Kagoda Haina Kesi, hawafikishwi Mahakamani Ng'o!

Jamani tuhamie nchi ipi kupata mafunzo ya kuleta mapinduzi, mapinduzi ya kung'oa udhalimu, wizi, ubazazi na kila aina ya dhuluma katika jamii. Kwa nini kuna watu wenye hadhi zaidi ya wengine mbele ya sheria? Nani kasema Kagoda haijulikani, mbona iko wazi kabisa? Hawataki kuishitaki kwa sababu wanalindana ndiyo maana nachagiza tutafute nguvu z amapinduzi ya kung'oa udhalimu!
 
kuna mtu ana takwimu ni kiasi gani mpaka sasa kinatuhumiwa kimeibwa kupitia EPA,ujenzi BOT,Alex Stewart,tenda ya kutengeneza noti BOT,kiwira,meremeta n.k especially zile ambazo uchunguzi huru umefanyika?

Ni impossible kumuibia asiyenacho, na ikiwa nchi inaibiwa basi inacho

je sisi ni maskini?

am justi kyurias
 
mkuu kwa hesabu ambayo sio conservative, hicho kiasi kinaweza kufikia bajeti ya mwaka huu ya nji .I mean kwenye trilions of money!

kwa maneno mengine, tuna uwezo wa kujitosheeza kwa bajeti bila kutegemea misaada ya 'wahisani', kama hii mianya ingezibwa
 
Jamani tuhamie nchi ipi kupata mafunzo ya kuleta mapinduzi, mapinduzi ya kung'oa udhalimu, wizi, ubazazi na kila aina ya dhuluma katika jamii. Kwa nini kuna watu wenye hadhi zaidi ya wengine mbele ya sheria? Nani kasema Kagoda haijulikani, mbona iko wazi kabisa? Hawataki kuishitaki kwa sababu wanalindana ndiyo maana nachagiza tutafute nguvu z amapinduzi ya kung'oa udhalimu!

Haya ndio maswali ambayo mimi yananikuna kwa sasa. Yatosha. Its time for action and not blah blah blah!
 
mhh! Karudisha bilioni 40? Kwa nini asirudisha na riba? Kwani amekaa na pesa hizo kwa muda gani na alizifanyia nini kama si kupata faida? Basi angeweka na interest! Lakini yote ni bure kwani kesi ya nyani itasililizwa vipi na kima?

Tukubali imekula kwetu!
kurudishwa ni kwa paperwork hata bilioni 80 wangerudisha tuu.
 
Pasco mkuu, maneno yako nimeyasoma kwa uchungu mkuu sana. Sasa naanza kuamini yale yaliyosemwa humu jamvini siku za nyuma kuwa NCHI YETU IMELAANIWA. Iweje haya yote yanafahamika na hakuna linalofanyika?
Pole mkuu JK tumemuajiri wenyewe na mwakani atakuja kutuomba tumuongezee muda wa miaka mitano mingine ili amalizie haya mazuri, na tutamuongezea!.
 
Wana bodi, hii ni kubwa kuliko na kali ya aina yake sio tetesi, ni uhakika wa 100% Kagoda inajulikana na wote, ni Safi, na kamwe haitafikishwa mahakamani.

Nikiwa mjini Dodoma kwenye kona kona za hapa na pale, nilibahatika kukutana mmoja wa waheshimiwa wenye nguvu sana nchi hii. Katika mazungumzo yetu, mimi nilimbeza kuwa Mkuu wa kaya ni dhaifu, hana uwezo, na too weak to fight mafisadi kweli.

Basis ya udhaifu wa mkuu wa kaya niliuelekeza kwa kile kitendo cha kuushindwa mpasuko wa Zanzibar nikampa na angalizo kuwa kitendo cha kumuonea aibu Kagoda na kuendelea kuwakumbatia mafisadi ndani ya chama, kitamcost, kasababu atafikia mahali akashindwa kuwabeba, uzito utamwelemea, mwisho au watamuangusha, au wataanguka nae.

Akamtetea mkuu wa kaya kuwa sio kweli ni dhaifu, issue ya Zanzibar hata yeye haimfurahishi, ila wengi wape.

Ndipo akanipa siri ya Kagoda, kumbe Kagoda, alirudisha fedha zote, hivyo hadaiwi hata senti moja, hivyo unamfikisha mahakamani kumdai nini?

Eti kumbe Kagonda ni mtu safi, clean, tatizo liko wapi?

Kwa hiyo wanabodi, suala la Kagoda ni kelele tuu za mlango, hazimkoseshi mwenye nyumba usingizi.

NB. Pamoja na JF 'where we dare talk open', nawaombeni nimhifadhi source wangu kwa kutumia 'confidentiality of the source', ukiaminiwa, jiaminishe.

Naomba kuwasilisha
Pasco

Asante MMKJJ, kwa mujibu wa mtoaji habari wangu, aliyerudisha fedha za Kagoda sio Manji, mtoa habari huyo aliidefendi Kagoda kuwa kama ni fedha fedha za Kagoda zilitumika kufanikisha uchaguzi wa CCM, mtoa habari huyo akaniuliza sasa hawa Kagoda walipata wapi hiyo bilioni 40 iliyorudishwa!.
Kwa maoni yangu, ni kweli Kagoda alichota hizo bilioni 40 pia ni kweli ndizo zilizoibeba CCM na JK wake. Ila haijarudishwa hata senti 5, bali paperwork imefanyika kuonyesha pesa imerudishwa. Wahusika wote wakuu wanalijua hili, ndio maana wanampigia magoti all the time.
Sitta ilikuwa ang'olewe, amenusuriwa sio kwa sababu anakubalika, bali kuondoa uwezekano wa kumeguka na pande kubwa, but his days are numbered na jamaa atahit back big blow baada ya bunge kuvunjwa Ijumaa ya Agosti 6, 2010.
Leo nilikuwa napita pita humu, nikakutana na bandiko hili la 2009, 14 years ago!.
Watu wakija kumjua aliyelipwa fedha za Simbion ni nani, na wakaja kumjua mfadhili Mkuu wa ile movie ya ..., ndio mtaelewa hata CAG ni mtu mdogo tuu na ripoti ya CAG ni ripoti ya kawaida tuu, baadhi ya hoja za CAG ni fedha zilizokwapuliwa kwaajili ya matumizi mazuri tuu.

Mungu ibariki Tanzania
P.
 
Ooh kumbe!?
 
Ooh kumbe!?
Nadhani kwenye katiba mpya tutaweka maximum transparency clause, akitokea mtu anamfadhili rais wetu na kuifadhili Ikulu yetu, Watanzania tuelezwe wazi ni nani, anafadhili kwa kiasi gani, sources of funds and what is the motives behind ufadhili huo and what is s/he stands to gain kwa ufadhili huo?
P
 
Kama alivyosema Kambarage "UKISHAKULA NYAMA YA MTU[BINADAMU] HUWEZI KUACHA" na hawa mafisadi watabuni EPA nyingine ya kuwavusha 2010 kama sio KILIMO KWANZA basi itakuwa MRADI WA VITAMBULISHO!!
Na hicho ndio kinachomfanya Samia asimuondoe Mwigulu ili watengeneze EPA nyingine ya kumvusha 2025!! Hizi zilizochukuliwa kama alivyoonesha CAG ni za awalli, zenyewe zinafuata mwaka kesho! Huu sio uzushi ndio kawaida ya ccm na ndio utaratibu waliojiwekea wa kukwapua fedha za wananchi ili kuwavusha wenye uchaguzi ; kwa ushahidi zaidi soma kitabu cha Marehemu Ben Mkapa!
 
Leo nilikuwa napita pita humu, nikakutana na bandiko hili la 2009, 14 years ago!.
Watu wakija kumjua aliyelipwa fedha za Simbion ni nani, na wakaja kumjua mfadhili Mkuu wa ile movie ya ..., ndio mtaelewa hata CAG ni mtu mdogo tuu na ripoti ya CAG ni ripoti ya kawaida tuu, baadhi ya hoja za CAG ni fedha zilizokwapuliwa kwaajili ya matumizi mazuri tuu.

Mungu ibariki Tanzania
P.
Hatari
 
Na hicho ndio kinachomfanya Samia asimuondoe Mwigulu ili watengeneze EPA nyingine ya kumvusha 2025!! Hizi zilizochukuliwa kama alivyoonesha CAG ni za awalli, zenyewe zinafuata mwaka kesho!
Mimi namuunga mkono Samia, asimchukulie hatua mtu yoyote kwasababu tuu watu wanasema!, awachukulie hatua watu kwasababu wanahusika.
P
 
Back
Top Bottom