Kagasheki Ni shujaa aliyewfia Vitani

Jun 21, 2013
21
0
Bado naamini kuwa waziri aliyejiuzulu, ni mtu muhimu sana ndani ya mapambano dhidi ya ujangili ulioundiwa ngome imara. Yawezekana Tanzania isimpate shujaa kama huyu milele. Ni shujaa aliyeangamizwa na oparesheni yake mwenyewe. Operesheni tokomeza majangili ikamgeuka na kuwa operesheni tokomeza Kagasheki. Nakutia Moyo shujaa uliyeuawa vitani. Wameua mwili wako lakini naamini wameshindwa kuua uzalendo wako mtukuka! Kwa tafakuri pevu, vita yako takatifu imenajisiwa na kuonekana si kitu. Bunge letu tukufu kwa kusukumwa na upofu wa kura za mwaka 2015 limeshughulikia matawi na sio tatizo lenyewe! Wakati kamati ya uchunguzi ilipaswa kuja na majibu ya kwa nini wale waliotumwa na kagasheki kupigana vita takatifu wameigeuza kuwa vita ya kishetani, tume hiyo imekuja na majibu ya matokeo ya uasi wa vita takatifu iliyoasisiwa na mheshimiwa Kagasheki. Wabuge wetu wakatumia bunge kama eneo la kuhakikishia usalama wa kura zao! Vita takatifu imepoteza udhu!
 

ndetichia

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
27,732
2,000
akafie mbele huyu mzee itabidi ujiulize kina sana kwa nini ajiuzulu sasa..
 

Mapi

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
6,853
1,250
unamtetea kwakuwa unaamin alkuwa aktenda kazi kwa usahihi? Kama ndivyo kama kiongoz anaejua wajibu wake kwanini kajiuzulu baada ya mambo kufka bungeni? Naamin yaliyosomwa bungeni jana ktk taarifa ya kamati si mageni kwake kwani taarfa zote za yaliyotokda alkuwa nazo hvyo angejitazama mapema na kung'atuka... kumuona safi sahv wakat alishafunika kombe ni kujitia upofu wa lazima
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom