengi wenye uwezo wa kurejesha walichoiba na bado wamehukumiwa kwa kosa la wizi. Hivyo huyo mnene uliyeongea naye ama uwezo wake wa kutafakari na kutafsiri sheria ni wa chekechea au ni fisadi anajaribu kufunika kombe mwanaharamu apite!
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Nov 3, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Pole sana pasco. Tulishayasema haya humu. Aliyerudisha fedha ni manji kwa niaba ya kina ra. Na ndiye pekee aliyefanya hivyo kwa hiari. Hivi watu hamjajiuliza kwa nini fedha zilizorejeshwa zimepelekwa kwenye kilimo? Si inaitwa kagoda agriculture?
   
 7. l

  lukule2009 Senior Member

  #7
  Nov 3, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na wakati huo huo Patel kapewa tenda ya kuleta matrekta katika kilimo kwanza.. so unaweza kukuta ni mkakati uliobuniwa wa kuzirejesha pesa kwa mlango wa nyuma.. simpel unaoverprice tu hizo trekta bei mara mbili .. basi ..
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  the dots CONNECTED!
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280


  Isije ikawa hata hii kauli mbiu ya Kilimo kwanza ilibuniwa ili kufunika funika yajayo, manake sasa kama tenda ya matrekta ta 'kilimo kwanza' ndo anayo huyo na kama kuna hu uwezekano wa kuinflate bei, basi imekula kwetu! hawa jamaa wako maili kumi mbele yetu! unaweza kudhani wana mind reading capabilities!
   
 10. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Sasa macho yangu yamefunguka kwani nilikuwa najiuliza Rai walikuwa wanaikandia kauri ya kilimo kwanza na kusema inatokea South Africa na Muasisi wake ni Nelson Mandela Rais msitafu wa SA, kumbe wanajaribu kuamisha concentration kutoka kwa kagoda Ltd na kuipeleka SA.

  Hapa kama hatuko macho mapesa yaliyorudishwa yote yanarudi kwa manji kwa kauri mbiu ya kilimo kwanza kwani kagoda inajishugulisha na kilimo hata wakipewa tutaambiwa tenda ilitangazwa wakashinda wakapewa mapesa hayo.

  Hivi sisi watanzania tumerogwa au, na kama tumerogwa basi aliyeturoga ameshakufa hata dawa hatutaipata.

  Hivi wanaboard niambieni mbona sioni chama kilichoserious katika kutetea haki za watz, wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, mtaani kwetu chama cha upinzani kilikuwa CUF tu na walisimamisha mtu ambaye kwangu mimi nasema hafai kulingana na quality za uongozi na ndio kilichotokea wakashindwa vibaya sana.

  Sasa tutawezaje kusimamisha ujinga wa CCM bila kuwa na uongozi mbadala wa kutusaidia?
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,811
  Likes Received: 83,186
  Trophy Points: 280
  Kagoda alias Rostam Aziz ni sterling hata movie ikiisha yeye bado atakuwa kasimama. Pale Ikulu tuna njemba lakini mwenye madaraka zaidi ni Kagoda 'aka' RA huyu ataendelea kula kuku zake bila kuguswa na yeyote yule.
   
 12. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2009
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  bwana G hakukuwa na wizi pale. kwani ulishasikia kuwa benki kuu pamebomolewa? sasa utakuwaje ni wizi ilhali wamepewa fedha kwa utaratibu maalumu. ulishaambiwa wapo maafisa kadhaa wa serikali walioidhinisha malipo akiwepo Gavana Balali RIP.

  kwani nyumbani kwako mkeo akitoa pesa kwa wapita njia, hao wapita njia utawaita wezi?
   
 13. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  .....kama sisi sote tuna hasira hizi, na kama zingetafsiriwa kwa watanzania wengi, basi hawa jamaa wasingekuwa wanatugeuzageuza namna hii. wanachofanya ni kucheza na akili zetu, na bado wanazidi kuwa hapo.
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,595
  Likes Received: 18,589
  Trophy Points: 280
  Kagoda hakuwa mwizi, ni jamaa wa UWT walimtumia tuu kama njia, wakamwingiza mkenge Mama Megji kuwa ni za kazi maalum ya UWT, Mama Meghji akaingia line, wanaume wakachota na kazi ikafanyika vizuri kwa silimia 99% ila mmoja wa vifaranga kikakosa jimbo, JK akalipa fadhila akakipachika bungeni.
  Hivyo kwenye Kagoda hakuna wizi, hakuna uchunguzi, hakuna hatua zozote za kuchukuliwa, its over
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,595
  Likes Received: 18,589
  Trophy Points: 280
  .
  Kama Kagoda ndiye king maker, alimsaidia JK kufika Ikulu, then Kagoda ndiye Ikulu, JK akimsikiliza ili aweze kubaki Ikulu, na amini nawaambieni, kama ni kweli Kagoda anammaind spika Six, basi spika ataanguka, na jamaa Richmonduli ataibukia Ikulu, 2015!
   
 16. G

  Gashle Senior Member

  #16
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jamani jamani, tuacheni porojo, hela zimekwapuliwa, hakuna mwizi, Kagoda karudisha, hakuna mwizi... hallo:confused: Ninachojaribu kusema kuwa ni kuwa whoever who took that money, I care very little kwamba ni nani au nani ndio mwizi wetu huyo!

  Yale yale ya "baba kaniuliza swali, mama kaja na jibu... mjomba nikipata nauli..."
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,595
  Likes Received: 18,589
  Trophy Points: 280
  .
  Haiwezi kuwaondoa madarakani kama ni dhambi hii hii ndiyo iliyowaweka madarakani, wataitumia kuhakikisha wanatawala milele.
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,595
  Likes Received: 18,589
  Trophy Points: 280
  kuna tofauti ya kuiba na kuchukua, kuiba ni kuchukua bila idhini, kuchukua kwa idhini na baadaye ukarudisha kosa liko wapi?.
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  ...and the movie continues. Stay tuned!
   
 20. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #20
  Nov 4, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ukizungumzia Kagoda, Meremeta...unazungumzia Mr Clean, CCM na utawala uliopo. Hakuna anayeweza kuukata mkono uliompa ulaji.

  Leka
   
Loading...