Kagera: Watumishi wa Umma washtakiwa kwa Kuficha Mapato ya Manispaa Tsh. Milioni 409.4

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,123
1695363293548.png

Watumishi hao ni Richard L. Kubona, Adelina K. Leonard na Musa S. Kalumba ambao ni Maafisa Biashara wa Manispaa ya Bukoba wamefunguliwa Kesi ya Uhujumu Uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba Mkoani mbele ya Hakimu Mfawidhi Janeth Massesa.

Washtakiwa wamesomewa Makosa ya Matumizi Mabaya ya Madaraka, Ubadhirifu, Ufujaji na Matumizi ya Nyaraka ili kumdanganya Mwajiri, Kinyume na Sheria. Mengine ni Kughushi Nyaraka na Kuisababishia Serikali Hasara.

Katika Kesi ya Msingi, Watuhumiwa wote Wanashtakiwa kwa kukusanya na Kufuja Mapato ya Manispaa ya Bukoba kwa manufaa yao, huku wakiidanganya Mamlaka kuingiza Fedha hizo Benki wakati wakijua kuwa ni uongo.

Washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote kwasababu Mahakama hiyo haina Mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, hivyo wamepelekwa Rumande hadi Oktoba 4, 2023 Shauri lao litakapotajwa tena.
 
Back
Top Bottom