Designer_3434
JF-Expert Member
- Dec 4, 2015
- 4,746
- 3,702
Pole kwa wafiwa.
Acha kuleta uchama kwenye haya mamboPoleni sana wana Ngara na Watanzania wenzetu. Nikiangalia hali za hao watoto hao naamini ule usemi kuwa CCM itatawala milele navuta picha za wazazi wao nachoka.
Takribani wanafunzi 3 wameripotiwa kufariki dunia mpaka sasa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mlipuko wa bomu wilayani Ngara.
Diwani wa Kata ya Kibogora wilayani humo, Ndg Adronizi Burindoli ameeleza kuwa jitihada za kuokoa uhai wa majeruhi zinaendelea..
Taarifa zaidi zitafuata...
Mwendelezo:
========
=> Wanafunzi sita wa shule ya msingi Kihinga mkoani Kagera Kaskazini Magharibi mwa Tanzania wamefariki dunia na wengine zaidi ya 25 wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu wakicheza.
Kamanda wa polisi wa mkoa, Augustine Orom huo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari wananchi wamejitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi.
Kwa mujibu wa Dokta Mariagoreth Fredrick ambaye ni mganga mkuu hosipitali ya Rulenge, amethibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi ambao baadhi wako katika hali mbaya na tayari wanapatiwa matibabu.
"Tulionao hali ya sio nzuri. Wengine wameumia matumbo, wengine wamechanika bandama, wengine wamevunjika miguu, wengine vichwa vimepata majeraha, wengine wameumia macho." Dokta Mariagoreth ameiambia BBC.
Inaelezwa kwamba kabla ya kulipukiwa na kifaa hicho kinachoarifiwa kuwa ni bomu, wanafunzi hao walikuwa wanakichezea.
=> Mganga wa Hospitali ya Rulenge wilayani Ngara, Kagera Sister Mariagoreth Fransis amesema wamepokea majeruhi 45 waliotokana na mlipuko unaodhaniwa kuwa ni bomu. Kati ya majeruhi hao, 13 wamejeruhiwa vibaya na wawili wamefariki
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya msingi Kihinga,iliyopo wilayani Ngara mkoani Kagera walionusurika wakiwa Hospitali ya misheni Rulenge wilayani humo.
Madaktari wa Hospitali ya Mission Rulenge wakiendelea na Matibabu kwa Majeruhi.
Kamanga wa Jeshi la Polosi mkoani Kagera Agustino Olomi amesema chanzo cha wanafunzi hao kujeruhiwa kwa bomu ni zoezi la kuuza vyuma chakavu ambapo mwanafunzi aliliokota na kuja nalo shuleni ili alipeleke kwa mnunuzi na kupewa madaftari.
Hata hivyo Kamanda wa Kikosi cha Kulinda mipaka cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wilaya ya Ngara ,Meja TR Mutaguzwa amesema Bomu hilo lilikuwa na vipande 36 na lingelipukia ndani ya darasa wangeleta athari zaidi .
Hivi huyo mama alienda leba kukuzaa si bora angekutupa jaani tu kwa akili hiziWatakuwa ni ccm tu hao
Maana kazi imewashinda
Loo!!!! mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi Amen, Habari mbaya na ni msiba mkubwa. Mungu awape wazazi moyo wa subira. Nashauri elimu itolewe kwa wananchi kuhusu kuokota vitu tusivyivifahamu vizuri, elimu hii itolewe mashuleni pia hasa katika maeneo yaliyoathirika na ujio wa wakimbiziMambo ya wakimbizi hayo.